Sunday, August 6, 2017

ALLAH KATEREMSHA AYA NA KUAPA KWA YESU KRISTO MUNGU WAKE MKUU

Image may contain: text
Kwanza tujifunze maana ya kuapa ili tuweze elewa kwanini Allah aliapa kwa Yehova.
Nini maana ya kuapa?
Kuapa, au Kula kiapo, au Kula Yamini, kunamaanisha kumthibitishia, kwa kutumia Jina la Mwenyezi Mungu, kwamba jambo fulani linaloapiwa – na ambalo halina ushahidi wazi wazi- ni kweli na sahihi kama linavyodaiwa na mwenye kula kiapo hicho na hivyo basi ni budi kusadikiwa madai hayo kwani Mdhamini Mkuu ni Mwenyezi Mungu, Mjuzi Pekee wa ukweli au uwongo wa mambo yaliyofichika nyoyoni!
katika Hadithi iliyopokelewe na Abdallah bin `Umar R.A.A. na iliyotolewa na L-Bukhari, “
"إِنَّ اللَّهَ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ ، فَمَنْ كَانَ حَالِفًا فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ أو فَلْيَصْمُتْ"
Maana yake, “Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kuapa kwa baba zenu, atakaeapa aape kwa Mwenyezi Mungu au anyamaze
Sasa tumsome Allah ambaye sio Yehova "Yahuh", je yeye anaapa kwa nani?
Qurani 91:1-7 Suratul Ash-Shams (Jua)
Naapa kwa jua na kwa mwangaza wake. Na kwa mwezi napoliandama. Na kwa mchana unapolidhihirisha. Na kwa usiku unapolifunika.Na kwa mbingu na kwa Aliyezijenga. Na kwa ardhi na Aliyeitandaza. Na kwa nafsi (roho) na Aliyeitengeneza.
Qurani 92:1-3 Suratul Al-Layl (Usiku)
Naapa kwa usiku ufunikapo (kila kitu). Na kwa mchana uangazapo. Na kwa aliyeumba kiume na kike.
Hapa tunaona Allah anayeabudiwa na Waislamu anaapa kwa mbingu na kwa aliyezinjenga, kwa ardhi na aliyeitandaza.
Je, huyo mtandazi wa ardhi na mjengaji wa mbingu ni nani?
Kwa maana Allah wa Islam, anaapa kwake. Jibu unalo, Mungu Yehova Kaumba kiume na Kike, Mungu Yehova Kaumba Mbingu na Nchi, lakini Allah anaapa kwa aliye umba Mbingu na Nchi pamoja na aliye umba kiume na Kike. Allah anaapa kwa Yehova, Mungu wa Wakristo.
Je Nani kaumba Kiume na Kike?
QURAN 92 1-3
1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..
Hivi mtu anaye apa kwa mwengine anakuwa Mungu au binadamu?
Je, nani kaumba hapo. Maana Allah anaapa kwa aliye umba, na kuumba ni sifa ya Mungu. Kumbe Allah hakuumba.
Je, ni nani huyu aliye umba Kiume na Kike ambaye Allah wa Islam anaapa kwake?
Endelea kusoma...kutoka Biblia Takatifu….
Yeremia 27: 5 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.
Sasa tunamsoma Yehovah ambaye ni Mungu wa Biblia kuwa yeye ndie aliye umba kila kitu, pamoja na Kiume na Kike ambacho Allah wa Islam anaapa kwake. Kwahiyo, Jehovah aliumba kiume na kike, na Allah wa Islam anaapa kwake, sasa jaza mwenyewe nani ni Mungu?
Je, Mungu anaweza kuapa kwa Mwengine? Endelea kupata elimu …
Waebrania 6:13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.
Jehova anasema hakuna Mkubwa wangu wa kuapa kwake, lakini Allah katika Kuran anasema kuwa yeye anaapa kwa aliye umba kiume na kike.
Hivyo basi leo tunafahamu kuwa aliye umba ni Jehona na Allah anaapa kwa Jehovah Mungu wa Biblia na Wakristo.
Mungu awabairiki sana
Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW