Wednesday, February 8, 2017

MASWALI MAGUMU AMBAYO WAISLAM WAMEGOMA KUYAJIBU.

Image may contain: 1 person, text
1. Adamu na Hawa walifukuzwa kwenye Bustani ya Edeni kutokana na dhambi. Sisi pia tulio uzao wao ni wenye dhambi? Suluhisho la tatizo hili ni moja tu kulingana na Biblia – Yesu Kristo alikufa msalabani na kufanyika sadaka au dhabihu ili sisi tusiendelee kuchinja wanyama kila siku kwa ajili ya dhambi zetu kama torati inavyosema, badala yake tuamini TU katika sadaka ya Yesu na kupokea msamaha wa dhambi na wokovu wa Mungu bure.
Waislamu hamumwamini Yesu Kristo kama mwokozi aliyefia dhambi za wanadamu wote. Je, suluhisho la dhambi kwa mwanadamu ni nini? Kwa maana nyingine, ninyi Waislamu mtaponaje na jehanamu ya moto ilhali ni wazi kuwa ninyi, kama ilivyo kwa kila mwanadamu, mna dhambi ambazo ndizo hizohizo zilimtenga Adamu na Mungu?
2. Biblia inasema: Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:8-9). Kwa hiyo mimi Mkristo nikijikuta nimetenda dhambi nakwenda mwenyewe kwa Bwana Yesu na kumwambia, “Bwana wangu, nimesema uongo, nimeiba, nimetukana, nimetamani, … n.k. naomba unisamehe.” Sisubiri hadi mchungaji au mtu mwingine anikamate kwenye kosa kama polisi wanavyokamata wahalifu.
Ninyi Waislamu mnasema kuwa torati ndiyo njia sahihi ya maisha ya mwanadamu, kwamba mtu akifanya makosa ni lazima aadhibiwe kama vile kupigwa mawe, kuchapwa viboko, kukatwa mikono, n.k.
Swali ni kuwa, kwa nini hatusikii Waislamu wakijipeleka wenyewe kupokea adhabu hizo baada ya kufanya dhambi? Hatujawahi kusikia Mwislamu ameenda kusema, “Jamani nimezini kwa hiyo nimekuja mnipige mawe; Nimeiba, hivyo nimekuja mnikate mkono.” Kwa nini wanaoadhibiwa ni wale TU wanaokamatwa? Mnataka kutuambia kuwa wakosaji ni hao tu? Kama unaamini kuwa mzinzi ni lazima apigwe mawe, si uende ukaombe wakupige mawe baada ya kuzini. Kwa nini hamfanyi hivyo?

3. Huenda katika swali la hapo juu utajitetea kwa kusema huendi kwa sababu hujakamatwa (ingawaje Mungu tayari anakuwa ameshakukamata). Sasa, mbona hatusikii mkiwapiga viboko mia, au kuwakata mikono watoto wenu wenyewe kwenye familia zenu pale wanapoiba mboga au fedha nyumbani?
Bila shaka wizi ni wizi tu hata kama aliyeufanya ni mtoto. Ndiyo maana huwa tunawachapa viboko kwa namna ya kawaida isiyo ya kidini. Kwa nini basi sheria za kiislamu zinakuwa sahihi pale zinapohusu tu watoto wa wengine?
4. Hivi ni mwanadamu gani anayeweza kusema kuwa anaweza akae japo siku moja bila kutenda dhambi? Au hata nusu siku? Au hata saa moja tu? Hivi kuna mtu anaweza kuoga mara moja kwa mwezi halafu akabaki safi kwa mwezi huo mzima? Mimi naamini hilo haliwezekani. Ukitaka kuwa safi ni lazima uoge kila siku. Sasa, kama ambavyo jasho, vumbi na harufu mbaya ni uchafu wa mwili, je, dhambi si ndiyo uchafu wa roho? Na kama dhambi ni uchafu wa roho, “logic” ya ninyi Waislamu kuwa na mwezi mmoja wa toba ni nini? Unawezaje kutubu kwa mwezi mmoja halafu eti uwe safi mwaka mzima?
5. Bila shaka ninyi mnaamini kabisa kuwa Uislamu ni dini inayowapeleka mbinguni. Pili, mnaamini kuwa mtu akijitoa muhanga kuua makafiri (yaani akifa huku anatetea dini ya Mwenyezi Mungu), anakwenda peponi moja kwa moja.
Na bila shaka mnaamini kuwa wale makafiri wanaouawa na mwislamu kama huyo wanakwenda motoni, maana hata hivyo, wao si ni maadui wa Allah na dini yake?
Tuchukulie kuwa una watoto watatu – Amri, Hemedi na Sauda. Amri anakuja kwako na kusema, “Baba, Hemedi na Sauda wamekataa kufua nguo kama ulivyosema. Kwa hiyo nimewaua.”
Hivi, ni mwislamu gani atakayesema, “Safi sana mwanangu. Wewe ndiye unayefaa kabisa kuwa mwanangu.”
Mungu ameumba waislamu pamoja na makafiri ambao “hawataki kufua” – yaani hawataki kushika dini yake. Lakini kuna waislamu leo wanatarajia kuwa baada ya kufa, labda watamwendea Mungu huyu aliyewaumba wanadamu wote, na kusema, “Baba, nimeua makafiri mia moja kwa sababu walikuwa hawataki kufuata dini yako” – ambao maana yake ni kuwa hao mia moja wameenda jehanamu ya moto.
Kwa maneno mengine, mwislamu huyu anachomwambia Mungu hapo ni hiki: “Baba, nifungulie mlango wa pepo mimi kiumbe wako mmoja maana nimepeleka viumbe wako mia moja jehanamu.”
Swali ni kwamba: Inawezekanaje wewe ukaenda mbinguni kutokana na kupeleka wengine jehanamu? Tena wale mia moja ni watoto wa baba yuleyule unayemwomba akufungulie mlango wa mbingu!
6. Kama Mungu aliumba mbingu na nchi na kila kitu kwa neno lake tu, iweje leo neno lake hilohilo lishindwe kubadili tabia tu za watu hadi Uislamu ulazimishe kwa nguvu ya upanga kuliingiza neno hilo ndani ya wanadamu? Kwa nini nchi za Kiislamu kama vile Iran, Saudi Arabia, n.k. zina polisi na mahakama kwa ajili ya kuzuia watu kutenda dhambi!!!!! Yaani polisi wanapita huku na kule kuhakikisha watu hawazini, hawalewi, n.k. Ajabu mno! Hivi ni kweli Allah anaweza kusema kwa ujasiri kwamba watu katika nchi hizo wanampenda? Si kwamba watu kama hao wanaogopa tu polisi na mahakama?
Hata hivyo, wanachofanya polisi ni kuzuia watu kutenda dhambi kwa nje. Je, moyoni inakuwaje? Au hamjui kwamba wizi, uzinzi n.k. haukai mwilini bali moyoni? Maskini wee! Mbona Mungu wenu kawaacha mnahangaika peke yenu? Mnahangaika kutafuta waumini kwa kutumia upanga! Mkishawapata mnahangaika kuwalinda kwa polisi na mahakama ili wasitoke! Mnahangaika kuzuia dini zingine kuhubiriwa kwenye nchi za Kiislamu ili watu wasijui ukweli utakaowafanya wauache Uislamu! Kweli ndugu zangu mnatia huruma kupita kiasi.
7. Kama Uislamu ungekuwa na neno la kweli, kwa nini nchi za kiislamu zinaogopa na kupiga vita kabisa Ukristo kuhubiriwa humo? Je, hii si ishara kuwa mnafahamu kuwa watu watajua kweli ambazo zitawafanya waukimbie Uislamu?
Natumaini ndugu zangu Hamudi na Maalim Moses na Waislamu wengine mtanisaidia kupata majibu ya maswali haya. Nawaalika mpokee wokovu wa Yesu Kristo kungali mapema, maana mlango wa wokovu utafika mahali utafungwa na wale wote ambao watakuwa wako nje, kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, gharika itawakumba. Na gharika ya sasa si ya maji, bali ni ya moto. Bwana Yesu akubariki ndugu msomaji.
Shalom.

No comments:

 

TRENDING NOW