S: Hoja kuwa "kushindwa kuelezeka kirahisi kwa ulimwengu kunaonyesha kuwa ni lazima kuwe na muumba" inaonekana nzuri, hadi inapochukuliwa kwenye hitimisho lake la kimantiki. Vipi kuhusu ugumu wa Mungu kueleweka? Kama kitu chenye utatanishi kinahitaji muumba basi Mungu lazima ahitaji muumba mkubwa zaidi, na kwa jinsi hiyohiyo na kuendelea. Je hoja hii inaishia wapi? Hoja hii inaishia na "kurudi nyuma kusikokuwa na ukomo," na hakuna jibu kwa hili? Ama je lipo?
J: Kabla ya kuijibu hoja hii, hebu nilikuze "tatizo hili" kwanza. Licha ya ugumu wa kuelezeka, suala hil pia ni aina iliyopotoka ya hoja ya muundo na umbo la ulimwengu. Kama kila kitu kina chanzo, basi Mungu naye pia ana chanzo.
Kwa kuwa kila kitu ni lazima kiwe na mwisho, vinginevyo hakitakuwa na mwisho, kuna majibu mawili tu yanayoweza kutolewa:
hakuna mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na ukomo
hakuna mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na mwisho, chanzo ambacho hakijasababishwa na kitu kingine chochote.
hakuna mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na mwisho, chanzo ambacho hakijasababishwa na kitu kingine chochote.
Kama a), kusingekuwa na mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na ukomo, basi si kila kitu kingekuwa na chanzo kwa sababu kurudi nyuma kusikokuwa na mwisho kwenyewe hakuna chanzo. Kwa hiyo, kwa vyovyote vile kuna mtu/kitu ambacho hakina chanzo.
Kama b), kuna mwisho wa kurudi nyuma kusikokuwa na mwisho, basi ni lazima kuwe na chanzo cha kwanza, cha ugumu fulani wa kufahamika. Kwa ajili hiyo, jambo hili linamaanisha kuwa Mungu si nafsi iliyotokana na kitu kingine, si matunda ya uumbaji.
Hata hivyo nashangaa, kama Mungu angeiona hoja hii yote kuwa nyepesi namna hii, kw asababu tunafikiri kuhusu vyanzo ndani ya muda. Kama mungu anaishi nje ya muda na pia ndani yake, na kama muda ni kitu kimojawapo kilichoumbwa na Mungu, basi kusema kuwa hali ilikuwaje kabla ya kuwepo kwa Mungu ni kujipinga.

S: Kwenye Mwanzo 1, Mungu anaweza kuwa aliumba viumbe wengine na ulimwengu mwingine?
J: Aliumba viumbe wengine: malaika na mapepo. Kuhusu kuumba ulimwengu mwingine wenye viumbe ndani yake, Biblia haituambii haya yote tunayotaka kujua — na tunapaswa kuhakikisha kuwa walau tunasoma jambo hilo. Mungu angeweza kuwa ameumba ulimwengu mwingine, na huenda hizo ndizo mbungu na kzimu.
S: Kwenye Mwanzo 1, kwa nini Mungu aliwaumba Adam na Hawa, kwa kuwa Munug alijua kabla kwamba hawatamtii?
J: Pamoja na Mungu kujua kuwa watafanya dhambi, anatuambia vitu kadhaa kutuonyesha kuwa kwa nini aliumba watu.
J: Pamoja na Mungu kujua kuwa watafanya dhambi, anatuambia vitu kadhaa kutuonyesha kuwa kwa nini aliumba watu.
Kwa utukufu wake: Mungu aliumba watoto wake kwa utukfu wake. Isaya 43:7; 61:34.
Watu wa kuwapenda: Mungu anatupenda sana. Zaburi 145:9,17; 1 Yohana 3:1.
Kuwa watoto wake: 1 Yohana 3:1-2; Wagalatia 3:28, Warumi 8:15-17.
Kuishi ndani mwetu: 1 Yohana 4:12-16; Warumi 8:9-11.
Mungu hataki mtu yoyote apotee. Ezekiel 18:23, 32; 33:11; 2 Petro 3:9. Hata hivyo, Mungu hajuti kwa kuwaumba watu ambao walipopewa nafasi walichagua kwa hiari zao wenyewe kumkataa. Mungu aliishajua kabla kuwa watafanya dhambi, na bado hakupenda kuingilia uchaguzi wao au "kutokuwaumba."
Huenda moja ya sababu ya Mungu kuwaumba viumbe ambao watakuwa na sura yake inafanana na sababu ya wazazi kuwa na watoto. Ni kweli, watoto wana gharamua: nepi, chakula, na kweli wanasababisha maumivu ya kichwa tokana na kuugua, kuumia, na kutokutii lakini pamoja na hayo yote upendo unawafanya wastahili kuwepo.

S: Kwenye Mwa 1:1, Mungu aliumba kwa sababu alihitaji kuumba?
J: Biblia haiungi mkono hisia hizi. Mungu hana uhitaji wowote ule, kwa maana ya kwamba atadhulika au kukoma kuwepo kama hangeumba vitu vingine. Kwa upande mwingine, lengo la Mungu lilikuwa kuumba, na Mungu alitimiza lengo hilo kwa kiasi kikubwa kikubwa sana.
S: Kwenye Mwa 1:1, je kulikuwa na uumbaji zaidi ya Mwanzo?
J: Maandiko hayasemi chochote kuhusu jambo hili, na Mungu Mungu anao uhuru wa kufanya kama apendavyo. Kama Mungu angeumba viumbe wengine, wangekuwa kama malaika, mapepo, kama Adam na Hawa kabla ya anguko, kama sisi, kama mapepo, kama wanyama, au kitu tofauti kabisa.
S: Kwenye Mwa 1:2, kama Roho ya Mungu ilikuwa inatulia juu ya uso wa maji, jambo hili linamaanisha Roho wa Mungu si nafsi hai yenye akili bali nguvu itendayo kazi kama Mashahidi wa Yehova wanavyodai?
J: Hapana. Kwamba Roho Mtakatifu hana mwili na anaweza kutembea juu ya maji haipingani na ukweli kwamba Maandiko yanamwonyesha Roha Mtakatifu kuwa kiumbe kinachoishi na chenye nafsi.
Yafuatayo ni marudio ya maelezo ya 1 Yohana 5:6-8.
Shahidi anaweza kuwa ni nafsi hai au kitu kisichokuwa na uhai. Kosa la Mashahidi wa Yehova (Jehovah’s Witnesses) ni kwamba kwa kuwa Roho Mtakatifu ana sifa nyingi ambazo mwanadamu hana, basi (kwa kupanua hoja) Roho Mtakatifu hawezi kuwa na nafsi. Kwenye 1 Yohana 5:6-8 tunaona kuwa kuna mashahidi watatu wa ukweli kuwa Yesu alikuwa na mwili. Damu inayomaanisha kusulubiwa kwake, na Roho ni ushuhuda wa ndani kwa Wakristo. Maji yanamaanisha kubatizwa kwa Yesu na Yohana, au yawezekana maji yanayomzunguka mtoto wakati wa kuzaliwa.
Yafuatayo ni mambo mbalimbai ambayo Biblia inatufundisha kuhusu nafsi ya Roho Mtakatifu.

Parakletos (mfariji, yeye anayekuwa pamoja nasi - Yohana 14:16, 26; 15:26)
Hufahamu mawazo ya ndani ya Mungu (1 Korintho 2:10-11)
Huongea nasi (Mdo 13:2; Ebr 3:7)
Huongea nasi (Mdo 13:2; Ebr 3:7)
Hutufundisha (Yohana 14:26)
Kama mzazi, ili kwamba tusiwe yatima (orphanos kwenye Kigiriki - Yohana 14:18)
Hutuongoza (Yohana 16:13)
Hutufundisha (Yohana 14:26; 1 Kor 2:13)
Huishi ndani yetu (1 Kor 3:16; 2 Tim 1:14; Rum 8:9, 11; Efe 2:22)
Mioyoni mwetu (2 Kor 1:22; Gal 4:6)
Mioyoni mwetu (2 Kor 1:22; Gal 4:6)
Hutuombea (vitu visivyo na uhai haviombi au kuombea - Rum 8:26-27)
Anaweza kufanyiwa jeuri (Ebr 10:29)
Humshuhudia Kristo (Yohana 15:26)
Anao ufahamu (Rum 8:27)
Anao ufahamu (Rum 8:27)
Anaweweza kuhuzunishwa (Isa 63:10; Efe 4:30)
Hufanya maamuzi (1 Kor 12:11)
Hufanya maamuzi (1 Kor 12:11)
Hupenda (Rum 15:30)
Anaweza kupendezwa na mambo (Mdo 15:28)
Huchunguza mambo ya ndani ya Mungu (1 Kor 2:9-10)
Huugua (na kwa ajili hiyo hutujali - Rum 8:26)
USIKOSE SEHEMU YA TATU
Kwenye Mwa 1:10, ilikuwaje Mung aumbe dunia wakati dunia ilikuwa tayari imeishaumbwa kwenye Mwa 1:1?
Kwenye Mwa 1:10, ilikuwaje Mung aumbe dunia wakati dunia ilikuwa tayari imeishaumbwa kwenye Mwa 1:1?
Shalom,
Max Shimba Ministries
No comments:
Post a Comment