Sunday, September 10, 2017

KIVIPI UTAWEZA KUMJUA MCHAWI?

No automatic alt text available.
Zifuatazo ni dalili zitazokuwezesha kutofautisha baina ya mganga na mchawi. Utakapoona mojawapo ya dalili zufuatazo utambuwe kuwa huyo ni mchawi bila shaka yeyote-
 Mchawi huuliza jina la mgonjwa na jina la mama yake
 Huchukua baadhi ya vitu vya mgonjwa kama vile nguo za nje au za ndani au kitambaa cha kufutia jasho n.k.
 Hutaka mnyama mwenye sifa maalum au rangi maalum ili achinjwe na anapigiwa BismiLLaahi anapochinjwa
 Huandika hirizi kwa aya za Quran na wino mwekundu.
 Husema maneno yasiyojulikana kwa lugha ya Kiarabu.
 Humtaka mgonjwa aepukane na watu muda maalum na akae katika chumba kisichofikiwa na juwa
 Mara nyengine humtaka mgonjwa asiguse maji muda wa siku arubaini hivi (anasema Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali kwamba akikutaka ufanye hivyo ujue kwamba Jinni anayemtumikia mchawi huyo ni muislam)
 Humpa mgonjwa vitu ili avifukie ardhini
 Humpa mgonjwa karatasi aziunguze kisha ajifukize na moshi wake
 Mara nyengine humwambia mgonjwa jina lake na mji anaoishi
 Huandika maneno katika karatasi na kumwambia mgonjwa azichemshe na kunywa maji yake
UKIONA DALILI HIZI KWA MGANGA UMJUE HAPOHAPO KUWA NI MCHAWI NA UEPUKANE NAYE
Mungu awarehemu na kuwasamehe ndugu zetu wote wanao fanya Uchawi. Maana Biblia inasema kuwa WACHAWI WOTE WATAINGIA JEHANNAM.
1 Samweli 15 : 23 .......... dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
Ndugu msomaji, mpokee Yesu aliye hai na upate uzima wa milele. Dini haita kusaidia kitu, maana sasa unaelewa kuwa, ni dini ambayo inakufanya uwe mchawi na kuachana na upendo wa Mungu.
Katika huduma yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW