Thursday, December 14, 2017

KUTA ZA YERUSALEM ZILIJENGWA NA WAISRAEL

Image may contain: night, sky and outdoor
ANGALIA kazi inayofanywa hapa. Waisraeli wanajenga kuta za Yerusalemu. Mfalme Nebukadreza alipoharibu Yerusalemu miaka 152 iliyopita, aliangusha kuta na kuchoma malango ya mji.
Unamjua Nehemia?
Nehemia ni Mwisraeli kutoka mji wa Shu′shani, wanaokaa Mordekai na Esta. Nehemia alifanya kazi katika jumba la mfalme. Labda alikuwa rafiki mzuri wa Mordekai na Malkia Esta. Lakini Biblia haisemi Nehemia alimtumikia Mfalme A·has·u·e′ro, mume wa Esta. Alimtumikia Mfalme Ar·ta·ksase, aliyefuata.
Kumbuka, Ar·ta·ksase ni mfalme yule mzuri aliyempa Ezra fedha apeleke Yerusalemu kwenda kutengeneza hekalu la Yehova. Lakini Ezra hakujenga kuta za mji zilizobomoka. Na tuone ilivyokuwa hata Nehemia akafanya kazi hiyo.
Imekuwa miaka 13 tangu Ar·ta·ksase alipompa Ezra fedha za kutengeneza hekalu. Nehemia sasa ni mnyweshaji wa Mfalme Ar·ta·ksase. Maana yake anamnywesha mfalme divai, na kuona kwamba hakuna mtu anayejaribu kumpa mfalme sumu. Hiyo ni kazi ya maana sana.
Basi, siku moja Hanani ndugu ya Nehemia na watu wengine kutoka nchi ya Israeli wanakuja kumtembelea Nehemia. Wanamwambia habari ya kutaabika kwa Waisraeli, na namna kuta za Yerusalemu zingali zimebomoka. Nehemia anahuzunika sana, naye amwomba Yehova juu ya hilo.
Siku moja mfalme anaona kwamba Nehemia ana huzuni, anauliza: ‘Sababu gani una huzuni?’ Nehemia anasema Yerusalemu umeharibika sana na kuta zimebomoka. ‘Wataka nini?’ mfalme auliza.
Nehemia akisimamia kazi ya ujenzi
‘Unipe ruhusa niende Yerusalemu,’ Nehemia asema, ‘nikajenge upya kuta hizo.’ Mfalme Ar·ta·ksase ni mwema sana. Akubali Nehemia aende, kisha amsaidia kupata mbao za kujengea. Mara Nehemia akiisha kufika Yerusalemu, anawaambia watu mipango yake. Wanapenda wazo hilo, na kusema: ‘Na tuanze kujenga.’

Adui za Waisraeli wanapoona ukuta unafika juu, wanasema: ‘Tutakwenda kuwaua, na kuzuia ujenzi.’ Lakini Nehemia anasikia habari hiyo, kisha awapa wafanya kazi panga na mikuki. Ndipo awaamgia hivi: ‘Msiogope adui zenu. Piganieni ndugu zenu, watoto wenu, wake zenu, na nyumba zenu.’
Watu wanakuwa hodari sana. Wanaziweka silaha zao tayari mchana na usiku, wanaendelea kujenga. Basi kwa muda wa siku 52 tu kuta zinamalizika. Sasa watu wanajisikia salama ndani ya mji. Nehemia na Ezra wawafundisha watu sheria ya Mungu, ana watu wafurahi.
Lakini mambo hayako namna yalivyokuwa kabla Waisraeli hawajapelekwa Babeli wakiwa wafungwa. Watu wanatawalwa na mfalme wa Ajemi na yawapasa wamtumikie. Lakini Yehova Mungu Mkuu ameahidi kutuma mfalme mpya, na mfalme huyo ataletea watu amani. Ni mfalme gani huyo? Ataletea dunia amani namna gani? Miaka 450 yapita kabla ya kupata habari zaidi. Halafu mtoto wa maana sana azaliwa. Lakini hiyo ni hadithi nyingine.
Nehemia sura za 1 mpaka 6.
USIKOSE SOMA LA MILANGO KUMI YA KUTA ZA YERUSALEM
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW