Sunday, December 31, 2017

MAOMBI YA KUFUNGA MWAKA NA KUANZA MWAKA MPYA 2018 KWA BARAKA TELE KUTOKA KWA MUNGU MKUU, YESU KRISTO ALIYE HAI

Image may contain: nature and outdoor
Ndugu msomaji na mpendwa katika Bwana. Bwana Yesu apewe sifa.
Mpendwa, yawezekana umekuwa ukiishi bila kutambua uwezo wa jina la Yesu katika kukuonyesha mwelekeo wa maisha yako.Je, unahitaji mwelekeo mpya katika maisha yako? Je, unahitaji kujua njia ya kutoka katika hali uliyonayo?
KAMA UMECHOKA NA MAISHA YA TABU, KAMA UMECHOKA KUISHI NA MAGONJWA, KAMA UMECHOKA KUWA MASKINI, KAMA UNAHITAJI KAZI, BIASHARA YAKO IFANIKIWE N.K. BASI HUU UJUMBE NI WAKO.
Napenda kukufahamisha kuwa, tupo katika Maombi kila siku mpaka tutakapo maliza mwaka huu wa 2017. Nafahamu wengi mmepata baraka tele katika Mwaka wa 2017 na labda wengi mmlikuwa katika mashindano na vita kubwa na nguvu za giza. Kumbuka USHINDI ni wetu katika Jina la Yesu.
Mpendwa , pengine hali ya maisha uliyonayo imekufanya ukate tamaa na kujiona kwamba hakuna njia ya kukufanya utimize furaha ya ndoto zako. Je, unahitaji njia ya kuishi kwa amani na furaha; njia ya kuwa na mahusiano mazuri katika ndoa yako; njia ya kuwa na mahusiano mazuri na ndugu zako, kazini kwako, kwenye biashara yako; unahitaji njia ya kuacha ulevi wa pombe na madawa ya kulevya, njia ya kuacha kuabudu sanamu, njia ya kuacha uongo, njia ya kuacha uzinzi, njia ya kuacha uchawi, njia ya kuacha tamaa ya mali zisizo halali; njia ya kuponywa maradhi, njia ya kupata utajiri, njia ya kupata kazi, njia ya kupata mtaji , njia ya kutoka kwenye madeni, njia ya kupandishwa cheo, njia ya kutimiza ndoto zako? Yesu ni njia ya kila mahitaji yetu hapa duniani, pia yeye ni njia ya kutufanya tujue kweli ya neno lake na tuweze kuurithi uzima wa milele.
Kama unahitaji lolote lile ambalo unataka upokee jibu kutoka kwa Mungu Mkuu, Yesu aliye hai, basi nakusihi ututumie hilo hitaji lako haraka ili tuwe pamoja katika maombi katika muda huu wa kumaliza mwaka wa 2017. Tuma ombi lako kupitia barua pepe maxshimbaministries@gmail.com
Matayo 7:7-11Neno: Biblia Takatifu (SNT):
7 “Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. 8 Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.
9 “Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?
Yesu katika Matayo hapo juu anakwambia "OMBENI NANYI MTAPEWA' Sasa Mpendwa unasubiri nini kumwomba Mungu Mkuu? Au unapenda kuwa katika matatizo na shida? Shetani teyari alisha wekwa chini ya miguu yetu.
Yesu anaweza kila kitu haijalishi umekuwa katika hiyo shida au hitaji kwa miaka mingapi. Huu ujumbe ni kwa wewe unaye soma, na Yesu anataka kukuhakikishia kuwa, teyari amesha kujibu na uanze kushukuru kwa kuwa alisha maliza yote pale Msalabani.
1. Kama unashida ya kupata Mtoto, basi tuma ombi lako mara moja.
2. Kama unashida ya Magonjwa, basi tuma ombi lako mara moja.
3. Kama unashida ya kupata kazi, basi tuma ombi lako mara moja.
4. Kama unashida ya kupata Mume au Mke, basi tuma ombi lako mara moja.
5. Kama unashida ya Fedha, basi tuma ombi lako mara moja.
6. Kama unashida yeyote ile, usiwe na wasiwasi, Yesu amesha sema katika Matayo kuwa OMBENI NANYI MTAPEWA.
Mpendwa, Shetani anaweza kukwambia kuwe, wewe matatizo yako hayatatuliki, au labda wewe huto weza kupona, HATA ikiwa una UKIMWI, SERATINI, MAGONJWA YA MOYO, KISUKARI, N.K. usiwe na wasi wasi tena, MAANA YESU ANASEMA KUWA
Mpendwa, Mungu anatupenda sana; ametupa njia bora kabisa na anataka tuishi maisha ya ushindi siku zote katika kila eneo kupitia mwana wake, Yesu Kristo.Mkaribishe leo Yesu na mfungulie yote yaliyomo moyoni mwako ili aweze kukuonyesha njia ya kila hitaji lako na ukawe na mwelekeo mpya wa maisha yako.
Tuma moambi yako kupitia barua pepe maxshimbaministries@gmail.com
Neema ya Mungu iwe nanyi
Max Shimba Ministries 2017

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW