Sunday, September 10, 2017

KWANINI WACHAWI WANAVAA MSAHAFU MGUUNI NA KUINGIA NAO CHOONI?

Image may contain: one or more people and text
NINI MAANA YA UCHAWI?
Al Azhari ambaye ni mtungaji wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo “LisanulArab” amesema:
“Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na Shaytwaan na kwa msaada wake (Shaytwaan)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”
Ama Swahaba Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."
Hayo ni katika kamusi za lugha.
Amma katika kamusi ya dini, maana ya neno Uchawi (As Sihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhruddin Al Razi kuwa;
"Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa (khidaa)."
Amma Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho 'Al Saarim Al Batar fiy muhaarabat Al Saharatul ashraar', na kitabu kiitwacho "Al wiqaya mina l jinni wa shaytan", ambaye pia ni mtaalamu maarufu katika elimu ya majini na Mashaytwaan na uchawi na ambaye pia ni katika maulamaa maarufu wanaotoa majini kwa njia ya kusoma Qur-aan, yeye anasema:
"Uchawi ni makubaliano baina ya mchawi na Jinni akishurutishwa mchawi kufanya mambo ya haramu au ya shirki, na baada ya kufanya hayo, Jinni anashurutishwa kumsaidia na kumtii mchawi huyo kwa kila anachotaka."
Baadhi ya yale ambayo mchawi anatakiwa na Shaytwaan ayatende ili ajikurubishe naye ni:
 Mchawi anatakiwa auvae msahafu miguuni na aingie nao chooni
 Aandike baadhi ya aya za Qur-aan kwa damu ya hedhi.
 Miongoni mwao wanashurutishwa kuandika aya za Qur-aan penye nyayo za miguu.
 Au aiandike suratul Fatiha kinyume nyume.
 Asali bila ya Udhuu.
 Wengine hutakiwa kuchinja mnyama na kulitaja jina la Allaah kisha amtupe mnyama huyo mahali maalum anapoamrishwa na Shaytwaan.
 Wamo miongoni mwao wanaozungumza na nyota au kuzisujudia.
 Au hutakiwa kuandika herizi kwa maneno yenye kufru ndani yake
USILIKOSE SEHEMU YA PILI == VIPI TUNAWEZA KUMJUA MCHAW

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW