Sunday, September 10, 2017

JE, UNAYO NEEMA YA YESU KRISTO, MUNGU MKUU?

Image may contain: food
Nini basi maana ya neema? Watu wengi wamekuwa wakiimba ,”Neema, neema imefunuliwa” na kukariri na kuisema Neema ya Bwana (2 WAKORINTHO 13:14) kama Kasuku huku hawajui wayasemayo. Nini basi maana ya neema?
Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa, bila kustahili kutokana na matendo yoyote aliyoyafanya mtu au sifa aliyonayo mtu.
Neema pia, ni uwezo wa kushinda katika tabia na utumishi wa Mungu sawasawa na mapenzi yake, tunaopewa na Mungu bila gharama yoyote au nguvuzetu au kufanyia kazi yoyote.
1. Upendeleo wa kuchaguliwa bila kustahili- Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki mbele za Mungu (WARUMI 3:20). Tangu kabisa amekuwa akimhuzunisha Mungu (MWANZO 6:5-7). Wakati wa Nuhu, watu waliangamizwa kwa Gharika. Wakati wa Musa, Mungu alitaka pia kufuta kabisa kizazi cha Wausraeli na kubaki na Musa tu kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Wakati wote, wanadamu wote wamepotoka na kuoza (WARUMI 3:12). Ni Yesu peke yake tu ambaye siku zote alifanya yanayompendeza Mungu (YOHANA8:29).Alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (WAEBRANIA 4:14-15). Yesu huyu anayempendeza Mungu ndiye aliyekufa msalabani na Baraba aliyekuwa mhalifu mkubwa akafunguliwa. Kama Baraba alivyofunguliwa pamoja na ukosaji wake, kila mwanadamu amefunguliwa, akiamini tu. Mbele za Mungu kila mtu amepimwa na kuonekana amepungua (DANIELI 5:27). Sasa kwa kuamini tu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu pale msalabani, sisi tunaokolewa. Watu wengi hawaokolewi kwa sababu hawajui tunaokolewa kwa neema tu kwa njia ya imani peke yake (WAEFESO 2:5). Kazi aliyoifanya Yesu msalabani imetupa kuirithi mbingu aliyokwenda bila sisi kuifanya. Ni kama ambavyo bondia anavyopigana ulingoni kwa shida kubwa na kasha akishinda na kupewa mamilioni ya fedha, mke wake aliyebaki nyumbani bila kupigana naye atakuwa milionea. Hii ndiyo neema.
2. Uwezo wa kushinda bila kutumia nguvu zetu- Neema ni uwezo wa kushinda dhambi na kumtumikia Mungu apendavyo. Neema ndiyo inayotufundisha (inayotuwezesha) kukataa ubaya na tama za kidunia na kuishi kwa kiasi na haki na utakatifu (TITO 2:11-12; WAGALATIA 2:8). Maisha ya wokovu siyo ya kutumia nguvu zetu au kujitahidi. Uweza wa Mungu unatimilika kwetu katika udhaifu wetu yaani kutokuweza kwetu. Hatupaswi kujitumainia wenyewe katika kufanya lolote (2 WAKORINTHO 1:8-9).
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW