Tuesday, August 22, 2017

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: text
Leo, ponografia imeenea sana na kukubaliwa na watu wengi katika jamii ya kisasa. Wakati mmoja ponografia ilipatikana katika sinema fulani tu za kimahaba na katika mitaa ya makahaba, lakini sasa imeenea kwa wingi katika jamii nyingi. Nchini Marekani pekee, ponografia ni biashara inayochuma zaidi ya dola bilioni kumi kila mwaka!
Biblia inatuhimiza hivi: “Mambo yoyote yaliyo safi kiadili, mambo yoyote yaliyo ya kupendeka, mambo yoyote yaliyo ya kusemwa vema, wema wa adili wowote ulioko . . . endeleeni kufikiria mambo haya.” (Wafilipi 4:8) Mtu anayetazama ponografia na kuijaza akilini mwake analikataa himizo la Paulo. Ponografia haina kiasi kwa sababu inafunulia watu wote mambo ya siri na ya faragha. Ni tendo la kipumbavu kwa sababu linamshusha mhusika na kushusha heshima. Hilo si tendo la upendo kwa kuwa halichangii hali ya kuwajali wengine. Hilo hukazia tu tamaa ya mtu binafsi.
Kwa kuonyesha matendo yasiyo ya kiadili na yaliyopotoka kingono, ponografia hudhoofisha na kuharibu jitihada ya Mkristo ya ‘kuchukia mabaya.’ (Amosi 5:15) Ponografia huwatia watu moyo kufanya dhambi na ni kinyume kabisa cha himizo la Paulo kwa Waefeso la kuacha ‘uasherati na ukosefu wa usafi wa kila namna au pupa hata visitajwe hata miongoni mwao, kama vile ifaavyo watu watakatifu; wala mwenendo wa aibu wala kufanya mzaha wenye aibu, mambo yasiyofaa.’—Waefeso 5:3, 4.
Kwa kweli ponografia haikosi kuleta madhara. Hiyo hutumikisha na kufisidi. Inaweza kuharibu mahusiano mazuri, na kupotosha njia ya kiasili ya kuonyesha ukaribu wa kingono kuwa uraibu wa kutazama picha za kiponografia. Hiyo huharibu akili na hali ya kiroho ya mraibu. Hiyo hukuza ubinafsi, pupa na kumfanya mtu kuwaona wengine kama vyombo tu vya kutosheleza tamaa zao. Hiyo huharibu jitihada ya mtu ya kufanya mema na kuwa na dhamiri safi. Jambo baya hata zaidi, ponografia inaweza kuathiri vibaya au hata kuharibu kabisa uhusiano wa mtu wa kiroho pamoja na Mungu. (Waefeso 4:17-19) Kwa kweli, ponografia ni janga linalopasa kuepukwa.—Mithali 4:14, 15.
USIKOSE SEHEMU YA TATU
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW