Sunday, August 6, 2017

MUHAMMAD ALIKUWA MTENDA DHAMBI LAKINI YESU HAKUWAI TENDA DHAMBI HATA MOJA

Image may contain: 2 people, outdoor
Wakati Biblia na Quran zinasema Yesu alikuwa hana dhambi na hakuwai tenda dhambi, hivi ndivyo Kuran na Bukhari Hadith zinavyosema kuhusu Muhammad. Katika sura 40:55 na 48:1-2, Allah anamwambia Muhammad kuomba msamaha kwa ajili ya dhambi zake (au udhaifu wake). Sasa, watu hawahitaji msamaha kwa ajili ya madhaifu ya miili bali maadili. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 sura ya 268 na.1695 uk.373 inasema Muhammad aliomba, "Nilijikosea mwenyewe na kufanya toba ya dhambi zangu. Nisamehe dhambi zangu . . ." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 2 sura ya 13 na.19 uk.23; juzuu ya 1.12.57 na. 781 uk. 434; juzuu ya 6.60.3 na. 3 uk.4; juzuu ya 8.75.3 na. 319 uk. 213; na juzuu ya 8.75.62 kabla ya na. 407 uk. 271 kabla ya kueleza dhambi za Muhammad. Mambo bayana yaliyoelezwa kwenye Bukhari juzuu ya 1.4.70 na.234 uk.148; Bukhari juzuu ya 8.82.1 na. 794-795 uk. 520 ni kukata watu mikono na miguu, kuchoma macho yao, na kuwanyima maji hadi kufa baada ya kukatwa miguu na mikono. Angalia Bukhari juzuu ya 8.82.3 na. 796 sura ya 4 uk. 797; Bukhari juzuu ya 6 sura ya 150 kabla ya na.198 uk.158-159 pia Fiqh us-Sunnah juzuu ya 1 uk.133.
Bila shaka utakubali kwamba hizi ni dhambi nzito sana. Kwa vile Muhammad alifanya hivi, alihitaji sana msamaha.
Swali la kidadisi ni hili: "Ni nani hasa anayelipa gharama ya dhambi zako?" Yesu alisema alilipa fidia ya dhambi zetu. Uislam haufundishi kuwa kuna mtu yeyote aliyelipa gharama. Je, dhambi zako zinalipwaje, au Allah anazifumbia macho baadhi ya dhambi na kuadhibu nyingine?
Watu wengine wanaweza kufikiri kuwa uovu hauna madhara yoyote ili mradi mtu anajiita Muislam. Katika karne hii Waislam wanawaua wakiristo na kufanya mauaji ya kinyama kwenye vijiji vyao katika nchi za Sudan, Nigeria na Indonesia. Wakati watu walioitwa wakristo waliwaua Waislam, watu walisema kuwa wanafanya kinyume cha tabia ya Kristo. Wakati Waislam wanawaua Wakristo, wanaomwabudu Mungu wa kweli, sijawahi kusikia mtu yeyote akisema wanafanya kinyume cha tabia ya Muhammad.
Nisamehe kwa kusema bila kuficha kiasi hiki, lakini mauaji ya watu wanaomwabudu Mungu yanayofanywa na Waislam lazima yaachwe. Waislam wanapohalalisha mauaji haya kwa sababu hata nabii wao alifanya hivyo, watu hushangazwa na nabii wao, na Allah wao ambaye anatengua neno lake, na chimbuko la Uislam.
Mfikirie Nabii asiyekuwa na dhambi tofauti na Muhammad, kuna mmoja ambaye alisema kuwa ni nabii wa Mungu alitimiza mamia ya unabii na maana zake hakuwahi kusamehewa, kwa sababu hakuwa na dhambi inayohitaji kusamehewa.
Hakuwahi kuua, wala kutishia maisha ya msafiri yeyote yule
alikuwa na kiwango cha juu sana cha uadilifu (hakuruhusu ufanyaji tendo la ndoa kwa kutumia nguvu) aliahidi kulipa adhabu ya dhambi zetu aliteseka na kufa kwa ajili yako, na
hana kaburi, kwani alifufuka kutoka katika wafu.
Huyu ni Yesu Kristo. Wakristo hawasemi kuhusu Yesu kuwa: "amani ya Mungu na iwe juu yake", Yesu ndiye mfalme wa amani; amani ya Mungu ipo juu yake. Lakini, tumaini langu ni kuwa utaweza kujua namna ya kuona kuwa amani na upendo wa Yesu vinaishi moyoni mwako.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW