Tuesday, August 22, 2017

ALLAH ALIPATAJE MABINTI WATATU LAT, UZZA NA MANNAT BILA YA MKE? (SEHEMU YA KWANZA)

Image may contain: one or more people and people standing
TAFADHALI SOMA KISA HIKI CHA KUSISIMUA
Mara nyingi Waislam wamekuwa wepesi kuwaambia watu wengine kuwa Mungu ameruhusu Biblia kupotoshwa. Kitu wanachodokeza ni kuwa Kurani leo hii ni neno la Mungu lenye kuaminika wakati ambapo Biblia sivyo. Biblia ina maandiko yanayotofautiana mengi yenye tofauti ndogo, lakini ushahidi wa mabadiliko ya mafundisho hauna uzito. Kurani ina ushahidi mkubwa zaidi wa kupotoshwa kwa mujibu wa Ubai, aya zilizobatilishwa‘Uthman, na matatizo mengine ya Kurani. Hata hivyo, tofauti kubwa zaidi ya mafundisho ya Kurani, iliyoletwa na Waislam wenyewe, ni "mabinti wa Allah."
Muhtasari
Tovuti ya Kikristo http://answering-islam.org/Responses/Saifullah/sverses.htm inasema, "Moja ya matukio yenye kuaibisha zaidi kwenye maisha ya Muhammad lilitokea wakati Shetani alipoweka maneno yake kwenye mdomo wa Muhammad. Muhammad alisema maneno ya Shetani kama neno la Mungu. Tukio hili limethibitishwa kwa maandishi na waandishi kadhaa wa Kiislam wa kale na limeongelewa kwenye Hadithi na Kurani. Waislam wa miaka iliyofuata, kwa kujisikia aibu kuwa nabii wao aliyejitangaza mwenyewe amesema maneno ya Shetani, walikana kuwa tukio hili lilitokea. Visingizio na kukana kwingi vimekuwa vikitolewa na hawa Waislam wa miaka iliyofuata ili kulifunika kosa lenye kuhusisha dhambi la Muhammad.
Ni muhimu ikafahamika tena kuwa tukio la ‘Aya za Shetani’ si jambo ambalo limetungwa na watu wasiokuwa Waislam. Tukio hili limerekodiwa na vyazo vya kale zaidi vya Kiislam vilivyokuwepo wakati wa uhai wa Muhammad. Mtu yoyote asifikiri kuwa jambo hili ni hadithi iliyotungwa na watu wenye kuupinga Uislam. Ni kisa kinachopatikana moja kwa moja kwenye rekodi za kale za Kiislam.
Hili moja ya masomo yenye kubishaniwa zaidi kwenye Uislam. Shetani alimsababishia Muhammad kunena maneno yake (Shetani) kama maneno ya Mungu."
Je Kurani Ilisema Nini Mwanzoni?
Sura ya Nyota (Sura 53) mistari ya 19-20 inasema, "Je umemwona Lat, na ‘Uzza, Na mwingine, (mungu mke) wa tata, Manat?"
Allah alikuwa maarufu huko Arabia kabla ya kuja kwa uislam, kama mungu aliyekuwa na mabinti watatu: al-Lat, al-Uzza, na Manat. (Kumbuka kuwa al- inamaanisha ‘yule’, kwa Kiingereza "the".)
Waandishi wanne wa mwanzo wa maisha ya Muhammad waliandika kuwa awali aya hizi zilifuatwa na:
"Hawa ni mawinchi (wasuluhishi) ambao maombi yao yanapaswa kutumainiwa"
Tafsiri: Mabinti wa Allah walifikiriwa kuwa viumbe wa mbinguni wenye kuomba kwa ajili ya wengine. Mawinchi marefu ya Kinumidia ilikuwa ni sitiari yao. Maneno mbadala ya "inatakiwa kutumainiwa" (turtaja) ni "imekubaliwa kwa kuthibitishwa" (turtada). (Kutoka kwenye tafsiri ya Alfred Guillaume ya The Life of Mohammed, iliyoandikwa na Ibn Ishaq, uk.166.
Baadaye, kifungu hiki kiliondolewa na kifungu kifuatacho kiliwekwa badala yake:
"Nini! Kwako wewe mwenye jinsia ya kiume, Na kwake (mwanaume), mwanamke? Tazama, hakika mgawanyo huu hautakuwa wa haki kabisa." (aya za 53:21-22 leo)
Tafsiri: Wale wanaoamini kuwa Allah alikuwa na mabinti watatu hawakuntendea haki Allah, kwa sababu walipendelea watoto wa kiume ingawa walisema kuwa Allah alikuwa na wasichana tu.
Hizi ndizo ambazo zimeitwa "Aya za Shetani." Katika nyakati za sasa Salmon Rushdie alitumia msemo huu tu kwenye kichwa cha riwaya yake ya kubuniwa na isiyohusika na aya hizi, na andiko hili halikiongelei kisa hiki cha kisasa. Kwa upande wa Aya za Sheatani za asili, Muislam au mtu mwingine asiyekuwa Muislam mwenye kutazama jambo hil bila upendeleo anawezaje kujua aya ambazo zilikuwemo toka awali? Sehemu iliyobaki ya andiko hili inatoa ushahidi wa moja kwa moja na ule usio wa moja kwa moja kuwa Aya za Shetani zilikuwemo asilia, na mapingamizi tisa ya Kiislam.
Waandishi Wanne wa Maisha ya Muhammad: Ushahidi wa Moja kwa Moja
Ingawa si kila kitu Waislam wa kale walichosema kuhusu Muhammad kilikuwa kweli, wanazuoni wa kiislam wana uwezekano mkubwa zaidi wa kukubali mambo ambayo Muhammad aliyasema ambayo yameshuhudiwa na vyanzo vitatu au zaidi. Tunajua kuwa Aya za Shetani hazikutokana na vyanzo visivyokuwa vya kiislam, lakini kutoka wanazuoni wanne tofauti wa kale wa kiislam ambao walikuwa waandishi wa maisha ya Muhammad. Kumbuka kuwa watatu kati ya waandishi hawa walisimulia maisha ya Muhammad hata kabla ya mkusanyiko mashuhuri wa Hadithi ambao dhehebu la Kiisuni limejengeka juu yake.
Al-Wahidi/Wakidi (aliyekufa mwaka 207/823 BK) aliandika Asbab al-Nozul. "Kwenye siku fulani, wakuu wa Maka, walikusanyika kwenye kundi pembeni mwa Kaaba, walijadili kama ilivyo kawaida ya mambo ya mji wao; wakati Muhammad alipotokea na, kukaa karibu yao kwa namna ya kirafiki, alianza kusema sura 53 huku wakimsikia…. ‘Na usimwangalie Lat na Ozza, na Manat wa tatu zaidi?’ Alipofika kwenye aya hii, mwovu alipendekeza njia ya kujieleza mawazo yake ambayo iliitawala nafsi yake kwa siku nyingi; na aliweka mdomoni mwake maneno ya upatanisho na masikilizano, ufunuo aliokuwa anausubiri kwa hamu kubwa sana toka kwa Mungu, yaani; ‘Hawa ni wanawake waliotukuka, na hakika maombezi yao yanatakiwa kutumainiwa. ’ Wakoreish walishangazwa na kufurahishwa na kukubaliwa huku kwa miungu yao; na kama Mahomet alivyoimalizia Sura kwa maneno ya hitimisho ‘Kwa hiyo inama mbele ya Mungu, na mtumikie’ kusanyiko zima lilijiinamisha kwa moyo mmoja chini na kuabudu. … Jioni Gabriel alimtembelea; na nabii aliisema Sura hiyo kwake. Na Gabriel alisema, ‘Umefanya kitu gani? Umeyarudia mbele ya watu maneno ambayo sikuwahi kukupa’. Kwa hiyo Muhammad alisononeka zaidi …"
Ibn Sa’ad/Sa’d (aliyekufa mwaka 230/845 BK), aliifahamu kazi ya al-Wahidi lakini yeye mwenyewe alikuwa mwandishi wa habari za maisha ya watu aliyeandika kitabu chenye juzuu 15 kiitwacho Kitab al Tabaqat al Kabir.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Shalom,

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW