Friday, July 14, 2017

KWANINI TUNASEMA YESU NI MUNGU MKUU?

Image may contain: text


Tito 2:13 “Tukilitazamia tumaini lenye mafunuo ya KRISTO YESU MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU”.
YESU NI MUNGU aliyejifunua katika mwili Warumi 9:5 “Na katika hao alitoka KRISTO KWA NJIA YA MWILI, NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE, MUNGU, MWENYE KUHIMIDIWA MILELE. AMINA.
Mhalifu msalabani alimwita YESU Mungu na kumuomba YESU atakapokuwa katika ufalme wake amkumbuke mharifu huyo”. Luka 23:39-43. Yesu hakukataa kuwa SI MUNGU bali alisema, Amini nakuambia leo hivi, utakuwa pamoja nami peponi.
Tumeanza kwa aya inayo kiri kuwa Yesu ni Mungu Mkuu. Je, kwanini tunamwita Yesu Mungu Mkuu?
Yohana 3:30 “Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya vyote. Yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani, yeye ajaye kutoka mbinguni yuu juu ya yote”.
Aya inatuambiwa kuwa Yesu yupo juu ya yote, kwamaana ametoka Mbinguni.
YESU ANATUMILIKI WATU WOTE, WAFU NA WALIO HAI
Warumi 14:9 “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia”. Neno kumiliki ni kutawala sifa ya kutawala ni sifa ya Mungu pekee.
Warumi inaendelea kutuambia kuwa Yesu anatumiliki watu wote, wafu na walio hai. Je, nani mwenye uwezo huo kama sio MUNGU MKUU? Kumbe hata Muhammad na Allah wanamilikiwa na Yesu Mungu Mkuu.
YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WALIMWENGU (WATU) WOTE.
Ufunuo 18;8 “Kwasababu hiyo, mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti na huzuni na njaa naye atateketeza kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“. Tene ndiye atakaye ihukumu Dunia yote “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote,bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.
Mathayo 25:31-32 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake,naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi” .
Matendo 10:42 “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( Warumi 2:16 ) “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na injili yangu,kwa Kristo Yesu“.
2 Timotheo 4:1 “Nakuagiza mmbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu,atakayewahukumu waliohai na waliokufa;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.
Ndio maana tutaendelea kusema kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, maana hayo yote yanawezekana kwa Yesu Pekee ambaye ni Mungu Mkuu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW