Wednesday, February 8, 2017

ALLAH SIO JINA LA MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)


Ndugu msomaji,
Waislam wamekuwa wakidanganya kila siku kuwa eti Mungu anaitwa Allah. Sasa leo nataka tujadili kwa amani na upendo hapa kuhusu huyu ALLAH.
Allah sio jina bali wadhifa tu. Ndio maana Allah AMEKIRI KUWA YEYE ana majina 99, ANGALIA HAPA KWA USHAHID http://www.islamicity.com/mosque/99names.htm.
Kati ya hayo majina 99 hakuna jina la Yehova, JAHAWEH, MIMI NIKO nk ingawa Waislam kila kukicha wanadai eti Mungu wa Musa ni huyo Allah au Mungu wa Daudi ni huyo Allah. Ili kuthibitisha ninacho sema, Mungu wa kwenye Biblia kasema hivi kwenye Yeremia.
Mungu mwenyewe alisema: “Watajua kwamba jina langu ni Yehova.” (Yeremia 16:21)
Sasa, wote tunafahamu kuwa Biblia ilikuja miaka 650 kabla ya Quran na kwenye hiyo Biblia Mungu alisema kuwa yeye jina lake ni "MIMI NIKO", "YEHOVA" n.k. LAKINI CHA AJABU, Allah HAKUSEMA KUWA YEYE NI "MIMI NIKO" AU "YEHOVA" kwenye hayo majina yake 99.
Je, Allah ni nani huyu, maana teyari anapinga na YEHOVA wa kwenye Yeremia 16 aya 21 na AMEKATAA kuyatumia hayo majina ya Mungu wa kwenye Biblia?
Zaidi ya hapo, wapi Mungu anasema kwenye Taurat kuwa jina lake ni Allah?
Wapi Mungu anasema kwenye Zaburi kuwa Jina lake ni Allah?
Wapi Mungu anasema kwenye Injili kuwa Jina lake ni Allah?
Haya ni maswali rahisi sana kwa Waislam na hayahitaji jazba katika kuyajibu zaidi ya wao watuletee aya kutoka Taurat au Zaburi au Injili kuwa Mungu anasema kuwa yeye jina lake ni Allah.
Wakishindwa kutuletea aya basi watuletee aya kutoka Quran ambayo Allah anasema kuwa yeye jina lake ni Yehova au Yahawe au Mimi Niko.
Leo ningependa tujadili kwa kutumia aya na kwa upendo.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

 

TRENDING NOW