Friday, September 9, 2016

UJUMBE KWA WAISLAMU WOTE;



Mwanamke aliyefumaniwa akizini
**************************************
YOHANA 8:1-11
1 Lakini Yesu akaenda katika Mlima wa Mizeituni.
2 Alfajiri na mapema Yesu akaja tena hekaluni, watu wote wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha.
3 Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote.
4 Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini.
5 Katika sheria, Mose alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, mpaka wafe. Sasa Wewe wasemaje?’’
6 Walimwuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki Mwanamke Aliyefumaniwa Akizini Lakini Yesu akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole Chake.
7 Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu ye yote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.’’
8 Akainama tena na kuandika ardhini.
9 Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Yesu akabaki peke Yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele Yake.
10 Yesu akainuka na kumwambia, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?’’
11 Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana.’’
Yesu akamwambia, “Hata Mimi sikuhukumu. Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena.’’
MUNGU AWAPE HEKIMA YA KUSOMA NENO LAKE (BIBLIA) MKAPATE NURU.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW