Friday, June 8, 2018

ROHO SABA ZA MUNGU

Image may contain: text
Kwanza tuanze na maana ya namba Saba Kibiblia:
Namba Saba hutumiwa mara nyingi kumaanisha ukamilifu. Kwa mfano, Waisraeli waliagizwa na Mungu kuzunguka jiji la Yeriko kwa siku saba, na kuizunguka mara saba katika siku ya mwisho. (Yoshua 6:15) Biblia ina mifano mingi ambapo namba saba imetumiwa kwa njia hiyohiyo. (Mambo ya Walawi 4:6; 25:8; 26:18; Zaburi 119:164; Ufunuo 1:20; 13:1; 17:10) Yesu alipomwambia Petro kwamba amsamehe ndugu yake “si, Mpaka mara 7, bali, Mpaka mara 77,” kurudia namba 7 kulionyesha kwamba alipaswa kuendelea kusamehe “bila kuacha”.—Mathayo 18:21, 22.
Ufunuo 1:4 inasema kwamba Roho Saba ziko mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ufunuo 3:1 inaonyesha kwamba Yesu Kristo "anashikilia" roho saba za Mungu. Ufunuo 4:5 unaunganisha roho saba za Mungu na taa saba zinazowaka zilizo mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ufunuo 5:6 hubainisha roho saba na "macho saba" ya Mwanakondoo na inasema kwamba "zimetumwa duniani kote."
Mtu mwenye Roho zote saba za Mungu, anaitwa amejaa Roho mtakatifu pasipo kipimo, Amejaa utimilifu wa Mungu
Roho saba ni “jinsi” saba za “tabia” na “udhirihisho” wa ukamilifu wa Roho ya Mungu katika nafsi zake zote tatu. (Isaya 11:1-3).
Kama Yesu ilivyoandikwa “yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo” (Yohana 3:34).
Yesu alijaa roho zote saba za Mungu katika ukamilifu wa udhihirisho wake.
Sasa Nasisi Mungu ametutaka tujae Roho wake pasipo kimipo. Kama alivyosema “msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roh”(Efe 5:18).
Hapo asemapo ujazwe Roho haimaanishi Roho anakuwa amekuacha.
Bali Anataka ujae ukamilifu na utendaji wa Roho zote saba za Mungu.
Mtu mwenye udhihirisho wa Roho ya Hekima na Maarifa unakuwa amejaa Zaidi kuliko mtu mwenye udhihirisho wa Roho ya Hekima Pekeyake.
Biblia, na hasa kitabu cha Ufunuo, inatumia namba 7 kutaja ukamilifu na kukamilika. Ikiwa hiyo ndiyo maana ya "saba" katika "roho saba," basi haimaanishi roho saba za Mungu tofauti, lakini badala yake Roho Mtakatifu kamili na mkamilifu.
Mtazamo mwingine ni kwamba roho saba za Mungu zinarejelea viumbe saba vya malaika, labda serafi au makerubi. Hii ingekuwa sawa na viumbe wengine wengi wa malaika ambao wanaelezewa katika kitabu cha Ufunuo (Ufunuo 4:6-9, 5:6-14; 19:4-5).
Vivyo hivyo, katika Isaya 11:2, inasema, "Na Roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA." Hii labda inaweza kuelezea roho saba za Mungu: (1) Roho ya BWANA, (2) Roho ya hekima, (3) Roho ya ufahamu, (4) Roho ya shauri, (5) Roho ya uweza, (6) Roho ya maarifa, (7) Roho ya kumcha Bwana. Biblia haituambii hasa ni nani/nini roho saba, lakini tafsiri ya kwanza, kwamba ni Roho Mtakatifu, inaonekana ya uwezekano zaidi.
Basi tumjue Mungu sana, ili haya mambo yawekwe wazi kwetu. Naye Bwana ni mwaminifu, kama alivyosema “hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo”(Wafilipi 3:15)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW