Thursday, September 22, 2016

MAMLAKA ULIYONAYO UNAPOLITUMIA JINA LA YESU KRISTO!


“Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” (Wafilipi 2:9-11)
Kwa mistari hii michache tunaona ya kuwa jina la Yesu kristo lina mamlaka MBINGUNI, DUNIANI na CHINI YA NCHI au KUZIMU.
“Kwa jina la Yesu kila goti lipigwe” maana yake jina la Yesu lipate heshima linavyostahili kila mahali.Likiwa mojawapo ya funguo za ufalme wa mbinguni, jina la Yesu linatupa MAMLAKA mbinguni, duniani na chini ya nchi.
Kwa mfano: tunaokolewa kwa jina la Yesu (matendo ya mitume 4:12). Tunazaliwa mara ya pili kwa jina la Yesu (yohana 1:12). Kwa maneno mengine kwa sababu ya jina lake, Yesu alisema; “Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu” (yohana 16:23-24)
Mtu anapata furaha iliyo timilifu anapoomba kwa jina la Yesu Kristo! Kwa nini? Kwa sababu akiomba kwa jina la Yesu Kristo – anapata kile alichoomba. Heshima yote hii ya kujibiwa maombi yetu na Mungu Baba inatokana na Jina la Yesu Kristo, aliye Bwana na mwokozi wetu. Yesu Kristo alisema, “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.” (yohana 12:26)
Hebu tuyatafakari maneno yafuatayo aliyoyasema Kristo juu ya mamlaka iliyomo katika Jina lake.
Biblia inasema, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu
-watatoa pepo;
-watasema kwa lugha mpya;
-watashika nyoka;
-hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;
-wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”. (marko 16:17-18).
Hebu na tuangalie kwa undani zaidi baadhi ya ishara alizosema zitatokea tukilitumia Jina la Yesu Kristo.
“Kwa Jina Langu watatoa pepo”
Yesu Kristo alitaka sisi tumwaminio tujue ya kuwa kwa jina lake tuna mamlaka juu ya mapepo. Ni vizuri ufahamu ya kuwa kwa kuwa umemwamini Kristo rohoni mwako kama Bwana na mwokozi wako, basi, una mamlaka yakuwatoa pepo mahali walipo! Ukijua pepo yuko mahali Fulani, una uwezo nanmamlaka ya kumtoa mahali hapo kwa jina la Yesu Kristo, naye atatii!!

Daktari Luka mwandishi wa kitabu cha matendo ya mitume, anaeleza uweza wa jina la Yesu Kristo juu ya pepo waliokuwa katika hiduma na Mtime Paulo huko Filipi, mji wa makedinia, anaposema hivi;
“Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.” (Matendo ya mitume 16:16-18)
Unaona jinsi mtume Paulo alivyofanya alipotambua kuwa huyo mtu aliyewafuata alikuwa na pepo? Paulo alimwambia yule pepo, “nakuamuru kwa jina la Yesu kristo, mtoke huyu”. Na yule pepo hakuwa nauwezo wa kubisha kwa kuwa anamfahamu Yesu Kristo na uwezo alionao juu ya shetani na kazi zake zote, kwa hiyo ilibidi atii amri hiyo. Biblia inasema akamtoka saa ile ile.
Na wewe ndivyo unavytakiwa kufanya unapotambua kuwa kuna mtu anayesumbuliwa na pepo. Bila wasiwasi mwamuru huyo pepo kwa kusema; ‘nakuamuru kwa Jina la Yesu Kristo mtoke huyu’. Naye atamtoka! Usiwe na hofu na kuanza kufikiri labda hatatoka, au labda atakudhuru wewe. Simama katika imani ya jina la Yesu Kristo lenye uwezo wa kutoa pepo. Tena kumbuka Yesu Kristo alisema, “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni. ” (luka 10:19-20).
Siku moja (Kama nilivyokuambia katika sura ya kwanza) nilipomaliza kufundisha neno la Mungu mahali fulani, mama mmoja aliniomba nimwombee ili maumivu aliyokuwa nayo kifuani yamwondoke.
Tukiwa tumesimama nikamwambia aweke mkono wake kifuani mahali alipokuwa naumwa, naye akafanya hivyo. Halafu mimi nikaweka kiganja change juu ya kiganya cha mkono wake aliouweka kifuani pake, na nikasema, “KWA JINA LA YESU KRISTO.”
Kabla sijaendelea na sentensi hiyo, Yule mama alianguka chini, na pepo likaanza kupiga kelele za hofu na kulalamika toka ndani yake. Nikaliamuru lile pepo limtoke, kwa kusema, “kwa jina la Yesu Kristo wa nazarethi, wewe pepo mtoke mama huyu sasa hivi.” Naye akamtoka saa ile ile. Yule mama akaamka akiwa mzima na maumivu aliyokuwa akiyasikia kifuani hayakuwepo tena!
“Kwa jina langu…wataweka mikono juuya wagonjwa…”
Kumbuka Yesu Kristo alisema, “na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.” (Marko 16:17)
Nakumbuka kuna wakati niliwahi kumsomea mstari huu msichana mdogo wa umri wa miaka kumi na miwili aliyekuwa anasumbuliwa na uvimbe katika pua zake na hata kumletea shida ya kupumua. Baada ya kumsomea maneno hayo ya Yesu Kristo, nilimuuliza kuwa anayamini, naye akajibu kuwa “ndiyo nayaamini”. Nikamwuliza tena; “Je! Unaamini kuwa utapona nikiweka mikono yangu juu ya pua yako kwa Jina la Yesu Kristo?” Naye akajibu tena, akasema, ndiyo.
Kwa hiyo nikaweka mkono wangu juu ya pua ya Yule msichana, na nikauamuru ule uvimbe katika pua utoweke, na nikamshukuru Mungu kwa uponyaji huo. Yule msichana akaondoka kurudi nyumbani kwao.Kesho yake nililetewa habari kuwa, Yule msichana amepona, na uvimbe uliokuwa unamsumbua puani haupo tena!
Ni furaha kujua kuwa tuna Jina lenye mamlaka namna hii – mbinguni, duniani na chini ya nchi (kuzimu). Wagonjwa wanapaya afya wakiombewa kwa jina la Yesu Kristo, kw a kuwa jina hili lina afya ndani yake.
Nakumbuka mwaka 1985 tukiwa na mke wangu mahali fulani, mtu fulani alitujia kwa ajili ya kuhitaji maombi; kwa kuwa alikuwa amesumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda ambao wakati huo ulikuwa si chini ya miaka kumi na mitano.
Sisi tuliposikia hayo tukamsomea neno la Mungu toka katika Biblia- marko 16:17,18 linalosema hivi;
“na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; waasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”
Baada ya kuzungumza naye Kwa kifupi juu ya maneno ya mganga mkuu _ Yesu Kristo, tuliweka mikono yetu juu ya tumbo lake na tukaomba kwa Mungu vidonda vya tumbo vipone. Baada ya maombi hayo tukamtangazia uponyaji – ya kuwa Yesu Kristo amekwisha mponya.
Sisi tuliondoka eneo hilo nakuelekea mahali pengine kwa ajili ya huduma, na baada ya siku kadhaa kupita tulipata barua kutoka kwa mtu huyo tuliyemwombea juu ya vidonda vya tumbo akitueleza jinsi alivyopokea uponyaji siku ile tulipomwombea, na jinsi anavyoendelea vizuri katika uponyaji huo, na kwamba anaweza hata kula chakula bila shida yoyote, ambacho hapo mwanzo alikuwa akila anapata maumivu makali – sasa akila hapati maumivu yoyote.
Jina la Yesu Kristo libarikiwe sana maana ni ngome imara – walio na shida hulikimbilia na kupata pumziko na msaada!!
Barikiwa sana katika Jina la Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW