Sunday, September 10, 2017

OMBA KWA JINA LA YESU KRISTO SEHEMU YA PILI

Image may contain: one or more people, cloud, sky and text
Maombi ya mapatano kwa Jina la Yesu Kristo.
“Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” (Mathayo 18:19-20)
Maombi ya mapatano kwa Jina la Yesu Kristo yana uwezo wa ajabu. Yesu Kristo alisema watu waliokusanyika kwa jina lake wakipatana kuomba JAMBO LOLOTE watafanyiwa na baba yetu aliye mbinguni.
Kwa nini iwe hivyo? Yesu Kristo alisema, “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.” Kwa maneno mengine tunaweza kusema jina la yesu Kristo limebeba uwepo wa Yesu Kristo. Palipo na Jina la Yesu Kristo, Yeye mwenyewe Yesu Kristo yupo – na atahakikisha mnaloliomba linapatikana. Unapoliitia jina la Bwana mahali popote ulipo, Yesu Kristo anatokea hatakama humuono kwa macho ya kimwili.
Kuna wakati Fulani mwaka 1986, watu Fulani walifika nyumbani kuambia kuwa matokeo ya mitihani waliyofanya mwishoni mwa mwaka wa kwanza katika chuo walichokuwa wanasoma yametoka, na kwamba mwenzao mmoja ameshindwa masomo matatu kwa hataendelea na masomo tena. Kwa hiyo kwa kufika nyumbani kwangu, walikuwa wamemsindikiza mwenzao kuniaga.
Habari hizo nilipozisikia sikuzipenda kwa kuwa nilifahamu kuwa watu hao walikuwa wacha Mungu, wameokoka na wanampenda Yesu Kristo sana. Na biblia imesema wazi kabisa kuwa Bwana atawafanya watu wake, “kuwa kichwa, wala si mkia” (kumb. La torati 28:13). Bwana atawafanya kuwa juu tu, wala siyo chini.
Kwa hiyo nilijua hakika haukuwa mpango wa Munguhuyo mmojawao ashindwe mitihani. Ndipo nilipoanza kumwuliza maswali huyu kijana; “je umefeli mtihani au umefelishwa”?
Yeye akajibu kwa mshangao akasema; “matokeo ya mitihani yametoka na yanaonyesha kuwa nimeshindwa mitihani mitatu – ambayo kwa utaratibu wa chuo huwezi ukaendelea na masomo”.
Kwa jibu hili nilielewa kuwa alikuwa haaelewa kwa nini nilimuuliza swali hilo. Kwa hiyo nilimwuliza swali jingine, nikasema; “Je uliwahi, kushuhudiwa rohoni juu ya matatizo utakayokuwa nayo kimasomo?” Yule msichana akajibu, “ndiyo”, na niliomba sana hata kwa kufunga”.
“Je uliomba tu pamoja na kuomba ulofanya bidii ya kusoma? Mimi nilimuuliza. Nilimuuliza swali hili kwa kuwa kuna wanafunzi wengine wakiokoka wanadhani watafaulu mitihani kwa maombi tu bila kufanya bidii katika kusoma. Wamesahau Biblia imesema “…..ufanye bidii katika KUSOMA…” (Timotheo 4:13)
Yule msichana akasema nilipokuwa naomba niliweka bidii pia katika kusoma masomo. Je ulipomaliza kufanya mitihani ya masomo yote, ni masomo mangapi ambayo ulikuwa huna uhakika wa kufaulu?” nilimuuliza tena.
“Masomo mawili tu – ambazo kufuatana na taratibu za chuo nisingefukuzwa bali ningerudia mwaka mmoja tena” alieleza yule msichana. Baada ya mazungumzo hayo nilifahamu moyoni mwangu ya kuwa Ibilisi alikuwa alikuwa amenuia kuharibu masomo ya kijana huyo. Ghafla wazo lilinijia moyoni mwangu, halafu nikamwuliza swali Yule msichana; “Je unataka kurudi nyumbani au unataka kuendelea na masomo?”
Yule msichana alishangaa nilipomwuliza swali hilo, lakini akanijivbu akasema; “napenda kuendelea na masomo, lakini wamekwisha sema nimeshindwa na matokeo yamekwisha kupelekwa makao makuu ya wizara.
Ndipo nikamkumbusha nikasema; “Mungu tunayemtumikia na kumwabudu katika Kristo Yesu, ni Mungu yule yule wa Joshua aliyesimamisha jua na mwezi visisogee mpaka wana wa Israeli walipomaliza vita kwa ushindi”.
Nikaendelea kusema kuwa; “zaidi ya hayo tunalo jina la Yesu Kristo ambalo linapita majina yote na lina mamlaka mbinguni, duniani, na chini ya nchi. Yesu Kristo alisema tukipatana lolote duniani na kuomba kwa Jina lake tutafanyiwa na Baba Mungu. Kwa hiyo tunakwenda kupatana na kuomba kwa Mungu kuwa matokeo ya mitihani yabadilishwe na urudi chuoni uendelee na masomo. Je! Wote tunakubaliana na patano hili?”
“ndiyo!” walijibu wale vijana kwa pamoja.
Halafu nikasema hivi ndivyo mtakavyofanya; “mtarudi chuoni na kuanza kumtafakari Mungu, uku wake na matendo yake yaliyoandikwa katika Biblia. Pia, mtafakarimambo ambayo amekwisha watendea ninyi binafsi. Baada ya muda mtaona ndani ya mioyo yenu uzito wa mawazo ya kushindwa mtihani yanatoweka; na badala yake mioyoni mwenu mtajaa imani ya kujua hakuna lisilowezekana kwa Mungu”
“kwa maneno mengine nataka mumtafakari Mungu na ukuu wake, kiasi ambacho mfikie ndani yenu anakuwa mkubwa kuliko tatizo mlilonalo”.
“Mkiifikia hali hiyo, ingieni katika maombi kama tulivyokubaliana, bila kusahau kutubu kwa ajili ya kushindwa mitihani. Na mimi nitashirikiana nanyi katika maombi nikiwa hapa nyumbani. Halafu kesho asubuhi uende (nikimtazama yule msichana aliyeshindwa mtihani) kwa mwalimu wako umwombe uone alama za matokeo ya mitihani ya masomo wanayosema umeshindwa – mwambie ya kuwa wewe unaamini kuwa umefaulu.
Kwa jinsi ya kibinadamu lilionekana kama ni jambo lisilowezekana – lakini wale vijana walilikubali na wakaondoka. Kesho yake jioni walirudi nyumbani kwangu kwa furaha, na yule kijana akanieleza yafuatayo:- “tulifanya kama ulivyotuambia, tukaomba na asubuhi leo nilikwenda kumwona mwalimu. Akanionyesha alama za mitihani yangu, na wakagundua kuwa kulikuwa na makosa kwa upande wao katika kuandika alama katika somo moja – badala ya kuandika maksi 19 waliandika 9. Wakaniambia nandike barua kwa mkuu wa chuo, na nikafanya hivyo, na mkuu wa chuo akasema niendelee na masomo.
Yule kijana aliendelea na masomo vizuri, sasa amemaliza na anafanya kazi! Jina la Bwana libarikiwe!
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW