Sunday, December 31, 2017

ANZA MWAKA KWA KUWATUMA MALAIKA WA BWANA KUKUHUDUMIA

Image may contain: one or more people
Najua kuna wengi watasema Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu sasa umeanza kukufuru na kuachana na Yesu Mungu Mkuu. La hasha.
Mwaka huu, nataka kukufundisha jinsi ya kuwa Mkristo na jinsi ya kutumia Malaika wako na Malaika walio umbwa kwa ajili yako ili wakutumikie. Je, unafahamu kuwa Mungu aliumba Malaika kwa ajili yako, peke yako, na anaye takiwa kukutumia kila siku?
[Luka 4 aya 10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.]
[Zaburi 91: 11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. 12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.]
Ni jinsi gani Malaika wanavyotuhudumia?
Kwa mwamini, kule kufahamu kwamba Malaika wapo kwa faida yake hii ni msaada wa kutosha. Kama tunavyoweza kuwa na Imani na daktari wa upasuaji mkubwa (ingawaje hatumuoni kwa macho kwa sababu ya dawa ya usingizi na ganzi), hivyo kuelewa kazi ya malaika ni kuwa na imani katika ulinzi wa Mungu kwetu na namna Mungu anavyohusika katika maisha yetu. Kwa hakika, kwa matendo ni kitu zaidi ya hapo. Kama kweli tuwaaminifu, tunamwomba Mungu na Mungu anajibu maombi yetu kwa pamoja kama anavyopenda yeye. Hutuma Malaika wake ambaye, bila kuonekana anaamuru mazingira na hali tulizonazo, na hivyo kubadilisha maisha yetu: Hatua za mtu huimarishwa na BWANA.
Tufupishe kwa kusema, kweli Malaika wanaishi na wapo kwa ajili ya kutusaidia kama tunamcha Mungu.
Ukweli hautegemei yale tunayoyaona. Na hali ndilo kosa kubwa alilolifanya Bwana Khrushchev. Vitu kinavyoonekana ni ya muda tu bali visivyoonekana ni vya milele ( 2Wakorintho 4:18,UV).
Wakati Jeshi la mbinguni wanapotumwa kuwakusanya wateule pamoja kwa ajili ya hukumu Yesu atakaporudi, wateule wataweza kukutana na kuwaona malaika kwa mara ya kwanza Mwaliko huenda ukawa hivi, ‘Bwana amekuja anawaita!" (Yohana 11:28). Kwa sasa ni wakati wa kumwamini BWANA
MUNGU na malaika zake na hivyo kujiandaa kwa ajili ya tukio hili kubwa: "Unifumbue macho yangu, ili niyatazame maajabu yatokayo katika Sheria yako". (Zaburi 119:18)
USIKOSE SOMO LA "MALAIKA NI WALINZI"
Shalom

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW