Sunday, April 30, 2017

YESU NI MUNGU KUTOKANA NA QURAN (SEHEMU YA NNE)

Image may contain: text
1. Allah kasema Yesu ni NENO
2. Biblia inasema kuwa Neno ni Mungu
Allah anasema kuwa Yesu wa Quran ni NENO litokalo kwake. Ikiimaanisha kuwa, asili ya Yesu si binadamu bali ni Neno litokalo kwa Mungu. Quran hiyo hiyo inasema kuwa Neno la Allah halina mwanzo, ikiimaanisha kuwa NENO la Allah lilikuwa na Allah karne zote na NENO la Allah halikuumbwa. (Allah's word is eternal) Sura 6:115, Sura 10:64, Sura 18:27.
Hebu tusome aya kutoka Quran kuwa Yesu ni NENO:
Surat Al Imran 45. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).
Quran inakiri kuwa Maryam alipata MWANA KWA KUPITIA NENO LA ALLAH. Hivyo basi Yesu asili yane ni NENO na sio binadamu. Rejea Surat Al Imran aya 45.
Surat An Nisaai 171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na NENO LAKE tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.
Allah anaendelea kusema kuwa Yesu ni NENO LAKE. Kumbe basi Yesu ambaye ni Neno la Mungu alikuwa na Mungu siku zote. Soma Sura 6:115, Sura 10:64, Sura 18:27.
Je Biblia nayo inasema nini kuhusu NENO?
BIBLIA INASEMA KUWA NENO NI MUNGU
Yohana 1: 1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye NENO alikuwa Mungu.
Katika Yohana Sura ya Kwanza aya ya Kwanza, tunafundishwa kuwa NENO alikuwepo na Mungu hapo Mwanzo kabla ya kuumbwa kitu chochote kile. Wakati huo huo, Quran nayo inasema kuwa Allah aliumba Yesu kwa kutumia Neno ambalo lilikuwa na Allah tokea Mwanzo.
Ningependa mfahamu kuwa, Quran ambayo inasema kuwa Yesu aliumbwa kutoka NENO iliandikwa miaka 632 baada ya Biblia. Ikimaanisha kuwa Biblia ndio ya kwanza kuandikwa halafu Quran ndio ikafuata.
ALLAH ANAKWAMBIA WEWE MWENYE SHAKA KUWA, KAMA HUAMINI ASEMAYO MAX SHIMBA, Basi waulize watu wa Kitabu. Sisi Wakristo na Wayahudi ndio watu wa Kitabu. Allah anamaanisha kuwa, Watu wa Kitabu ambao ni Sisi Wakristo na Wayahudi ndio tunayo haki na mamlaka ya kuthibitisha maneno ya Quran kama ni ya kweli au uongo. Soma
Surat Yunus 94. Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.
Aya hiyo katika Surat Yunus iliyoteremka Makka na kutafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani inathibitisha kuwa Watu wa Kitabu ndio wenye Mamlaka ya kuhakikisha na au thibitisha ukweli wa Quran. Hakika Mimi nathibitisha kuwa YESU NI NENO na NENO NI MUNGU, maana hayo yalisema miaka mia 632 kabla ya kuteremshwa kwa Surat Yunus Makka na yamo katika Injili kutokana na Yohana aya ya kwanza na sura ya kwanza.
Allah anamwambia Muhammad katia Suratul Yunus aya 94 kuwa, kama Muhammad anashaka na ukweli kuwa Yesu ni Neno na Neno ni Mungu. Basi Muhammad atuulize Wakristo kuwa, Je, hayo madai ya Allah ni ya kweli? Hakika Biblia imekamilika na kusema bila ya shaka yeyote ile kuwa Yesu ni Neno na Neno alikuwa na Mungu kabla ya Mwanzo kuwepo. Allah na yeye amekiri hayo kuwa Yesu ni Neno ambalo lilikuwa na Mungu hata kabla ya Mwanzo kuwepo.
Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni NENO na Biblia inasema kuwa NENO NI MUNGU.
Katika huduma yake,
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2015

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW