Tuesday, August 22, 2017

KAMA UNAMPENDA RAFIKI YAKO, MWAMBIE UKWELI AMBAO NI MCHUNGU

Image may contain: one or more people and text
Wengi tumejikuta tukiona ni vyema tukaambiwa yasiyo na ukweli maishani mwetu na kudanganywa ilimradi tu yanaturidhisha wakati huo lakini ajabu tunachukia na kutopenda ukweli ambao hata kama unaumiza lakini faida yake ni kubwa sasa na pia mbele twendako.
MITHALI 27: 5 Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika. 
6 Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; Bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
7 Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali; Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa kitamu.
Huwa natumiwa lawama kila siku, kwanini natoa mada chungu kwa Waislam kila siku?
Leo nimewajibu wale wote wanao ulizo hilo swali kwa kutumia aya.
Ukweli unaweza kukumiza lakini, kwa kusema uongo unaweza kuumia milele,Ni wazi kuwa watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli, na wakati mwingi baadhi ya watu husema uongo huku wakifikiri kufanya hivyo ni kujipa matumaini katika jambo fulani, lakini ukikaa na kufikiria unaposema uongo au unapokataa ukweli ujue unajidanganya mwenyewe na siku zote utabaki kuwa na maumivu moyoni mwako kutokana na kuishi na uongo ndani ya moyo wako.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW