Tuesday, August 22, 2017

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA TANO)

Image may contain: text


Madhara Yanayosababishwa na Ponografia:
Habari ya kila aina kuhusu ngono inapatikana kwa urahisi kupitia televisheni, sinema, video za muziki, na Internet. Je, ni kweli kwamba habari hizo chungu nzima za ponografia hazina madhara, kama watu wengi wanavyotaka tuamini?*
Jinsi Ponografia Inavyowaathiri Watu Wazima:
Hata watetezi waseme nini, ponografia inaathiri sana maoni ya watu kuhusu ngono na maadili. Watafiti kwenye Hazina ya Taifa ya Utafiti na Uelimishaji wa Jamii walikata kauli kwamba “kutazama ponografia kunaweza kuwafanya watazamaji wafanye ngono potovu.” Ripoti hiyo inasema “imani ya kwamba wanawake husababisha na hufurahia ubakaji, na kwamba wabakaji ni watu wa kawaida imeenea sana miongoni mwa wanaume wenye zoea la kutazama ponografia.”
Watafiti fulani wanasema kwamba kuzoea kutazama ponografia kunaweza kuathiri uwezo wa kufurahia na kufanya ngono katika ndoa. Dakt. Victor Cline, mtaalamu wa kutibu watu wanaotawaliwa na mambo ya ngono, ametambua kwamba watu wanaotazama ponografia huendelea tu bila kuacha. Mtu anayeanza kutazama ponografia kidogo-kidogo, asipoacha mwishowe anaweza kuwa na zoea la kusoma habari na kutazama picha chafu zaidi za ponografia. Cline anadai kwamba zoea hilo linaweza kuongoza kwenye matendo mapotovu ya ngono. Wanasayansi wanaochunguza tabia za wanadamu wanakubaliana na jambo hilo. Dakt. Cline anaripoti kwamba “upotovu wowote wa ngono unaweza kuanza hivyo . . . na kwamba mtu hawezi kuacha hata akisumbuliwa sana na dhamiri.” Hatimaye, huenda mtu anayetazama ponografia akajaribu kufanya mambo yasiyo ya adili aliyoona, na mara nyingi matokeo huwa mabaya.
Tatizo hilo linaweza kuanza hatua kwa hatua bila kutambuliwa, asema Cline. Aongeza: “Huongezeka na kuenea kama kansa. Kwa kawaida zoea hilo halikomi, wala haliwezi kutatuliwa kwa urahisi. Haishangazi kwamba mara nyingi wanaume waliozoea kutazama ponografia hawakubali kwamba wana tatizo, na ni kawaida kwa wenzi wa ndoa kukosana, nyakati nyingine kutalikiana, na hata mahusiano mengine ya karibu huharibika kwa sababu hiyo.”
USIKOSE SEHEMU YA SITA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi Wetu.

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW