Thursday, December 14, 2017

MALANGO KUMI YA UKUTA WA YERUSALEMU


Nehemia 1: 3, "Wakaniambia, watu wa uhamisho, waliosalia huko katika wilaya ile, wamo katika hali ya dhiki nyingi na mashutumu; tena ukuta wa Yerusalemu umebomolewa, na malango yake yameteketezwa kwa moto.

Kuonyesha namna Nehemia aliporudi Yerusalemu alivyowaandaa watu kujenga tena kuta zake na milango. Mungu hakuwasahau watu wake kamwe. Hata ingawaje wana wa Israeli mara nyingi walimsahau yeye, bali Mungu kamwe hakusahau Israeli, kwamba ni wakati walikupotwaliwa mateka katika nchi ya mbali; au wapo katika kona nne za dunia walikotawanyikia kama ilivyo leo. 

Kama ilivyo katika miili yetu tunayo milango 5 macho, masikio, ngozi, pua, tunapaswa kuyawekea ulinzi katika maisha yetu.kanisa nalo linayo milango yake ambayo pia tunapaswa kuuilinda kwa ajiri ya utumishi wetu kama ilivyo kuwa kwenye kuta zilizojengwa na nehemia wakati wake. Akaweka malango kumi katika ukuta wa Yerusalemu.ambayo huzungumzia injiri/mpango wa Mungu/kazi ya Yesu ya wokovu kwa ajiri ya waamini.

Nehemia 6:. 15-16, "Basi huo ukuta ukamalizika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Eluli, katika muda wa siku hamsini na mbili. Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo makafiri wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tama sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu. 


1) Lango la Kondoo. ( Nehemia 3:1-2)

Lango hili lilikuwa kwa ajiri ya kupitisha kondoo au wanyama kwa ajiri ya sadaka au dhabihu. lango hili hudhihirisha hali halisi ya kujitoa kuwa sadaka ya dhambi za watu wote ulimwenguni. Leo nilazima sisi tulio okoka, viongozi na makuhani kusimama kama kielelezo cha vitendo kwa kazi ya Bwana. Tuwavute watu wengi weze kuingia kwenye ufalme huu. Wakati mtu anaokoka hupitia lango hili. Yohana14:6,;10:7 na Matendo 4:12


2) Lango la Samaki. (Nehemia 3:3-5)

Lango hili lili tumika kupitishia samaki ndani ya mji kutoka Bahari kuu na kutoka kwenye mto Yordani. Hili hutufundisha jisi ya kufanyika kuwa wavuvi wa watu kwa kila mteule. Hutupa shauku ya jinsi ya kumtumikia Mungu kwa kumzalia matunda kwa uaminifu. Tusilale uvuvi upona unaendelea. Mathayo 4:19


3) Lango la kale (Nehemia 3:6-12).

Hili ndilo lango la kwanza kujengwa tangu zamani. Ni vyema kuzirejea njia na mapityo ya zamani ya imani na nguvu za Mungu.Mwanzoni tulipo anza tusiwe na enzi zetu.watu hawana tofauti hawawezi kupima. Yeremia 6:16,Yuda 1:3 na Mathayo 11:28-30.


4) Lango la Bondeni (Nehemia 3:13) 

Ni lango ambalo watu walipitia kwenda kwenye bonde la wana wa Hinomu. Bonde kwa maana ya kushuka chini.Lango hili huzungumzia unyenyekevu. Filipi 2:5-8.


5) Lango la jaa (takataka) Nehemia 3:14

Lango hili watu walilitumia kwenda kutupa takata za mji. Takataka zilipoteketezwa moto wake haukuzimika. Na waharifu walitupwa ndani ya moto usiozimika.Lango hili hutukumbusha juu ya msamaha,kujitakasa,kuvua utu wa kale na kutotenda dhambi tena. 1 Yohana 1:1:9;3:3; na Wafilipi 3:8,9. Tulikuwa kama takataka tukasafishwa kwa moto usiozima.


6) Lango la Chemichemi. (Nehemia 3:15-25)

Lango hili huzungumzia mwamini jinsi anayotakiwa kububujika na kujaa Roho Mtakatifuili kusudi tuishi tuenende na kuongozwa na Roho Mtakatifu. Wagalatia 5:18,25 na Yohana 7:37-39.


7) Lango la maji. (Nehemia 3:26-27)

Lango hili lilitumika kuleta maji ndani ya mji.lango hili huzungumzia Roho mtakatifu na Neno la Mungu lililo hai ambalo ndilo hutusafisha ,linaloponya na kutuokoa. Yohana 3:3- 6, Petro 1:23, Yohana 17:17


8) Lango la Farasi. (Nehemia 3:28)

Farasi ni wanyama waliokuwa wakiendeshwa na maaskari (Zekaria 1:8) Farasi huzungumzia vita au nguvu ya kupigana. Farasi wengi wa kivita walipitia lango hili. Lango hili hutukumbusha vita vya kiroho vinavyolikabili kanisa au wateule. 2 Korintho 10:3-5; Efeso 6:10-18; 2Timothy 2:3


9) Lango la mashariki (Nehemia 3:29-30)

Hili ndilo lango ambalo lilikuwa linafunguliwa asubuhi mapema sana.Kwa sasa lango hili bado limefungwa tangu Yesu alipo paa kwani alipitia katika lango hili. Lango hili linakumbusha mambo mawili. kwamba Yesu atarudi mala ya pili wima huo huo wa mashariki na tujitayarishe. (Zekaria 14:4 na Ezekieli 43:2). Pili ni kutukumbusha jinsi utukufu ulivyo ondoka kwa wayahudi Ezekieli 10:18-19


10) Lango la Gereza (Inspection gate) Nehemia 3:31-32

Lango hili Daudi alilitumia kukagua, kutathini na kujipanga upya maaslari wake walipo kuwa vitani. Pia aliwashukuru maaskari wake kwa utii unyofu na uaminifu wa kipekee. Pale kwenye gate lile kulikuwa na kukaguliwa unachunguzwa kwamba ukikutwa na hatia unafanywa nini unahukumiwa. Lango hili huzungumzia hukumu ya wateule katika kiti cha hukumu cha Kristo. Mbinguni hatutaingia hivihivi lazima kukaguliwa kama tumebeba mambo ya hatari. hivyo tukazane 2 Korinthion 5:10


Mambo yakafanyika kuwa kivuli na mwelekeo wa maisha yetu ya kiroho ili tuwe salama. Kazi kubwa ambayo Mungu alikuwa amemuitia akayafanya kwa uaminifu na hatari na hasara zote zilizokuwepo kabla ya ukuta kumalizika Mungu akawaponya nazo.

Kwa hiyo kwa kupitia habari ya ujenzi wa ukuta wa yerusalemu ambao ulikuwa umevujwa tumejifunza mambo mengi ya msingi yahusuyo injiri, wokovu, mpango wa Mungu na maisha kamili ya mkristo ndani ya wokovu.

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW