Friday, December 22, 2017

VITA VYETU SI VYA DAMU NA NYAMA


"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho." Waefeso 6:12

Ndio maana kina Meshaki, Shadraka na Abednego walipotupwa katika moto hawakuwa peke yao naye akawa ndani ya moto na kuwaokoa mwisho wa siku Mungu akajipatia utukufu kwa mfalme Nebukadreza (Daniel 3;28). Mungu wao akatukuzwa katika jamii yote ndiye Mungu aokoae ambaye ni Yesu Kristo Mungu Mkuu Tito 2:13.

Hata Danieli alipotupwa katika tundu la Simba wakali ndani ya tundu la Simba, Danieli hakuwa peke yake Malaika alikuwa naye akamlinda na Simba hawakumdhuru. Akatoka salama na Mungu wa Danieli akatukuzwa katika jamii YOTE YA DUNIA kuwa ndiye Mungu aponyaye, aokoaye na kutenda ishara na maajabu. (Daniel 6;25)

Unapopita katika jaribu nawe ukishinda Mungu wako anapata sifa kwa jamii na kutukuzwa ndio maana wakati mwingine lazima upite katika jaribu ili Mungu wako apate kutukuzwa nawe pia unaposhinda unapandishwa cheo katika ulimwengu wa roho huwi vilevile, Yesu aliposhinda alipewa mamlaka mbinguni na Duniani..

Basi kama kama upo katika majaribu usidhani unapita peke yako, Mungu aliye kuwa na Daniel yupo pamoja nawe. Unatembea naye katika hilo jaribu mwisho wake ushindi, sifa na utukufu zitamwendea Mungu wako aliyekushindia.

MBARIKIWE.

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW