Thursday, June 14, 2018

BARAKA ZA YESU KRISTO MUNGU MKUU


Baraka huleta “furaha, hali njema, au ufanisi.” Kila baraka ya kweli na yenye kudumu hutoka kwa Bwana.
Mithali 10:22 Inatuambia; "Baraka ya Bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo."
Kuna uhusiano mkubwa na wa moja kwa moja kati ya baraka ya Bwana na maisha yenye utajiri wa kweli.
(Yakobo 1:17) Yeye huwabariki wanadamu wote, hata wale wasiomjua. Yesu alisema hivi: “Yeye hufanya jua lake lichomoze juu ya watu waovu na wema na kufanya mvua inyeshe juu ya watu waadilifu na wasio waadilifu.” (Mathayo 5:45) Hata hivyo, Mungu huwaonyesha hangaiko la pekee wale wampendao.—Kumbukumbu la Torati 28:1-14; Ayubu 1:1; 42:12.
Wako watu wengi siku hizi wanaotafuta utajiri kwa njia ya kijiunga na taasisi za siri za kishetani kama za Ki-Masonic. Wengine wamepata umaarufu mkubwa kwenye fani za sanaa ya maigizo, uimbaji, mitindo nk kwa msaada wa taasisi hizi. Wengine ni wafanya biashara wakubwa, wanasiasa wakubws kwa nguvu hizi za giza.
Mungu anafanya kazi zake Kwa mpangilio. Kumbukumbu La Torati 11:27-28 inasema Kama ukimtii Mungu, utapokea Baraka lakini usipomtii Mungu laana itakujia,
Tunawezaje kupokea baraka za Mwenyezi Mungu? Kwanza, tunahitaji kusitawisha sifa zinazompendeza. (Kumbukumbu la Torati 30:16, 19, 20; Mika 6:8) Mifano ya watumishi watatu wa zamani wa Yehova itatusaidia kuelewa jambo hilo.
Anza kufuata mpangilio wa Bwana maishani mwako. Imani ndio msingi.
Marko 11: 22 Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu.
23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Anza kuamini unayo sema na usiogope wala kuwa na shaka moyoni mwako, HAKIKA UTAYAPOKEA NAYO YAKUWA YAKO.
Shakom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW