Saturday, December 16, 2017

USHAHIDI WA KIHISTORIA WA YESU


Masimulizi kuhusu maisha na huduma ya Yesu yameandikwa katika Biblia, nayo hujulikana kuwa Injili, na yanaitwa kwa majina ya waandikaji wake, yaani, Mathayo, Marko, Luka, na Yohana. Kwa kuongezea, vyanzo vingine vya habari visivyo vya Kikristo vinaeleza kuhusu Yesu.

TACITUS

(c. 56-120 W.K., au Wakati wa Kawaida) Tacitus anajulikana kuwa mmoja kati ya wanahistoria mashuhuri zaidi wa Roma ya kale. Maandishi Yake yanaeleza kuhusu Milki ya Roma kuanzia mwaka wa 14 W.K. hadi 68 W.K. (Yesu alikufa mwaka wa 33 W.K.) Tacitus aliandika kwamba moto mkubwa ulipoharibu Roma mwaka wa 64 W.K., ilidhaniwa kwamba Maliki Nero alihusika. Hata hivyo, Tacitus aliandika kwamba “ili kumaliza uvumi huo,” Nero aliwalaumu Wakristo kuhusika na moto huo. Kisha, Tacitus alisema: “Kristo, ambaye ni chanzo cha jina [Mkristo], alihukumiwa kifo katika utawala wa Tiberio, kupitia hukumu iliyotolewa na mtesaji Pontio Pilato.”—Annals, XV, 44.

FLAVIUS 

Flavius Josephus (Yosefasi) ni mwanahistoria maarufu wa Kiyahudi. Katika uandishi wake unamrejelea Yakobo “ndugu yake Yesu, aliyeitwa Kristo” Kuna aya ya kutatanisha aya (18:3) ambayo yasema, “Sasa kulikuwa na huu wakati Yesu, mtu wa hekima, kama itakuwa kisheria kumwita mtu. Ni yeye alifanya maajabu, alikuwa Kristo, alitokea kwao akiwa hai tena siku ya tatu, vile unabii wa kweli ulikwishasema juu yake na vitu vingine elfu kumi vilisema kuhusu juu yake. “Tafsiri moja yasoma, “kwa wakati huu kulikuwa na mtu wa hekima aitwaye Yesu. Tabia yake ilikuwa nzuri, alijulikana kwa maadili mema. Na watu wengi kutoka kwa Wayahudi na mataifa mengine wakawa wanafunzi wake na hawakuacha huanafunzi wao. Waliripoti kwamba aliwatokea siku tatu baada ya kusulubiwa kwake; kwa hivyo alikuwa Masia, ambae manabii walisema makuu yake.”

JULIUS

Julius Africans anamnukuu Thallus mwanahistoria kwa mjadala juu ya giza lilokuja baada ya kusulubiwa kwa Yesu (Extant writings, 18).

SUETONIUS

(c. 69–a. 122 W.K.) Katika kitabu chake Lives of the Caesars, mwanahistoria huyo Mroma alirekodi matukio ya utawala wa maliki wa kwanza wa Roma hadi maliki wa 11. Katika sehemu anayoeleza kuhusu maliki Claudius anataja vurugu iliyotokea miongoni mwa Wayahudi huko Roma, ambayo huenda ilisababishwa na bishano kumhusu Yesu. (Matendo 18:2) Suetonius aliandika hivi: “Kwa kuwa Wayahudi walifanya vurugu mara kwa mara kwa kuchochewa na Kristo, [Claudius] aliwafukuza Roma.” (The Deified Claudius, XXV, 4) Ingawa dai lake kwamba Yesu alianzisha vurugu ni la uwongo, Suetonius aliamini kwamba Yesu alikuwa mtu halisi.

PLINI MDOGO

(c. 61-113 W.K.) Mtungaji huyo Mroma na msimamizi wa Bithynia (sasa Uturuki) alimwandikia Maliki Mroma Trajan jinsi ya kushughulika na Wakristo katika eneo lake. Plini alisema kwamba aliwalazimisha Wakristo wakane imani yao, na aliwaua wote waliokataa kufanya hivyo. Alifafanua hivi: “Wale . . . waliorudia kiapo kwa Miungu [ya kipagani], na kuabudu sanamu yako kwa kufukiza ubani na divai . . . na ambao mwishowe walimlaani Kristo . . . , niliwaachia huru.”—Pliny—Letters, Book X, XCVI.

Mdhuluma wa Kibabeli (Sunhedrin 43a) anatibitisha kwamba kusulubiwa kwa Yesu siku ya pasaka na makisio kwamba Yesu alifanya uchawi na kuipa moyo fundisho potovu la Kiyahudi.

FLAVIO YOSEFO

(c. 37-100 C.E.) Mwanahistoria na kuhani huyo Myahudi alisema kwamba Anasi, kuhani mkuu Myahudi ambaye alikuwa na uvutano mkubwa wa kisiasa, “aliwashawishi mahakimu wa Sanhedrini [mahakama kuu ya Wayahudi] na kumleta mbele yao Yakobo, ndugu ya Yesu aliyeitwa pia Kristo.”—Jewish Antiquities, XX, 200.

LUCIANA

Luciana (Lucian) wa Samosata alikuwa mgiriki mwandishi katika karne ya pili anayekubali kwamba wakristo walimwabudu Yesu, na kuleta mafundisho mapya na alisulibiwa kwa ajili yao. Alisema kwamba mafundisho ya Yesu yalijumlisha undugu wa wakristo, umuimu wa kuokoka, na umuimu wa kukataa miungu. Wakristo waliishi kulingana na sheria ya Yesu, waliamini kuwa mili yao haiharabiki na walikuwa wakijulikana kwa kutoogopa kifo, na kutolea nafsi zao kwa hiari yao na kukataa utajili wa dunia.

MARA BAR-SEAPION

Mara Bar-seapion anatibitisha kwamba Yesu alifunzwa kuwa mtu wa hekima na maadili mema, alichukuliwa na wengi kuwa mfalme wa Israeli. Alisulubiwa na Wayahudi, na aliishi njia wanafunzi wake wanafundisha.

Pia tuko na maandishi ya Wayunani (Injili ya kweli/The Gospel of Truth, Kitabu kingine cha Yohana/Apocryphon of John, Injili ya Thomasi/ The Gospel of Thomas, Makubaliano juu ya ufufuo/The Treaties on Resurrection na mengine) yote yanamtaja Yesu.

Kwa kweli tunaweza kujenga injili kutoka kwa maandishi yasiyo ya kikristo. Yesu aliitwa Kristo (Josephus), alitenda “miujiza” aliwaongoza waisraeli kwa mafunzo mapya na aliangikwa siku ya pasaka kwa ajili yao (Ubebari wa kibabeli/ Babylonian Tulmud), katika Yuda (Tacticus), lakini alisema kuwa Mungu na atarudi (Eliezar), ambacho wanafunzi wake waliamini na kumwabudu kyeye kama Mungu (Pliny mdogo).

TALMUD

Mkusanyo huo wa maandishi ya kirabi ya Kiyahudi ya kuanzia karne ya tatu hadi sita W.K., huonyesha kwamba hata maadui wa Yesu waliamini kwamba alikuwa mtu halisi. Sehemu moja ilisema hivi: “Yesu Mnazareti alitundikwa mtini siku ya Pasaka,” hilo ni sahihi kihistoria. (Babylonian Talmud, Sanhedrin 43a, Munich Codex; soma Yohana 19:14-16) Sehemu nyingine inaeleza hivi: “Tusiwafundishe watoto katika njia itakayowaletea aibu hadharani kama Mnazareti,” jina ambalo nyakati zote lilirejelea Yesu.—Babylonian Talmud, Berakoth 17b, footnote, Munich Codex; soma Luka 18:37.

ALBERT EINSTEIN

Albert Einstein, mwanafizikia mzaliwa wa Ujerumani na Myahudi alieleza hivi: “Mimi ni Myahudi, lakini ninavutiwa sana na mfano mzuri wa Mnazareti.” Alipoulizwa ikiwa anaamini kwamba Yesu alikuwa mtu halisi, alijibu hivi: “Bila shaka! Hakuna mtu anayeweza kusoma Injili na akose kuamini kwamba Yesu alikuwa mtu halisi. Maneno yake yalifunua utu wake. Hakuna simulizi lingine lililo na mambo halisi kama hayo.”

“Hakuna mtu anayeweza kusoma Injili na akose kuamini kwamba Yesu alikuwa mtu halisi.”—Albert Einstein

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW