Thursday, July 27, 2017

JE, KUTAKUWA NA NDOA MBINGUNI?

Image may contain: 2 people, text and outdoorNdoa ni nini?
Katika tafsiri za kisheria Ndoa inatambulika kama mkataba wa kisheria kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke ambao unaweza kuvunjwa wakati wowote. Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
Katika imani ya kikristo, Ndoa inaweza kutafsiriwa kama “AGANO KATI YA MWANAMKE NA MWANAMUME AMBAO WAMEKUSUDIA KWA HIARI KUAMBATANA NA KUISHI PAMOJA KAMA MKE NA MUME KWA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAO.” Jambo la msingi kulitambua hapa ni kwamba Ndoa ya kikristo ni AGANO. Kuna tofauti kubwa kati ya kile kinachoitwa “AGANO” na “MKATABA” kimsingi agano ni zaidi ya mkataba kwa namna nyingi.
Biblia inatuambia, "Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama Malaika mbinguni" (Mathayo 22:30).
Hili lilikuwa ni jibu la Yesu alipokuwa akijibu swali la kuhusu mwanamke ambaye alikuwa ameolewa mara nyingi katika maisha, yeye ataolewa na nani mbinguni (Mathayo 22:23-28)?
Ni wazi kwamba, hakutakuwa na kama ndoa mbinguni. Hii haimaanishi kwamba mume na mke hawatambuana mbinguni. Hii pia haina maana kwamba mume na mke hataweza kuwa na uhusiano wa karibu mbinguni. Neno la Mungu linatuonyesha ni kuwa, mume na mke hawataoana tena mbinguni.
Kuna uwezekano mkubwa zaidi, hakutakuwa na ndoa mbinguni kwa sababu hatutajitaji ndoa. Wakati Mungu alianzisha ndoa, alifanya hivyo kutimiza mahitaji fulani.
Kwanza, aliona kwamba Adamu alikuwa na haja ya mwaharusi. "Mungu Bwana akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" (Mwanzo 2:18).
Hawa alikuwa suluhizo kwa tatizo la upweke wa Adamu, kama vile haja ya kuwa na "msaidizi," mtu ambaye atakaa pamoja naye kama rafiki na kutembea naye katika maisha. Mbinguni, hata hivyo, hakutakuwa na upweke, wala hitaji lolote la wasaidizi. Tutazungukwa na wingu la umati wa waumini na malaika (Ufunuo 7:9), na mahitaji yetu yote yatatimizwa, ikiwa ni pamoja na haja ya urafiki.
Pili, Mungu aliumba ndoa kama njia ya uzazi na kujaza dunia na binadamu. Mbinguni, hata hivyo, mbinguni haitajazwa na uzazi. Wanaoenda mbinguni hufika huko kwa imani katika Bwana Yesu Kristo; hawataumbwa huko kwa njia ya uzazi. Kwa hiyo, hakuna kusudi kwa ndoa mbinguni kwa vile hakuna uzazi au upweke.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW