Sunday, July 1, 2018
JE QURANI INAAMURU WATU KUVUA VIATU WAKATI WA IBADA?
Mwadishi: Ustadh Chaka Ibn Moosa:
Mhariri: Joseph Kimonyi
Barua pepe:abdulhaq2099@yahoo.com
Utangulizi
Mara nyingi sisi wakristo tumeshutumiwa sana na waislamu kwa kutotoa viatu wakati wa ibada. Kuna vikundi vingi sana vya waislamu hasa waendeshaji mihadhara, vikundi hivi vinazunguka sehemu mbalimbali wakifundisha watu kuwa nilazima watu kutoa viatu wakati wa ibada, Kwani hata Manabii wa zamani walifanya hivyo. Na ukiwauliza ni wapi qurani inaamuru kutoa viatu wanakuwa wakali. Swali la kujiuluza, je ni kweli au ni uongo. Fuatilia somo hili ili upate kufahamu.
Al'Hajj 22:67 (kuhiji)
“Kila umma tumeujalia kawaida ya ibada wanayoishika. Basi wasishindane nawe katika jambo hili. Na walinganie watu kwendea (Dini ya) Mola wako. Bila shaka wewe uko juu ya uongozi uliosawa kabisa.”
Kama waislamu wangalijua maana ya aya hii, wasingalipiga makelele. Kwani Mungu wao Allah anasema kuwa kila umma ameujalia kawaida ya lbada. Kwani kila umma una ibada tofauti umma mwingine.
Sehemu kuu ya somo hili
1. hoja za waislamu kuhusu kutoa viatu.
2. Kwa nini musa na Yoshwa akatoa viatu.
3. Je wakristo tuamurishwa kutoa viatu?
4. Je kuvua viatu ni ibada?
1. Hoja za waislamu kuhusu kutoa viatu.
Waislamu hupenda kutumia hoja zifuatazo kwa kudai kuwa zinamurisha watu kuvua viatu wakati wa ibada.
Kutoka 3:4-6
“Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema Musa! Musa! Akasema mimi hapa. Naye akasema, usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali usimamapo ni nchi takatifu. Tena akasema mimi ni Mungu wa baba yako Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake maana aliogopa kumwangalia Mungu.”
Andiko lingine wanalolipotosha ni hili.
Yoshwa 5:13-14
“Ikawa hapo Yoshwa alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho na kuangalia, na tazama mtu mume akasimama akamkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshwa akamwendea, na kumwambia, je! wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu? Akasema, la lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshwa akapomoka kiusouso hata nchi akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshwa, vua viatu vyako miguuni mwako, kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshwa akafanya vivyo.”
Hapa tunaona Musa na Yoshwa waliambiwa watoe viatu vyao, swali kwako wewe mwislamu unaotoa viatu wakati wa ibada. Je ni aya gani katika Qurani au Biblia inayokupa wewe ruhusa ya kutoa viatu, na kama hakuna amri hiyo mnatowa wapi.?
Wewe kama mwislamu tafakari aya zifwatazo kwa makini ili upate kuelewa.
Zaburi 139:7-12
“Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, wewe uko; ningefanya kuzimu kitanda changu, wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika. Kama nikisema, hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo imekuwa usiku; giza nalo halikuchi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawaswa.” (Pia tazama lsaya 6:3; Yeremia 23:23-24; Mithali 15:11)
Kwa mjibu wa Biblia tunaona kuwa Mungu yuko kila mahali, kwani hatuwezi kujificha uso wa Mungu.Hebu tuangalie jinsi Qurani inavyofundisha.
Al-an'am 6:3
“Na yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mbingu na katika ardhi, na anaijua ndani yenu na nje yenu; anayajua (yote) mnayoyachuma.”
Al Baqarah 2:115
“Na mashariki na magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Basi popote mgeuliapo (alikokuamrisheni Mwenyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu. Bila shaka mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa (mkubwa kabisa) na mwenye kujua kukubwa (kabisa vile vile) (24:35)”
Kwa kuwa Mungu yuko kila mahali, naomba majibu kwa maswali fwatayo.
· Je Musa na Yoshwa waliweka wapi viatu vyao?
· Na kama Musa na Yoshwa walivishika mkononi, hakuwa najisi?
· Je pahali pale palikuwa mahali pa ibada kama msikitini?
Kando na hawa kunaye mwingine aliyeamurishwa kuvua viatu?
Kwa hivyo mwislamu kabla ya kuanza kuzungumza, ni lazima ujihoji kwa maswali hayo hapo juu, na utaona ya kuwa Mungu hakuwa na maana kama waislamu wanayoichukulia, kwani Mungu mwenyewe asema hivi.
Isaya 55:8
“Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.”
2.kwa nini Musa naYoshwa wakatoa viatu.
Biblia inatufundisha ya kuwa wamesimama katika ichi takatifu. Mungu alikuwa na maana ya kujitakasa nafsi zao. Kwa mfano,
Walawi 11:44
“Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya nchi. Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka katika nchi ya misri, ili kwamba niwe Mungu kwenu; mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Mungu wetu mara nyingi hunena maneno ambayo katika hali ya mafumbo, na mtu wa mwili hawezi kufahamu. Kama vile, Mungu ametuambia kuwa tuzitahiri nyama ya govi ya roho zetu wala tusiwe wenye shingo ngumu. Kumbukumbu la Torati 10:16; Walawi 26:4; Yeremia 4:4; Wakolosai 2:11.mfano mingine wa kuangalia ni Ufunuo 2:7. Na mwenye sikio na asikie….
3. Je wakristo wameamriswa kutoa viatu?
Swala la msingi la kuchunguza ni jinsi Biblia inavyofundisha kuhusu viatu.
Kutoka 12:11
“Tena mtamla hivi, mtakuwa mefunga viuno vyenu, mmevaa viatu miguuni na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka ni pasaka ya Bwana.”
Kulingana na mafundisho ya Biblia hii ni ibada maluumu, na Mungu amesema kuwa watutakuwa wamevaa viatu. Fuatilia somo hili ili upate kujua ukweli wa mambo.
Kumbukumbu la torati 29:5
“Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.”
Mungu kwa miaka arobaini alikuwa akiwaongoza katika jangwa huku wamevaa viatu mguuni mwao. Kwa hivyo tunaona jinsi Mungu alivyo mwingi wa rehema, kwani katika mila na desturi za kiyahudi ni lazima kila mtu avae viatu. Na ndiposa nabii Yeremia ansema hivi.
Yeremia 2:25
“Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu…
Hata Yohana kwa ushuhuda wake anasema maneno haya.
Mathayo 3:11
“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuniliko mimi, wala sisitahili hata kuvichukwa viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na moto.”
Kwa wakristo Bwana Yesu ndiye mfano mwema, kwani yeye ndiye njia na kweli na uzima mtu hawezi kumfikia Mungu bila Bwana wetu Yesu kristo. Yohana 14:6.
Je kunayo aya yoyote inayowaruhusu waislamu watoe viatu wakati wa ibada?.
Al-Ahzab 33:21
“Bila shaka mnao mfano mwema (ruwaza nzuri) kwa mtume wa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kutaja Mwenyezi Mungu sana.”
Kwa waislamu mfano wao mzuri ni mtume Muhammad, kwani alichokitenda inawapasa wao kukitenda. Hebu tuangalie jinsi mtume alivyokuwa akiswali, tukichunguza na vitabu vingine. Kwa sababu Qurani inaruhusu kusoma hata hadithi za mtume.
Ash-shura 42:10
“Mkihitilafiana katika jambo lolote (rejeleeni kitabu cha Mwenyezi Mungu na hadithi za mtume kwani) hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu ninaye mtegemea, na kwake ninarejea.”
Hivyo kila mwislamu hata afanyenini ni lazima matamanio yake kama alivyotenda mtume. Na mojawapo ya yale alioyatenda ni kuswali huku amevaa viatu.
MISHKAT AL MASABIH VOL 1 SURA (CHAPTER) 10 SEHEMU 3.
Mtume alikuwa akisali huku amevaa viatu, Al Mughira alijaribu kumkumbusha Muhammad hasa pale alipomwona anatawadha juu ya viatu na kuingia navyo msikitini, hivyo Mughira akasema “Ewe Mtume wa Allah umesahau’’ Mtume akajibu kumwambia Al Mughira akisema “wewe ndiwe uliye sahau kwa maana hivi ndivyo alivyo niamuru Mungu.
Kama mtume aliambiwa aswali na viatu, mbona wewe mwislamu unatoa viatu?. Je wewe unamfuata nabii yupi?. Mafundisho ya kutoa viatu umeyapata wapi?
SAHIH MUSLIM VOL 1 HADITHI 1127. UK 277.
Abdullah bin Shakhkhir kuwa alikuwa akiswali na mtume wa Allah, (katika msikitini) kisha akamwona akitema mate na kuyafuta kwa kiatu.
Kunaruhusiwa kusali huku umevaa viatu.
SAHIH MUSLIM VOL 1 HADITHI 1129
Sa’d bin Yazid (Abu Mslama) akimliza mtume Anas bin Malik. Je mtume wa Allah alikuwa akisali na viatu vyake, Anas akajibu Ndio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?
Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment