Monday, June 4, 2018

QURAN NA HADITH ZATHIBITISHA UTUME WA PAULO



1. UTUME WA PAULO KWA MUJIBU WA QURANI TUKUFU
Kwa kuanza naomba niwakumbushe Waislam kwambu uislamu una sifa zifuatazo. (swifat ul I’iman mufaswalu)
1. Imani juu ya Mungu.
2. Imani Juu ya Malaika wa Mwenyezi Mungu.
3. Imani juu ya Vitabu vya Mwenyezi Mungu
4. Imani juu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu
5. Imani juu ya Kheri na Shari za Mwenyezi Mungu.
6. Imani juu ya Siku ya Mwisho.
Kwa mujibu wa Mada ya leo. Nitajikita juu ya Imani juu ya Mitume.
Waislamu wanaamini kwamba, wapo Mitume wapatao 124,000. Kati ya hao. ni 25 tu ndiyo ambao mtume Muhammad (S. A. W) aliweza kupewa habari zake. kama tunavyosoma.
[ AN-NISAAI – 164 ]
Na Mitume tulio kwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia. Na Mwenyezi Mungu alinena na Musa kwa maneno.
Hii inamaana kwamba Muhamad alifahamu kidogo sana kuhusu habari za mitume. yaani kama ni asilimia ni 0.0002 ya uelewa wake juu ya mitume. na huo ndio uelewa wa waislamu wote linapokuja swala la mitume. Hata hivyo. Allah s.w alikwisha kumwelekeza mtume mahala pa kupata nuru zaidi aliposema.
(YUNUS – 94)
Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.
Hivyo kwa habari za mitume, karibia mitume wote aliosimuliwa muhammad wamo kwenye Biblia. Basi kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya mada yetu leo twawagabarisha waislamu juu ya utume wa Paulo.
Hata hivyo ukisoma Quran kwa uangalifu utagundua kuwa Habari za Paulo zimeelezwa vizuri humo.
Chunguza aya hii.
(YA-SIN – 13-14)
Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa.
Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu.
Aya hii inaeleza kisa cha WAJUMBE WA MWENYEZI MUNGU.
Wafasiri na wanazuoni mfano Shekhe Balwani, Yusufu Ali wamefasiri aya hii na kusema mji huo walikotumwa wajumbe ni ANTIOKIA.
Ibin Kathir katika tafsir yake anasema wajumbe hao ni Yohana, Simoni na Paulo.
Na hapa namnukuru ibn Kathir.
Imesimuliwa na Ibn Jurayj kutoka kwa Wahb bin Sulayman, imepokelewa na Shu`ayb Al-Jaba’i, “Majina wajumbe wawili wa waliotumwa mwanzo ni Simoni na Yohana na jina la wa tatu ni Paulo. Na mji huo ulikuwa Antiokia” , and the city was Antioch. Na wakasema (kwa watu wa mji huo) “hakika sisi tumetumwa kwenu kama wajumbe”, hii ina maanisha “Wajumbe kutoka kwa Allah aliyewaumba nyinyi na anayewaamrisha mumwabudu yeye peke yake na msimfanyie washirika.” Qatada amesema walikuwa ni wajumbe wa Masihi Isa bin Maryam (a.s) waliotumwa kwa watu wa Antiokia. Wakasema “Ninyi ni wanadamu kama sisi…ni kwa vipi munaweza kupokea ufunuo wakati nyie ni wanadamu na sisi tu wanadamu kama nyie, kwanini sisi hatupokei ufunuo kama nyie?” hivi ndivyo ilivyokuwa kwa watu wa mataifa mengine walivyosema ‘hatuamini’, kama vile Allah anavyotuambia katika sura ya 64:6 , as Allah has told us in the Ayah: That was because there came to them their Messengers with clear proofs, but they said: “Shall mere men guide us!” (64: 6) “Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: Hivyo binadamu ndiyo atuongoe? Basi wakakufuru na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao…”
Hivyo twaona kuwa hoja ya kumkataa Paulo ni uzushi wa hivi karibuni. Waislamu, wasomi na Maulamaa wa kale hawakuwa na hoja hii ya kumkataa Paulo.
2. UTUME WA PAULO KWA MUJIBU WA HADITHI ZA MTUME.
Baada ya Kuona Ushahidi wa vitabu vitakatifu juu ya utume wa mtume Paulo. Sasa tugeukie hadith za mtume Muhammad. na kwa nini tugeukie hadithi? Ni kwa ushauri unaotolewa na Allah s.w ndani ya Quran yenyewe.
[ AN-NISAAI – 59 ]
Enyi mlio amini! Mt’iini Mwenyezi Mungu, na mt’iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.
Katika kitabu kiitwacho SIRAT NABAWIYA. Kilichoandikwa na Ibn Hisham, aliyekuwa mwanafunzi wa ibn Ishak. Katika juzu ya 4 ya kitabu hicho uk 140 tunakuta Muhammad anaorodhesha majina ya Wanafunzi wa Yesu. na anawagawa katika mafungu 2. la kwanza ni wale waliomfuata wakati wa uhai wake na wale waliomfuata baada yakuwa amepaa juu. Muhammad anaeleza kila mmoja wa wanafunzi hao na mahala walikotumwa, kuhusu Paulo anaeleza kuwa Yeye alitumwa Rumi.
Na hapa namnukuru ibn Hisham.
*أسماء رسل عيسى عليه السلام*
أسماء رسل عيسى عليه السلام
قال ابن إسحاق ‏:‏ وكان من بعث عيسى بن مريم عليه السلام من الحواريين والأتباع ، الذين كانوا بعدهم في الأرض ‏:‏ بطرس الحواري ، ومعه بولس ، وكان بولس من الأتباع ، ولم يكن من الحواريين ، إلى رومية ، وأندرائس ومنتا إلى الأرض التي يأكل أهلها الناس ، وتوماس ، إلى أرض بايل من أرض المشرق ، وفيلبس إلى أرض قرطاجنة ، وهي أفريقية ؛ ويحنس إلى أفسوس ، قرية الفتية أصحاب الكهف ؛ ويعقوبس إلى أوراشلم ، وهي إيلياء قرية بيت المقدس ، وابن ثلماء إلى الأعرابية ، وهي أرض الحجاز ؛ وسيمن إلى أرض البربر ، ويهوذا ، ولم يكن من الحواريين ، جعل مكان يودس ‏.‏
Majina ya Mitume wa Yesu Masihi:
“Amesema ibh Is-hak: walikuwa mionguni mwa wanafunzi wa Yesu (amani iwe juu yake) wale waliomfuata wale waliokuwa baada yake duniani: Petro Mwanafunzi wa Yesu, na pamoja naye alikuwepo Paulo miongoni mwa wafuasi, Paulo hakuwa miongoni mwa wale wanafunzi wa Yesu. Naye (Paulo) alitumwa Rumi. Na Andrea naye alitumwa katika nchi ambayo wakazi wake wanakula watu. Na Tomaso alitumwa katika nchi ya Babeli katika nchi za mashariki. Na Philipo alitumwa katika nchi pande za Afrika, na Yohana alitumwa Efeso na Yakobo alitumwa Yerusalemu na Batholomeo alitumwa Uarabuni katika nchi ya Hijaz. Na Simoni alitumwa Baribari.”
Yashangaza kuona kuwa licha ya ushahidi mkubwa namna hii waislamu wa leo (hasa wanaharakati) wameamua kufumbia macho ukweli huu na kuanza kudanganya watu. ama kwa maksudi ama kwakutokujua. SWALI NI HILI. wanafanya hivyo kwa faida ya nani?
Rafiki yangu mwislamu, napenda kukutahadharisha kwamba, shetani ni mjanja, siku zote atakuja kwa hila akiwatukia waalimu wa uongo, wengine watakuja kana kwamba ni watetezi wa dini kumbe ndiyo waharibifu wakubwa wa dini.
Allah s.w anasema ndani ya Quran kuwaambia waislamu
[ AL – BAQARA – 136 ]
Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.
Unaona kwamba Allah s.w amewaagiza waislam siyo tu kuamini wale kitume 25 waliotajwa ndani ya Quran lakini pia wanapaswa kuamini w aliyoteremshiwa wajukuu wa Yakobo, PAULO PIA NI MJUKUU WA manabii YAKOBO. Lakini siyo hivyo tu, Allah s.w amewataka manabii waislamu kuamini walioteremshiwa “manabii wengine”. PAULO PIA NI MIONGONI MWA MANABII WENGINE.
Hivyo kumpinga Paulo ni kuipinga imani, kupinga Quran na Mwinsho kumpinga Allah mwenyewe. NA HUU NDIO UKAFIRI ULIOKITHIRI.
Je kuha hadithi yoyote ya Mtume mahali ambapo, Mtume aliwatahadharisha masahaba zake au Waislamu kwa ujumla juu ya Mafundisho ya Paulo?
Hapana, badala yake tunaona Muhammad yeye mwnyewe alinukuru mafundisho ya Paulo na akiuita ni ujembe kutoka kwa Mwenyezi Mungu‏
“Imesimuliwa na Abu Huraira, Mjumbe wa Allah (s.a.w) alisema; Mwenyezi Mungu kasema, ‘Nimewaandalia waja wangu ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio halijawahi kusikia wala moyo wa mwanadamu hauwezi kuyafikiri”
Hivyo twaona kuwa hoja ya kukataa utume wa Paulo hainamsingi wa mafundisho ya vitabu vitakatifu, ni upotoshaji wa waalimu wa dini wanaotafuta masilahi yao binafsi.
Shalom,
Loud Cry Ministries by Permission
Max Shimba Ministries Org

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW