Tuesday, August 22, 2017

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA TATU)

No automatic alt text available.
Mapingamizi Tisa ya Kiislam na Maitikio Yake
Pingamizi la 1 la Waislam: Watu wengine mbali ya hawa kumi na moja hawajaziongelea aya za Shetani. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislam ambao hawakundika kuhusu aya za Shetani walkuwa Imam Muslim aliyeandika Sahih Muslim, Abu Dawud, Nas’ai, Ahmad bin Hanbal, and ibn Hisham.
Itikio: Kuna vitu vingi kwenye makusaniko ya Hadithi ambavyo havimo kwenye mikusanyiko mingine. Kwa mfano, Hadithi ndefu za Bukhari hazina mafundisho kuhuu sababu za kutoa zaka, adhabu ya kujilimbikizia vitu, na malaika wawili wanao mtembelea Muislam kila asubuhi kama yanavyopatikana kwenye Sahih Muslim juzuu ya 2 sura ya 371 na.2205, uk.484. Kama mfano wa pili, tunajua kuwa Ibn Hisham aliitumia Bukhari, lakini aliiacha sehemu inayohusu aya za Shetani. Kwenye nakala ya Ibn Hisham ya Ibn Ishaq, alisema aliondoa vitu alivyoona kuwa vibaya. Kama alijisikia aibu sana hata hakuweza kuziweka, huo sio uthibitisho kuwa hazikutokea.
Pingamizi la 2 la Waislam: Aya zinazodaiwa kuwa za Shetani haziendani sawa na sehemu nyingine ya Sura 53.
Itikio: Kumbuka kuwa sehemu ya sasa haikufuatia aya za Shetani, bali ilichukua nafasi zao. Pia nyakati zingine sehemu tofauti za Sura moja zilitolewa nyakati tofauti. Upande mmmoja, al-Wahidi alisema Muhammad alisema hadi maneno ya mwisho. Kwa upande mwingine, hatujui kuwa Sura yote ya Nyota (53) baada ya aya ya 22 iliandikwa wakati mmoja. Aya za 51-53 zinaonekana kuwa hazipo mahali ake kwani zinamongelea Muhammad mwenyewe.
Pingamizi la 3 la Waislam: Sura 53:19-21 inaweza kuwa ilikuwa mapema zaidi kuliko Sura zinazoongelea kunong’ona kwa Shetani.
Itikio: Tabari na ibn Sa’ad wanasema zilifunuliwa wakati mmoja na Sura 17:73-75. Hakuna mtu leo hii anayejua kwa uhakika wakati ambapo aya nyingi za Kurani ziliandikwa. Kwa upande mwingine, hata kama iliandikwa mapema haitaweza kukanusha maneno iliyoyasema. Kama Waislam wasahilina wanaiamini kabisa Kurani, ikiwa ni pamoja na Sura 17:73-75 na 22:52, watatakiwa kuamini kwamba Shetani anaongeza vitu kwenye Kurani. John Gilchrist, kwenye Muhammed and the Religion of Islam uk.120 anasema, "Hoja nyingine ni dhaifu kwa sababu hakuna ushahidi thabiti kuwa sehemu ya kwanza ya Surah 53 inaongelea miraj [kupaa kwa Muhammad] kulikotokea baada ya kuhamia Abyssinia. Kama ilivyokwishaonyeshwa, kuna uhakika wa kiasi kikubwa sana kuwa inaongelea moja ya ziara za mwanzo za Muhammad, ambazo Kurani yenyewe inaonyesha kuwa hazizidi mbili ambazo alizifanya wakati huduma yake ilipoanza. Kwa bahati mbaya inaonekana kuwa hoja zote za Waislam za uhalisi wa vipingamizi vya habari hii ni dhaifu."
Pingamizi la 4 la Waislam: Aya za Shetani zinapingana na mafundisho ya msingi kuwa kuna Mungu mmoja ambayo Muhammad alishikilia kufundisha.
Itikio: Muhammad hajawahi kuthibitishwa kushikilia kitu chochote kile. Kumbuka, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 10 na.490, uk.317; juzuu ya 4 kitabu cha 53 sura ya 38 kabla ya na.400, uk.266; juzuu ya 8 kitabu cha 53 sura ya 38 na.400, uk.267 inarekodi kuwa Muhammad alikuwa amerogwa na mwovu kwa kipindi fulani. Isitoshe waandishi wa maisha yake na watu wengine waliorekodi jambo hili walikuwa bado Waislam, kwa hiyo wana historia hawa wanathibitisha kuwa kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa tayari kumfuata Muhammad hata kama alisema uongo.
Pingamizi la 5 la Waislam: Vifungu vingi kwenye Kurani vinasema Muhammad hakuweza kusema maneno yoyote yasiyokuwa kweli, na kwa ajili hiyo jambo hili haliendani na tafsiri kuwa Shetani anaingilia mambo. Kwa mfano,
Sura 10:15b: "Sema; Si kwa ajili yangu, kwa hiari yangu, kubadilisha hili: Sifuati kitu chochote isipokuwa kile kilichofunuliwa kwangu…"
Sura 41:42: "Hakuna uongo unaoweza kulikaribia kutokea mbele au nyuma yake: Limetumwa na Yeye Aliyejaa Hekima na Mwenye Kustahili Sifa zote."
Sura 15:9: "Tumeutuma, bila shaka, Ujumbe; na tutaulinda kwa hakika (dhidi ya uharibifu)."
Sura 60:44-46: "Kama (Mjumbe) angetunga neno lolote kwa jina letu, Tungemkamata kwa mkono wa kulia na kisha tungeikata ateri ya moyo wake"
Itikio: Kwa upande mmoja, inadaiwa kuwa Shetani, siyo Muhammad, alitunga aya za Shetani, na kulindwa kwa Kurani haukanushi kuingia kwa mafundhisho ya uongo na Mungu kuyarekebisha. Kwa upande mwingine, kama Muislam anatafsiri aya hizi kuwa zinafundisha kwamba hakuna kitu cha uongo kitakachoweza kuingia ujumbe wa nabii, hata kama aya za Shetani hazitahusishwa, jambo hili litakuwa kinyume na kunong’oneza kwa Shetani ambako kumeelezwa kwenye Kurani.
USIKOSE SEHEMU YA NNE
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW