Tuesday, August 22, 2017

PASIPO YESU SISI HATUWEZI KUFANYA NENO LOLOTE

Image may contain: one or more people and text
Yohana 15: 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Ni muhimu wakati wote kukumbuka kwamba utoshelevu wetu watoka kwa Yesu (2 WAKORINTHO 3:5). Sisi ni matawi. Matawi yasipopata chakula na maji kutoka kwenye mizizi, hunyauka na kufa. Uwezo wetu wa kufanya neno lolote, unatoka kwa Yesu aliye mizizi. Bila yeye hatuwezi kufanya neno lolote. Hapa neno halisemi bila Yeye hatuwezi kufanya NENO LOLOTE KUBWA, kama kufufua watu, kuponya walio na Ukimwi n.k., neno linasema hatuwezi kufanya neno lolote hata lililo dogo. Katika yote, WAKATI WOTE, hatuna budi kuitumainia NEEMA ya Mungu na kamwe tusijitumainie wenyewe HATUWEZI! (2 WAKORINTHO 1:8-9; 12:9).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW