Wednesday, February 8, 2017

WAYAHUDI WANASEMA YESU KAKUFURU KWA KUJIITA MUNGU

Image may contain: 6 people, text
KUMBE YESU ALIJIITA MUNGU
Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.”
Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa Wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33).
Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu.
Katika aya zifuatazo hawasahihishi Wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30).
Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo Wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59).
Je, Wayahudi wangetaka kumpiga mawe Yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?
Shalom.
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

 

TRENDING NOW