Sunday, April 30, 2017

UNAZIJUA KAMBA ZA MAUTI ZILIZO KUFUNGA?

Image may contain: 1 person, text
Habari njema ni kuwa waliofungwa na kamba za mauti leo hii watawekwa huru na kufunguliwa kwa Jina la Yesu. Lengo la kufungwa na kamba za mauti ni kusababisha kifo; kifo katika uwezo wako wa kuomba, kifo cha uwezo wa kumtumikia Mungu, kifo cha uwezo wa kufanya kazi n.k.
Zaburi 18:4…[Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.]…
Ina maana Daudi alikuwa anatembea kama wewe na mimi lakini tayari katika ulimwengu wa roho Daudi amejiona akiwa amefungwa kamba za mauti.
Zaburi 116:3….[Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;]...
Pindi ufungwapo kamba za mauti, shida za kuzimu zitaanza kukufuata. Kamba za mauti ni 'ishara ya kifo'. Sanda vivyo hivyo, huvishwa watu wanapokuwa wamepoteza uhai wao (wafu).
Endapo watoto wako watakuwa wamefungwa kamba za mauti, utakuta kuwa, wale waliowafunga wameshawafanya 'maiti' ingawa wanatembea. Kwa hiyo, mtu anakuwa hai kimwili lakini katika ulimwengu wa roho mtu huyo walishamuua na hata pengine walishaadhimisha ‘arobaini’ ya huyo mtu bila yeye kujua.
MAOMBI: kwa Jina la Yesu , Ewe kamba uliyefungwa kwenye hatua zangu za maendeleo, funguka, kamba iliyofunga elimu yangu, kamba iliyofunga sura yangu isionekane, nakuamuru funguka na uondoke kwa Jina la Yesu. Amen
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

 

TRENDING NOW