Wednesday, February 22, 2017

HABARI NJEMA

Image may contain: text
Injili, ambayo inamaanisha, “Habari Njema,” ni kwamba Mungu ametuandalia njia ya kumrudia huku akiadhibu dhambi zetu. Njia hiyo ni kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” (Yohana 14:6)
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Warumi 5:8)
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.” (Waefeso 2:8)
“Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” (Wakorintho Wa Pili 5:21)
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

 

TRENDING NOW