Thursday, August 3, 2017

KWANINI ALLAH WA WAISLAM SIO MUNGU (SEHEMU YA TATU)

Image may contain: 1 person, text
MPANGO WA MUNGU KWA MWANADAMU
Mungu aliudhihirisha mpango wake kwa Mwanadamu kupitia Mitume na Manabii wake. Tunapo soma Zaburi Mlango wa Pili iliyo andikwa miaka 1000 KK tunajifunza kuwa Mungu alimfunua na kumtabulisha "MWANA WAKE WA PEKEE" na katika Zaburi 22 aliifunua kwa undani kuwa Mwana Wake wa Pekee atasulubiwa Msalabani.
Zaidi ya hapo, Mtume wa Mungu Isaya na yeye anatabiri hayo hayo katika Isaya 48 kuwa kuna Utatu katika Mungu miaka 700 KK.
Mungu anamtabulisha Mwana wake wa Pekee; Wakati Allah anapinga hili. Tukisoma Zaburi 2:7-8: 7 Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 8 Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
Lakini miaka 1600 baada ya Zaburi, Quran inakuja na kupinga haya.
[Sura 6.101] Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu.
Allah anapinga maneno ya Yehova aliyo ambiwa Daudi miaka 1000 Kabla ya Kuzaliwa Yesu.
Zaidi ya hapo, Allah anaendelea kupinga Utabiri wa Isaya unao husu Utatu. Isaya alisema: Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake. [Isaiah 48:16]
Lakini katika Sura 5:73 Allah anasema kuwa: Al Maida 73. Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru.
Yehova anasema kuhusu kusulubiwa kwa Yesu, wakati Allah anakuja mika mingi baadae na kupinga hilo:
Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli Na atazaliwa Bethlehem. Soma Mika 5:2 inazungumzia Yesu.
Zaidi ya hapo, Mitume na Manabii walitabiri kufa kwa Yesu kwa undani. Soma Zaburi 22, Isaya 53, Yuda kuchukia vipande 30 vya Silva Zakaria 11 na Jua litazama mchana saa 6 soma Amos 8 aya 9.
LAKINI, Allah anapinga haya yote mika mingi baadae kwa kusema: Surat An Nisaai 157. Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini
Yehova alimtambulisha Mwana na kuelezea kifo chake miaka 1000KK na zaidi ya hapo, alitueleza kuhusu Utatu Mtakatifu miaka 700KK, LAKINI Allah anapinga haya yote.
Kwa kiingereza naweza kusema kuwa:
God announces the sonship and describes the crucifixion about 1000BC and announces the Holy Trinity about 700BC, but Allah denies each element of God’s plan. Allah is not God.
ALLAH SIO MUNGU.
Shalom,
Max Shimba mtumnwa wa Yesu Kristo.

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW