Tuesday, July 3, 2018

Je, Wanawake Wanapaswa Kuwa Wahudumu Kanisani?

Image may contain: 5 people, people smiling, text


Swala kubwa katika mabishano ya kitheolojia ni je Mwanamke anaweza kuwa Mchungaji? Au Mwanamke anaweza kuwa Kuhani kwa wayahudi, au mwanamke aweza kuwa Rabbi kwa wayahudi na je mwanamke aweza kuwa sheihk kwa waislam? Maswali hayo yote yakijibiwa kwa ufasaha yanaweza kuleta jibu muafaka kama wanawake wanaweza kuzishika nafasi hizo nyeti katika imani,licha ya kuwa Mungu anaweza kuwakarimia karama zilezile ambazo wanaume wanaweza kuwa nazo bila upendeleo.

Biblia inasema nini kuhusu Mwanamke kuhudumu katika Kusanyiko?

Tuanze kwa kuwaangaliwa Wahudumu wa Karne ya Kwanza katika Kusanyiko. Biblia inasema nini?

Neno “mhudumu” maana yake nini? Watu wengi hufikiria kuhusu kiongozi wa kidini, awe mwanamume au mwanamke, anayeongoza kutaniko katika ibada. Lakini Biblia hutumia neno hilo katika maana pana. Mfikirie mwanamke Mkristo anayeitwa Fibi, ambaye mtume Paulo alimtaja kuwa “dada yetu, ambaye ni mhudumu wa kutaniko lililo katika Kenkrea.”—Waroma 16:1.

Kuna upinzani mwingi juu ya wanawake kuhudumu katika uchungaji. La kwanza, Paulo awazuia wanawake wasifundishe kwa kuwa katika karne ya kwanza wanawake hawakusoma. Ijapokuwa katika Timotheo wa kwanza 2:11-14 hawakutaja swala la elimu. Kama kusoma kungekuwa kigezo cha mtu kuhudumu basi wanafunzi wengi wa Yesu hawangehudumu. La pili ni kwamba Paulo aliwakataza wanawake wa kiefeso wasifundishe (Timotheo wa kwanza ni waraka kwa ajili ya Timotheo aliyekuwa mchungaji wa kanisa la Efeso). Mji wa Efeso ulijulikana sana kwa hekalu lake la Artemi, Mungu bandia wa kiyunani na kirumi. Wanawake walikuwa ndio wenye mamlaka katika ibaada ya Artemi, ambayo ndiyo sababu ya kukatazwa huku katika Timotheo wa kwanza 2:11-12.

Baada ya kupa mukhtasari huo, turudi na kumwangalia tena Fibi.

Je, unaweza kumwazia Fibi akisimama mbele ya kutaniko huko Kenkrea, akiongoza ibada ya kidini? Fibi alihudumu kwa njia gani? Katika barua yake kwa Wafilipi, Paulo anaandika kwamba wanawake fulani “wamefanya kazi ya kueneza injili . . . pamoja nami.”—Italiki ni zetu; Wafilipi 4:2, 3.

Njia ya msingi ambayo Wakristo katika karne ya kwanza walieneza injili ilikuwa “hadharani na nyumba kwa nyumba.” (Matendo 20:20) Wale walioshiriki katika kazi hiyo walikuwa wahudumu. Walitia ndani wanawake kama vile Prisila. Yeye pamoja na mume wake, ‘walimfafanulia kwa usahihi zaidi njia ya Mungu’ mwanamume fulani aliyemwogopa Mungu ambaye hakuwa amebatizwa kuwa Mkristo. (Matendo 18:25, 26) Kama tu Fibi—na wanawake wengine—Prisila pia alikuwa mhudumu mwenye matokeo.

Paulo azungumzia juu ya wake na waume zao wala si wanawake kwa wanaume kwa jumla. Neno la kiyunani katika Timotheo wa kwanza 2:11-14 yaweza kumaanisha waume kwa wake zao. Katika aya za 8-10 pia neno hilo limetumika tena. 

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume 18, Prisila na Akwila wanatambulishwa kama watumishi wa Kristo waaminifu. Jina la Prisila linatajwa kwanza, kuashiria alikuwa maarufu zaidi katika huduma kuliko mumewe.

Je, hawa Manabii/Mitume wa kike ni wa Kibiblia?

Biblia inatujibu kuwa Manabii wa Kike ni wa Kibiblia na zipo aya zinawaruhusu wanawake kuwa Manabii. Soma:

Yoeli 2: 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

Nukuu zaidi soma 1 Wakoritho 11:5, Matendo 2:17-18, Matendo 21:9, Phl 4:3,

Baada ya kusoma hiyo aya, swali linafuata, nionyeshe Nabii wa Kike kwenye Biblia? Hili ni swali nililo ulizwa na Muislam. Bila ya kupoteza muda naweka uthibitisho wa aya.

Kutoka 15: 20 Na Miriamu, nabii wa kike, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.

Miriam, Mtume wa Kike AU KWA KIINGEREZA TUNAMWITA "THE PROPHETESS" alikuwa dada ya Haruni "Aaron" Soma Kutoka 15:20, ni mwanamke wa kwanza kutajwa kwenye Biblia mwenye wadhifa huo wa Kitume. Hannah katika 1 Samuel 1:2 naye alifanya kazi kama Mtume na vile vile Huldah, ambaye alimtabiria Mfalme Josiah mara kadhaa. Debora katika Judges 4:5 alitajwa kama Mtume, 2 Wafalme 22:14

Daraka Lenye Kuheshimika

Je, kazi ya kuhubiri hadharani ilikuwa kazi ya hali ya chini ambayo ilipaswa kuachiwa wanawake huku wanaume wakifanya kazi ile muhimu ya kulisimamia kutaniko? La hasha, kwa sababu mbili zifuatazo. Kwanza, Biblia inaonyesha wazi kwamba Wakristo wote—kutia ndani wanaume wenye madaraka mazito kutanikoni—walipaswa kushiriki katika huduma ya hadharani. (Luka 9:1, 2) Pili, huduma ya hadharani ilikuwa, na bado ndiyo njia ya msingi ambayo Wakristo wote, iwe ni wanaume au wanawake, hutimiza amri ya Yesu ya ‘kufanya wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote na kuwafundisha.’—Mathayo 28:19, 20.

Kuna daraka lingine muhimu ambalo wanawake fulani wanatimiza kutanikoni. Paulo aliandika hivi: “Wanawake wenye umri mkubwa wawe . . . walimu wa yaliyo mema; ili kuziamsha akili za wanawake vijana wawapende waume zao, wawapende watoto wao.” (Tito 2:3, 4) Hivyo, wanawake wakomavu walio na uzoefu katika maisha ya Kikristo wana pendeleo la kuwasaidia wanawake wachanga, wasio na uzoefu wakomae. Hilo pia ni daraka zito, lenye kuheshimika.

Kufundisha Kutanikoni

Hata hivyo, Biblia haisemi mahali popote kwamba wanawake wanapaswa kufundisha mbele ya kutaniko. Badala yake, mtume Paulo aliwaagiza “wakae kimya katika mikutano.” Kwa nini? Aliandika kwamba sababu moja ni ili mambo yafanyike “kwa heshima na kwa utaratibu.” (1 Wakorintho 14:34, 40, BHN) Ili mambo kutanikoni yaendeshwe kwa utaratibu, Mungu amegawia kikundi kimoja daraka la kufundisha. Hata hivyo, mtu hapewi pendeleo la kusimamia kutaniko kwa sababu tu yeye ni mwanamume; daraka hilo linapewa wanaume ambao kwa kweli wanastahili.*—1 Timotheo 3:1-7; Tito 1:5-9.

Je, daraka ambalo Mungu amewapa wanawake linawavunjia heshima? La. Kumbuka kwamba Mungu amewaweka rasmi wafanye kazi muhimu, ile ya kutoa ushahidi hadharani kumhusu yeye. (Zaburi 68:11) Wanaume na Wanawake wanaohudumu hadharani wamewasaidia mamilioni ya watu watubu na kupata wokovu. (Matendo 2:21; 2 Petro 3:9) Hilo ni jambo muhimu sana!

Utaratibu uliowekwa kwa ajili ya wanaume na wanawake unachangia amani na heshima kati yao. Kwa mfano: Macho na masikio hufanya kazi pamoja ili kumsaidia mtu avuke barabara yenye magari mengi. Vivyo hivyo, wanaume na wanawake wanapotimiza mapenzi ya Mungu kulingana na madaraka ambayo wamegawiwa, Mungu hulibariki kutaniko kwa amani.—1 Wakorintho 14:33; Wafilipi 4:9.*

Ona pia kwamba mamlaka ya mwanamume kutanikoni ina mipaka. Anajitiisha kwa Kristo na lazima atende kupatana na kanuni za Biblia. (1 Wakorintho 11:3) Wale walio na madaraka kutanikoni wanapaswa pia ‘kujitiisha kwa mmoja na mwenzake,’ wakijinyenyekeza na kushirikiana.—Waefeso 5:21.

Wanapoheshimu daraka ambalo Mungu amewapa wanaume kutanikoni, wanawake Wakristo huwawekea malaika mbinguni mfano mzuri.—1 Wakorintho 11:10.

JE, UMEJIULIZA HIVI?

● Wanawake walifundisha kwa njia gani katika kutaniko la Kikristo la karne ya kwanza?—Matendo 18:26.

● Ni nani ambao wamewekwa rasmi kusimamia kutaniko?—1 Timotheo 3:1, 2.

● Mungu ana maoni gani kuhusu huduma ambayo wanawake Wakristo wanatimiza leo?—Zaburi 68:11.

Je, Biblia inaruhusu kuwa na Manabii wa Kike?

Nabii maana yake nini?

Kwanza tuanze kwa kutafuta maana ya neno Nabii.
Neno nabii (kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נְבִיאִים nevi'ìm, kwa Kiarabu نبي) linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa kusudi la kuelekeza wenzake wafuate imani na maadili sahihi.

Katika lugha nyingi, mtu huyo anaitwa kwa jina linalotokana na neno la Kigiriki προφήτης [prophētēs], maana yake "anayesema mbele", yaani hadharani (mbele ya wasikilizaji), au kabla ya (jambo kutokea).

Katika matumizi ya kawaida, neno hilo linatumika hasa kwa mtu ambaye anatabiri jambo, bila ya kujali asili ya maarifa yake.

Yoeli 2: 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

Nukuu zaidi soma 1 Wakoritho 11:5, Matendo 2:17-18, Matendo 21:9, Phl 4:3,

Baada ya kusoma hiyo aya, swali linafuata, nionyeshe Nabii wa Kike kwenye Biblia? Hili ni swali nililo ulizwa na Muislam. Bila ya kupoteza muda naweka uthibitisho wa aya.

NABII MIRIAM, DADA YA HARUNI NA MUSA:
Miriam = Soma Kutoka 15 aya 20. Naye Miriamu nabii, dada ya Haruni, akachukua tari mkononi mwake; na wanawake wote wakaanza kutoka pamoja naye wakiwa na matari na kucheza dansi

NABII DEBORA, MKE WA LAPIDOTHI:
Debora = Soma Waamuzi 4:4-5 Basi Debora, nabii wa kike, mke wa Lapidothi, ndiye aliyekuwa akihukumu Israeli wakati huo.

NABII HULDA, MKE WAS SHALUMU:
Hulda = Soma 2 Wafalme 22 na 2 Mambo ya Nyakati 34:22 Kwa hiyo Hilkia pamoja na wale wengine mfalme aliowatuma 34:22 Kiebrania hakina aliowatuma. walimwendea nabii Hulda, mkewe Shalumu, mwana wa Tokathi, mwana wa Hasra, mtunza mavazi yaliyotumika hekaluni (alikuwa anaishi Yerusalemu katika mtaa wa pili); nao walizungumza naye juu ya mambo yaliyotokea.

NABII ANNA BINTI YA FANUELI:
Anna = Soma Luka 2: 36 Basi kulikuwako Nabii Anna, binti ya Fanueli, wa kabila la Asheri (mwanamke huyu alikuwa amesonga sana katika miaka, na alikuwa ameishi pamoja na mume kwa miaka saba kutoka ubikira wake,

MKE WA NABII ISAYA:
Mke wa Isaya soma Isaya 8:3. Ndipo nikamkaribia yule nabii wa kike, naye akapata mimba na baada ya muda akazaa mwana. Mungu sasa akaniambia: “Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi,

MABINTI WATATU WA FILIPO:
Na Mabinti Watatu wa Filipo Soma Matendo 21.8 Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisarea. Huko Kaisarea tulikwenda nyumbani kwa mhubiri Filipo. Yeye alikuwa mmoja wa wale saba waliochaguliwa kule Yerusalemu. 9 Alikuwa na binti watatu ambao walikuwa na kipaji cha unabii.

Biblia inatuthibitishia kuwa Wanawake wana haki sawa na Wanaume mble ya Mungu wetu na ndio maana sio kosa kwa Mwanamke kuhudumu.


Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW