Sunday, September 10, 2017

OMBA KWA JINA LA YESU SEHEMU YA TATU

Image may contain: text
Mafanikio haya tuliyapata kwa sababu tulipatana na kuomba kwa JINA LA YESU KRISTO !
Naamini wakristo wengi waliowahi kufanya maombi ya mapatano namna hii kwa Jina la Yesu Kristo, wanakubaliana name nikisema maombi ya jinsi hii yana mafanikio makubwa.
Mke wangu, Diana, alikuwa ananishuhudia siku moja juu ya matendo makuu ya Jina La Yesu Kristo yaliyofanyika kwa mama mmoja aliyekuwa mjamzito. Alisema, mama huyo alikuwa amefanyiwa operesheni alipojifungua mtoto wa kwanza, lakini kwa mimba ya pili alitaka asijifungue kwa operesheni, bali ajifungue kwa njia ya kawaida.
Mke wangu alisema, katika kikundi chao cha maombi cha akina mama walipatana kama alivyosema huyo mama kuwa wamuombe Mungu kwa Jina la Yesu Kristo ili (huyo mama) ajifungue kwa njia ya kawaida. Kwa hiyo wakaomba hivyo.
Siku za kujifungua zilipowadia yule mama likwenda hospitalini na akalazwa kwa muda usiopungua wiki mbili bila kupata uchungu wowote wa kuzaa. Mara kwa mara daktari alimwambia kuwa anataka kumfanyia operesheni, lakini mara zote aliahirisha bila kutoa sababu za kuridhisha. Lakini yule mama alijua ni sababu ya maombi – maana walipoomba walikataa asifanyiwe operesheni.
Baada ya wiki mbili hizo kupita siku moja ghafla alianza kusikia uchungu wa kuzaa na kisha akajifungua mtoto kwa njia ya kawaida kama walivyopatana katika maombi yao! Jina la Bwana libarikiwe kwa uweza wake mkuu. Lakini nataka ujue ya kuwa kufanyiwa operesheni si upungufu wa imani, na wala sina maana hiyo. Ila yule mama alitaka ajifungue kwa njia ya kawaida! Na akapata alichoomba!
Siku zote ukiomba, omba kwa jina la Yesu Kristo ukiwa na uhakika ya kuwa uatpewa ulichoomba. Ukiweza kumpata mkristo mwenzako wa kupatana naye kwenye maombi hayo ni vizuri pia.
Kumbuka Yesu Kristo alisema, “Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. ” (mathayo 18:19-20)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WAISLAM WANAKATA VIUNO

 

TRENDING NOW