Friday, July 14, 2017

KWANINI TUNAOMBA KATIKA JINA LA YESU? SEHEMU YA KWANZA

Image may contain: ocean, sky, cloud, text, water, outdoor and nature


Kuomba katika jina la Yesu, kwa Muumini, ni njia ya kumfikia Mungu Baba. Imani yetu katika hilo jina takatifu hutuwezesha kuifikilia chumba cha enzi.
Nilipokuwa kijana mdogo, wazazi wangu walianza kunifundisha dini kwa kuniorodhesha katika shule ya Seminari. Miaka yangu mitatu katika masomo yalitokana na msingi huo wa elimu. Ombi la kwanza ambalo nakumbuka kuomba ni ombi la kukariri "neema” wakati wa chakula nikiwa katika shule hiyo.
Watoto wengi Seminari na Wakatoliki hukariri ombi hili fupi kwa Mungu wakatika wa kwenda kulala, wakisema, “Tubariki, Ee Bwana, kwa vipawa hivi ambavyo tuko tayari kupokea kutoka kwa utajiri wako, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Amin.”
Hilo ndilo lilikuwa ombi langu la kwanza. Ombi hili si baya. Sehemu ya mwisho katika ombi hilo ilinifurahisha sana, “kwa Yesu Kristo Bwana wetu.” Nilipoendelea kuwa mkubwa, nilianza kusikia wengine wakimaliza maombi kwa kusema “Katika jina la Yesu. Amin.” Nikaanza kuwaza na kuwazua “kwa nini” wanaomba “katika jina la Yesu.” Nikawa mtu mzima kabla moyo wangu kukubali ukweli wa maneno hayo.
Ombi Rahisi
Yesu alikuwa akiwapa wanafunzi wake funzo kamili kuhusu utiifu, Roho Mtakatifu na maombi katika Yohana 1:16. Katikati ya mafundisho hayo, mara tatu Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuomba Mungu “katika jina langu”: “Amin, amin, nawaambia, mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu” (Yohana 16:23,24). Kristo tayari ameshawishi jambo hili katika sura ya 14, na akarudia katika sura ya 15 (Yohana 14:13,14 na Yohana 15:16). Kurudia huku kulimaanisha kutilia mkazo kanuni hii rahisi: kukaribia moyo wa Mungu ni kupitia kwa jina la Mwanawe.
Kukosa Kuomba ni Kukosa kupokea:
Fundisho hili lilikuwa la kipekee, na geni kwa wanafunzi wa Kiyahudi. Katika historia yao, hawakuwahi kumwomba Yehovah Mungu katika jina la mtu! Ndio sababu Yesu alisema, “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu” (Yohana 16:23). Hili ni fundisho linalobadilisha. Ni kiini cha theologia ya Kikristo. Yesu
anasema kwamba kuna njia jipya ya kufika kitini pa enzi kwa Mungu, ambalo halijapitiwa na mtu mwingine awaye yote. Kuna nambari ya siri ya simu mpya isiyojulikana na yeyote, ya kwenda kwa kiti cha enzi cha Mungu. Hebu piga simu hiyo! “Hata sasa, hamjamwendea Baba kwa jina langu. Sasa fanya hivyo naye Baba yangu atakupa kila hitaji lako,” asema Bwana Yesu.
Hili laonekana kuwa kinyume, lakini sivyo kamwe! Hadi wakati huo, hakuna aliyewahi kumwomba Mungu “kwa jina la Yesu.” Labda hii haikufanywa na wafuasi wa kwanza wa Kristo hadi baada ya Pentekote.
Iligharimu uchochezi wa Roho Mtakatifu, aliyekuwa akiishi ndani yao, kuwafanya kuomba katika jina la Yesu.
Hivi sasa watu wengi wanaomba maombi kila siku, yakiwa maombi ya kukaririwa, na kuyamaliza kwa “jina la Yesu” bila kumaanisha. Kanisa likifahamu uwezo na nguvu iliyoko katika jina la Yesu, basi maombi yetu yataleta Pentekote mara nyingine. Kanisa la kwanza lilichochewa na imani katika hilo jina la Yesu. Jina hilo litaweza kuwasha imani na moto katika moyo wako ikiwa utatambua kwa nini Mungu anaheshimu jina la Yesu.
USIKOSE SEHEMU YA PILI ===>Mbona uombe katika jina la Yesu?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW