Friday, July 14, 2017

NANI KAMPA UTUME NA UNABII MTUME MUHAMMAD? SEHEMU YA PILI.

Image may contain: 1 person, smiling, text


Huu ni uhakikisho kwamba Muhammad hakupewa utume na Mungu wa israeli, sababu ukisoma pia kitabu chawakeze wakubwa na wanaweukurasa wa 12 kuna maneno yanayorudilia haya ambayo tumeyasoma hapo juu yakisema hivi:
Nanukuu,
Basi mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe, akamwadithia na palepale homa kubwa kabisa ikampanda, akataka afunikwe na maguo mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema: «Najihofia nafsi yangu kuchezewa na mashetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga!»
Hapo katika pango la Jabal Hira ndipo waislamu na qura’n hudai kwamba ndipo alipopokea Wahyi wa qura’n, utume na unabii.
Lakini twaona na kusikia maneno ya mtume mwenyewe yanashuhudia alichokutana nacho pangoni ambacho ni shetani sababu hata Biblia Takatifu hushuhudia hivi:
1Yohana 1:3
Hilo tuliloliona nakulisikia, twalihubiri na nyinyi: ili na nyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.»
Ukweli ni kwamba huyu shetani aliyekutana na maskini Muhammad pangoni hakumpa hata utume wala unabii isipokuwa mkewe Hadidja na Bwana Waraqa bin Naufal ndio waliomshauri Muhammad kujibashiria kuwa yeye ni mtume wa uma kama tulivyo soma katika kurasa ambazo tumekuwekea picha zake hapo juu.
Ikumbukwe vizuri kwamba haya yalitokea wakati ambao uislamu na qura’n havikuwepo kwanza na historia ya maisha ya mtume kinamtambuwa Waraqa bin Naufal kama mtu ambaye hakuwa naabudu sanamu za waarabu wenzake! Lakini yeye ni nani kutowa ruhusa kwa mtu kama Muhammad ili ajibashirie utume? Hapo kuna mashaka mengi.
Vipi kwa Hadidja?
Mjane aliyefiwa na waume wake 2 kisha akajichukulia Muhammad kama mume wake wa tatu, Huyu ndiye aliyeingia wa kwanza katika imani potofu ya uislamu. Lakini natujiulize hili swali: « je, inakuwaje mtu ambaye bado ni mkafiri kutowa utume kwa mwingine kabla yeye hajajuwa ujumbe wa mtume huyo nakuuamini?» Bila shaka jibu laweza kuwa ni upumbavu wakupindukia.
Hebu tuone qura’n inavyosema kuhusu kupewa utume, kupewa wahyi au ujumbe,
Qr.7:144 au surat Al-A’raaf 144
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteuwa wende kwa watu na ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukuwa niliyikupa na uwe katika wale wanaoshukuru.
Kwanini Allah Subhanau Watahallah hakufanya hivihivi kwa Muhammad s.a.w katika pango la Jabal Hira?
Swala la Muhammad kuwa ni mtume katika maandishi ya qura’n na hadithi zote siyo hoja lakini hoja tu ni «Kapewa na nani huo utume?»
Tuchunguze na kuchimbua tena hili andiko la Qura’n,
Qr. 13:43 au surat Ar-raa’d 43
Na waliokufuru wanasema kuwa wewe si mtume,
Sema, Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya kitabu.
Anayemwambia Muhammad kusema ni ALLAH wake na wa waislamu wote.
Anayedaiwa kuwa shahidi bain aya ALLAH na waislamu ni Mwenyezi Mungu.
Anayedaiwa kuwa ni mwenye ilimu ya kitabu ni Jibril.
Kwa wazi kabisa ni kwamba Allah wa awislamu ni tofauti na Mwenyezi Mungu sababu anamtowa kuwa shahidi kati yake na wafuasi wake yaani waislam. Je, Mwenyezi Mungu anasemaje kuhusu miungu mingine?
Isaya 42:8
«Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.»
Isaya 48:11
«Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.»
Kumbukumbu 18:18
« Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.
Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.»
Uislamu na qura’n wanadai aliyetabiriwa na nabii Musa kwamba ni Muhammad s.a.w lakini kama tulivyochunguza katika yale matoleo ya kwanza ni kwamba sio Muhammad bali alikuwa Yesu ambaye angekuwa masihi na Kristo wa dunia yote! Kwa sababu hizi chache tu:
ALLAH S.W NA MUHAMMAD S.A.W
YEHOVA MUNGU NA YESU KRISTO
mungu asye na jina kamili
Qr. 17 au surat Bani Israil 110 (Wana wa Israil)
Sema; muombeni (Mwenyenzi Mungu) kwa (jina la) Allah au muombeni (kwa jina la) Rahman. Kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa). Kwani ana majina mazuri mazuri………
Mungu anayejulikana
Kutoka 6:2-3,
Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, mimi ni YEHOVA;
Nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
mungu wao ana maadui wake ambao ni wakristo na wayahudi
Qr. 4:51 na 57 (surat Al Maida)
Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika hao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
Wafuasi wote wa Allah wanangojea moto wa jehanam kisha waokolewe waislam baadaye kutoka motoni
Qr. 19:70-72
Tena hakika sisi tunawajuwa vyema Zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo
Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako mlezi ambayo lazima itimizwe. Kisha tutawaokoa wale waliomcha Mungu; na tutawaacha madhalimu humo hali wamepiga magoti motoni.
Mungu wetu ni mwenye rehema na wafuasi wake hatuna adui
Mathayo 5:43-44
Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Kwetu wakristo sivyo ilivyo!
Zaburi 9:17
Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
Luka 16:23
Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
Allah wao ataionja jehanamu pia
Qr. 50 au Surat Qaf 30 (kuapa)
Siku tutakayoiambia Jahanamu, ‘Je! Umejaa?’ Nayo itasema ‘Je kuna ziada (zaidi? Naije tu!
Imesimuliwa na Anas kuwa: mtume alisema watu watatupwa jahanamu, Naye Allah ataiuliza jahanamu akisema je umejaa nayo jahanamu itasema kwani kuna nyingine zaidi na ije tu? Mpaka Allah atakapo ingiza mguu wake nayo jahanamu itasema inatosha! Inatosha
Dhawabu ya wakristo ni uzima wa milele
Yohana 14: 1-4
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia.
Hizi ni sababu ndogo kutoka katika zile sababu zaidi ya 100 ambazo ziko wazi kabisa kama Muhammad kapewa utume na yeye mwenyewe kwa shauri la mkewe Hadidja na Bwana Waraqa bin Naufal.
Twataka tukupe baadhi ya mashaka katika qura’n
# Katika Qura’n sur aya 3, aya yake ya 7 (surat Al I’mran) panasema kwamba kuna aya nyingi katika Qura’n ambayo mwanadamu hana uwezo kuzisoma na kuzitafsiri isipokuwa Allah.
# Katika sura za 11:114, sur aya 17:78-79, sura ya 20:130, na sur aya 30:17-18 za qura’n Allah anasema kwamba kila mwislam analazimika kusali mara tatu kwa siku, lakini katika hadithi za mtume huyo huyo Allah anawalazimisha waislam kusali mara tano kwa siku. Je, Allah hana uamzi moja? Waislam kazi kwenu!
# Katika sur aya 18:86 ya qura’n, Allah hukiri kwa Muhammad kwamba jua hutua katika dimbwi la maji machafu duniani. Je, hiyo ni kweli? Kama Mwenyezi Mungu ni muumba jinsi gani anaweza kufanya makosa kama haya? Na je, Biblia inasemaje kuhusu uumbaji? Soma kitabu cha Mwanzo sura 1 na mbili.
# Katika sura 2:106 na sura 16:101 katika qura’n Allah anasema kama alirekebisha aya katika qura’n na kutangua au kubadilisha aya zingine ili kuweka zilizo bora zaidi. Je mungu ni mtu ili abadilishe neno lake?
Isaya 40:8, «Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.»
Tunazo sababu zaidi tutakazoziweka hadharani katika sehemu zitakazofuata katika siku zinazokuja ili kukusaidia wewe muislam kuufikia wokovu kamili katika Kristo Yesu Bwana wetu na mwokozi wetu.
Twamalizia toleo hili tukikuomba katika upendo wa kristo kuikimbilia mbali sana ibada ya shetani katika dini ya uislamu na kukimbilia kwa Yesu Kristo ili upate uzima wa milele.
Matendo ya mitume 4:11,12
Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
MBARIKIWE NYOTE
Ndugu yako katika Kristo

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW