Friday, July 14, 2017

JINSI YA KUOMBA KWA IMANI, SEHEMU YA KWANZA

Image may contain: sky, text, nature and outdoor


Imani si kuamini kwamba Mungu anaweza, ama ataweza, bali imani ya kweli ni kuamini kwamba Mungu ameshatenda.
Je, umewahi kumwomba Mungu kitu kikubwa, na ukiisha sema “Amin,” ukawa na tashwishi kama kweli utapata jibu? Labda ulisema, “Hawezi kujibu ombi hili.”
Hebu sikiliza ahadi ya maandiko kuhusu maombi na imani:
Yesu akajibu, akawaambia:
“Mwamini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” – Marko 11:22-24
Kwa kuwa Mungu ni Baba yetu, anapendezwa tunapomwamini. Anapenda tuamini neno lake. Hakuna kitu kingine kinachompendeza kuliko imani ndogo kama ya mtoto mdogo. Waebrania inasema kwamba, “lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza” (Waebrania 11:6).
Hii ni haki kabisa tunapomwendea katika maombi. Bwana wetu alitilia jambo hili mkazo katika Marko 11:22-24. Alituamuru tuwe na imani kwa Mungu. Anatuhimiza tuombe tukiwa na imani ili tupate tayari majibu kwa maombi yetu. Maneno hayo yanatuonyesha Mungu alivyo. Anatamani kuwapa wanawe
wanaoamini mahitaji yao!
Imani ya kweli ni kwamba “Mungu tayari” ametimiza matakwa yangu. Hi ni imani yenye maana ambayo imeelezwa katika Waebrania 11: “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1).
Imani si kutumaini, bali ni kuwa nayo. Kiini cha neno “kuwa na hakika” ni halisi, au hali halisi ya kitu, kama vile tunaona katika Waebrania 1:3 kuhusu Kristo kuwa hakika ya Mungu mwenyewe. Nikiwa na imani kwa kitu cha kubainisha, basi kinafanyika kuwa halisi katika maisha yangu. Nikiliamini, basi ninalo!
Si ajabu hilo? Ndio, ni kweli.
Huyu ni Yesu akifundisha katika Marko 11;24: “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” Wakati ule ninapoamini kwa hakika, jibu li njiani, laja. Lugha iliyotumika katika maandiko pale mwanzoni ina uzito mwingi kwamba tafsiri ya New American Standard Bible inakosoa kwa usawa tafsiri iliyokubalika kutoka kwa “mtapokea” hadi “mmepokea.”
Kwa hivyo, mara tu unapoamini, tayari umepokea (hali ya kale)! Yesu ndiye aliyesema hayo, si mimi.
Imani ni kupokea. Mtu alieleza imani kibibilia hivi, “Imani ni kutenda kama ipo, hata kama haipo, na itakuwepo.” Imani ni kubadilisha bayana kuwa yaliyopo.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Imani Na Mapenzi Ya Mungu Yesu alituambia tuwe na “imani kwa Mungu.” Hi inahusu mpango na kusudi la Mungu kwa maisha yako.........====> SEHEMU YA PILI====>
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

 

TRENDING NOW