Sunday, September 10, 2017

KWANINI YESU ALIINGIA KWENYE SINAGOGI SIKU YA JUMAMOSI “SABATO”?



Kabla sijaanza kuelezea kwanini Yesu aliingia Sinagogi, ni vyema tukafahamu angalau kiufupi maana ya Sinagogi.

Sinagogi ni nyumba ya dini na ya jamii ya Wayahudi inayotumika hasa kusali. Jina hili Sinagogi linatokana na neno la Kigiriki συναγωγή sinagoge, likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya neno la Kiebrania בית כנסת beit knesset, yaani "nyumba ya mkutano".

Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia sinagogi.
Sasa basi, baada ya kulewa maana ya Sinagogi, huto shangaa kuwa Wayahudi ndio watumiaji wa hayo Masinagogi na waliingia siku ya Saba “Sabato” kusali au kusoma “Shule” kama ambavyo neno hili hutamkwa katika Kiyiddish.

Hivyo, basi, haikuwa jambo la ajabu au kustaabisha tunapo soma kuwa Bwana Yesu aliingia ndani ya Masinagogi ili awafundishe Wayahudi kuhusu Ufalme wa Mbinguni. "Luka 4:16. alipokwenda Hapo Alipozaliwa Nazaret alipozaliwa na Siku ya Sabato(jumamosi) alikwenda katk#Sinagogi kama Ilivyokuwa Desturi Yake. Akasimama ili asome 17. akapewa kitabu cha nabii isaya akafunua mahali palipo andikwa "#Roho_wa_Bwana yuu Juu Yangu. Amenipaka mafuta Kuhubiriia maskini Habari njema "

Basi Wasabato wanapo soma hiyo aya teyari wanasema kuwa Yesu aliitunza Sabato kwasababu aliingia Sinagogi siku ya Saba ya Juma = Jumamosi. Haya madai hayana nguvu yeyote ile bali ni madai dhaifu. Kuingia Sinagogi siku ya Jumamosi hakukufanyi na au hakumfanyi mtu kuwa Msabato.

HILI DAI LA KUINGIA SINAGOGI naweza kulifananisha na dai la Waislam kuwa, eti, Yesu aliingia Sinagogi na hivyo Yesu ni Muislam. Waislam wao wana hoja ya kuwa Sinagogi ni Msikiti, basi ukiingia kwenye Sinagogi basi wewe ni Muislam HUKU WASABATO wana hoja ya kuwa Yesu kaingia SINAGOGI SIKU YA JUMAMOSI, basi Yesu ni Msabato. HOJA ZOTE MBILI ZA WAISLAM NA WASABATO NI DHAIFU.
Wakristo wa mwanzo hawakutumia Sinagogi katika ibada zao ndio maana Bwana wetu Yesu Kristo alisema hivi: Kwa mfano, baada ya kumtakasa mtu yule aliyejaa ukoma, Yesu alimwambia, “Asimwambie mtu, ila, Nenda ukajionyeshe kwa kuhani; ukatoe kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.” (Luka 5:14). Haya maneno yanaashiria kuwa Yesu alipo fanya huu muujiza hakuwa kwenye Sinagogi na ndio maana alimwambia Nenda ukajionyeshe kwa kuhani; ukatoe kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.” (Luka 5:14).

Hiki ni kipindi ambacho ni cha kiimani zaidi. Kimsingi hiki ni kipindi ambacho kinaendelea hadi sasa. Huu ni wakati wa kupumzika kazi za mwili za uovu, yaani kuacha dhambi na kuishi kwa kumtegemea Kristo. Ni maisha ya imani.

Imeandikwa: Njoni kwangu ninyi nyote wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. (Matayo 11.28), yaani, nitawapa ‘sabato’. Pia ndiyo maana ya andiko lisemalo: Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato. (Matayo 12:8). Sabato iko kwake, si kwenye siku.

Ni maisha ya kujiachia mikononi mwa Mungu ambaye yeye ndiye anayeshughulikia kila kitu katika maisha yetu. Kazi yetu ni kuamini tu kuwa atafanya; naye hakika anafanya. Hilo ndilo pumziko! Hiyo ndiyo raha! Hiyo ndiyo starehe! Hiyo ndiyo Sabato!

Shalom
Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na mwokozi wetu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW