Tuesday, August 22, 2017

UNAYAJUA MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA UTUPU "PONOGRAFIA"? (SEHEMU YA SITA)

Image may contain: one or more people and text
Jinsi Vijana wanavyoathiriwa na picha za utupu:
Takwimu zinaonyesha kwamba watazamaji wengi wa ponografia ni wavulana wenye umri wa kati ya miaka 12 na 17. Kwa kweli, wengi wao hujifunza masuala ya ngono hasa kupitia ponografia. Hilo lina matokeo mabaya sana. Ripoti moja yasema kwamba “ponografia hazionyeshi kamwe mimba za matineja na magonjwa yanayoambukizwa kingono kama UKIMWI, na hilo hutokeza wazo la uwongo la kwamba mambo yanayoonyeshwa katika ponografia hayana madhara.”
Watafiti fulani husema kwamba kutazama ponografia kunaweza pia kuathiri ukuzi wa kawaida wa ubongo wa mtoto. Dakt. Judith Reisman, mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Vyombo vya Habari, akata kauli: “Uchunguzi wa athari za sauti na picha za ponografia katika utendaji wa kawaida wa ubongo unaonyesha kwamba kutazama ponografia huathiri kabisa uwezo wa kawaida wa kufikiri. Pia hudhuru ubongo wa watoto unaoathiriwa kwa urahisi kwa sababu hufanya wasione mambo kihalisi na hudhuru afya yao ya kiakili na ya kimwili, na huwazuia kupata furaha.”
Jinsi Mahusiano yanavyoathiriwa na unagaliaji wa ponografia:
Ponografia huathiri mitazamo na tabia. Ujumbe wake unavutia hasa kwa sababu si halisi na hivyo unaifanya ionekane kuwa yenye kusisimua zaidi kuliko mambo halisi. (Ona sanduku “Utakubali Ujumbe Gani?”) “Watu wanaotazama ponografia hutarajia mambo yasiyo halisi ambayo huharibu mahusiano,” yasema ripoti moja.
Ponografia inaweza kuwafanya wenzi wa ndoa wakose kuwa wanyofu na wakose kuaminiana, sifa ambazo ni muhimu katika ndoa. Kwa sababu ponografia hutazamwa hasa faraghani, mara nyingi humfanya mtu atumie hila na uwongo. Wenzi wa ndoa huhisi kwamba wamesalitiwa. Hawaelewi kwa nini mwenzi wao havutiwi nao tena.
USIKOSE SEHEMU YA SABA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW