Wednesday, August 10, 2016

JE ALLAH WA WAISLAMU NA MUNGU WA WAKRISTO (YEHOVA) NI MMOJA? (SEHEMU YA KWANZA)


UTANGULIZI.
Imekuwa ni kawaida sasa kwa miaka zaidi ya ishirini hivi, kusikia katika mihadhara inayoendeshwa na wahadhiri wa dini ya Uislamu, ambayo imeenea sehemu mbalimbali Duniani na haswa katika nchi za Africa Mashariki na Kati,(East and Central Africa). Wahadhiri hao hufundisha jamii kupitia Qurani na Biblia kwa kusema kuwa Mungu ni Mmoja tu. Wasema Mungu kwa Kiebrania anaitwa Yehova , kwa Kiarabu Allah, kwa Kiingereza God na kwa Kiswahili ni Mungu. Kwa hivyo wasema Mungu Allah kama Qurani inavyofundisha, ndiye Yehova kama Biblia inavyofundisha. Mihadhara hiyo inayoendeshwa na Waislamu imeenea sana, mfano Nchini Tanzania kuna vikundi vingi na kimoja wapo kinaitwa Al-Marid International Propagation Center. Hawa wameandika katika bango lao kwa kunukuu katika Biblia maneno aliyoandika Mtume Paulo katika Waefeso 4:4-6. Maneno waliyoyanukuu yanasema hivi “Bwana mmoja , Imani moja ….., Mungu mmoja , naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote. Nilipotembelea mkoa wa Morogoro pale mjini, eneo la kiwanja cha ndege nikaona Msikiti mmoja umeandikwa maneno haya ya Waefeso 4:4-6. Na nilipotembelea mji wa Nairobi Nchini Kenya pia nikaona kuna vikundi vingi vinavyoendesha mihadhara na kikundi kimoja wapo kinaitwa Kibera Islamic Propagation Centre. Hawa nao katika bango lao wameandika ujumbe unaosema hivi “Acha Biblia Ijisemee na kunukuu injili aya hii” Yohana 8:32 Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Kwa hivyo utaona kuwa wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia na kusema Allah Sub-Hana Wataala ndiye YEHOVA. Fundisho hili wanalieneza kwa kupitia Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingawa hawajabadili dini wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila mkristo, je, ni kweli Mungu Allah kama inavyotuhadithia Qurani ndiye Yehova kama Biblia inavyotufundisha? Nakusihi fuatilia somo hili kwa makini ili kujua Ukweli……
SEHEMU KUU ZA SOMO HILI NI HIZI……
1. Hoja za waislamu kusema Allah ndiye Yehova.
2. Je, jina la Mungu kadiri ya Qurani na Biblia ni moja?
3. Je, Malaika mkuu wa Allah ndiye wa Yehova?
4. Je, ni nani muumba,Allah au Yehova?
5. Mji aliochagua Allah je, ni sawa na wa Yehova?
6. Allah anavyofundisha kuhusu kujitakasa nafsi je, ni sawa na Yehova?
7. Je, mbingu ya Yehova ni sawa na ya Allah?
8. Mwisho wa wanaomwabudu Allah ni wapi?
:::::::::::::::::::::::SEHEMU YA KWANZA :::::::::::::::::::
1. HOJA ZA WAISLAM KUSEMA ALLAH NDIYE YEHOVA
Wahadhiri wa Dini ya Uislamu wanasema Mungu Allah ndiye Yehova kwa sababu Manabii wa Mungu kadiri ya Biblia na Qurani walifundisha kwa kusema Mungu ni mmoja tu. Na wanasoma aya hizi…
Nabii Musa alivyosema
Kumbukumbu la Torati 6:4
Sikiza ee Israeli; BWANA Mungu wetu BWANA ndiye mmoja.
Nabii Isaya alisema hivi
Isaya 45:18,21
Maana BWANA , aliyeumba mbingu, asema hivi, yeye ni Mungu ,ndiye aliyeumba Dunia na kuifanya ….. si mimi BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi. Mungu mwenye haki , mwokozi hapana mwingine zaidi ya mimi.
Nabii Daudi Alisema
Zaburi 86:10
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, wewe ndiwe mfanya miujiza , ndiwe Mungu peke yako.
Yesu alisema hivi
Yohana 17:3
na uzima wa milele ndio huu wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliye mtuma
Paulo naye Alisema hivi
1 Wakorintho 8:4
Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na yakuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.
Hapa wahadhiri wa Dini ya Uislamu wanasema Manabii wote kadiri ya Biblia wanafundisha kuwa Mungu ni mmoja tu. Je, Muhammad (s.a.w.) alifundisha nini kuhusu Mungu? Wanasoma aya hizi za Qurani……..
Qurani 41:6 Suratul Haa Mym Sajdah (Kusujudu)
Sema; bila shaka mimi ni mtu kama nyinyi. Nimeletewa Wahyi (inafunuliwa kwangu)ya kwamba Mungu wenu ni Mungu mmoja tu……
Hapa wahadhiri wanasema kama vile manabii wote walifundisha Mungu mmoja ndivyo ilivyo fundisha Muhammad.
Qurani 29:46-47 Suratul Al- Ankabuut (Buibui).
Wala mshibishane na watu waliopewa kitabu (kabla yenu) ila kwa yale (majadiliano) yaliyo mazuri, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni :tunaamini yaliyoteremshwa kwetu, na yaliyoteremshwa kwenu. Na mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja : nasi ni wenye kunyenyekea kwake. Na namna hivi tumekuteremshia kitabu (hiki cha Qurani) basi wale tuliowapa kitabu (kabla ya hiki kama taurati na injili) wanakiamini (hiki kitabu ulichoteremshiwa kwani hakipingani na hivyo walivyoteremshiwa). Na miongoni mwa hawa (Waarabu wasiokuwa na Kitabu chochote)wako wanaokiamini. Na hawazikatai aya zetu isipokuwa wale wanaotaka kuficha haki.
Hapa wahadhiri wa kiislamu wakisha soma aya hizi husema vitabu vya Torati na Injili havipingani na Qurani, na vitabu hivyo walipewa Wayahudi na Manasara(yaani Wakristo) na Mungu wa Waislamu na Wakristo ni mmoja tu.
Je, hoja hii ni kweli? Nitaijibu huko mbele.
Majibu kuhusu Mungu mmoja
Ukitazama kwa haraka haraka namna wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu wanavyolinganisha aya za Qurani na Biblia unaweza ukashawishika kuamini hicho wanachokifundisha, lakini ni vyema tukajifundisha kwa undani kadiri ya Qurani na Biblia na kisha tuone kama kuna ukweli juu ya hayo mafundisho yao, ya kusema Allah Sub-hana Wataala ndiye Yehova.tukumbuke kuwa Mungu tunayeabudu alitutahadhalisha sana Wakristo kwa kusema hivi…
Kutoka 20:1-3
Mungu akanena maneno haya yote akasema Mimi ni BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa usiwe na Miungu mingine ila mimi.
Tahadhari hii Ya Mungu wetu ya kusema usiwe na Miungu inamaanisha kuwa Miungu mingine yenye kuabundiwa na watu ipo. Kwa sababu katika Biblia neno Mungu Kiebrania“Elohim” Kiyunani "Theos" limetanjwa mara 3979 lakini pia miungu ya uongo imetanjwa mara 271. baadhi ya miungu hiyo ya uongo ni hii
mungu Dargoni Waamuzi16:23
mungu Baal Wafalme 18:21
mungu mke wa Waefeso aitwae Artemi Matendo 19:24-28.
Aidha tusomapo Qurani pia imetaja miungu mbalimbali iliyokuwa inaabundiwa kule Makka nayo ni hii;
Qurani 53:19-20,23 Suratul An- Najm (Nyota).
19. Je, mumewaona Lata na Uzza? 20. Na Manata (mungu wenu) mwingine wa tatu (kuwa ndio waungu hao badala ya mwenyenzi mungu)? 23. hayakuwa haya (majina ya Lata mungu mwanamke na Uzza mungu mwanamke mwenye enzi. Na Manata mungu mwanamke anayeneemesha ila ni majina tu mliowapa nyinyi na baba zenu…..
Hivyo basi tunaona kuwa miungu yenyewe kuabudiwa ni mingi na kila mwenye kuabudu humtegemea huyo mungu wake na kusema ni mmoja. Mfano waliyemuabudu Dagoni walisema ni mungu mmoja, waliyemwabudu Baali walisema ni mungu mmoja , waliyemwabudu Artemi walisema Artemi ndiye mungu mkuu.
Kadharika Manabii.
walimtumikia Mungu mmoja aitwaye Yehova, naye Muhammad alimwabudu "mungu" mmoja aitwaye Allah. Ninachotaka kukifundisha kwa jamii ijue je, huyo Allah ndiye Yehova?,
USIKOSE SEHEMU YA PILI YA SOMO "Je, jina la Mungu kadiri ya Qurani na Biblia ni moja?"
BARIKIWA SANA

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW