Sunday, September 10, 2017

JE UNAIJUA HOJA KUBWA NA PEKEE YA WASABATO “SDA” KUHUSU KUSHIKA SABATO? SEHEMU YA KWANZA

Image may contain: text
Iko hoja kwamba Sabato ni amri ya muhimu sana kwa sababu ilitoka moja kwa moja kinywani mwa Mungu tofauti na amri zingine ambazo zililetwa kupitia manabii au mitume.
Katika Agano la Kale Mungu alisema, “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase…Kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.” (Kutoka 20:8,11)
Hoja hii haina uzito kwa sababu kuu mbili:
Biblia kwa ujumla wake ni Neno la Mungu ambalo limetoka kinywani mwake lote. Na maandiko yako wazi kwamba: Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa, apate kutenda kila tendo jema. (2 Tim. 3:16-17).
Na kimsingi maandiko haya, ukisoma kwenye Biblia ya Kiingereza, hayasemi “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu”. Badala yake yanasema: All Scripture is God-breathed (NIV); au All scripture is given by inspiration of God (KJV). Hii ina maana kwamba: Maandiko yote yametokana na pumzi ya Mungu.
Kwa hiyo, hakuna mantiki kusema kwamba andiko hili lina maana zaidi kuliko lile kwa kuwa hili alitamka Mungu mwenyewe. Yote yana nguvu ileile; yote yametoka kwa Mungu yuleyule.
HOJA ZINAZOTUMIWA NA WASABATO KUISHIKILIA SABATO YA MWILINI
1. WANASEMA MUNGU SI KIGEUGEU
Yaani Mungu hawezi kusema alafu akaghairi (Malaki3:6) (Zaburi89:34) (Yakobo1:17)
Ni muhimu kujua Biblia inaposema Mungu hana kigeugeu lazima tujue hana kigeugeu anamaanisha nini?
Mungu hana kigeugeu au habadiliki katika ahadi, yaani Mungu akikuhaidi atakubariki na ukakaa katika njia zake, kubarikiwa ni lazima na hata hivyo akikuhadi kukubariki halafu ukaenda kinyume na mapenzi yake hugeuka na kutokutimiza aliyoyaahidi kwako (1Samweli 2:30).
Tukiyachunguza maandiko yote yanayoelezea kuwa Mungu si kigeugeu utaona chanzo cha maandiko haya ni ahadi (Malaki 3:5-6) Mungu anasema “Nita” maana yake anaahidi mambo kadhaa katika mstari wa 5, na katika mstari wa 6 anaeleza kuwa yeye si kigeugeu katika yale aliyoyaahidi katika mstari wa 5.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

1 comment:

Unknown said...

Mungu alitupa amri zake ili zituongoze kuenenda katika njia zake na tuziishi,na hizo amri ndiyo tabia ya Mungu.
SWALI:
Je yatupasa tuzishike au tuzitunze na kuzitenda amri zake zote,au tuchague baadhitu na zingine tuachane nazo?
Naomba jibu tafadhali.

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW