Thursday, August 3, 2017

UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO (SEHEMU YA NANE)

Image may contain: mountain, text, nature and outdoor
Sauti ya dhamira umshuhudia Aliye Juu:
Tofauti na wanyama, mwanadamu mwenye ufahamu ana dhamira inayomsonda au "sauti ndogo" nafisini. Sauti hii hujuza mema ("fanya hivi") na mabaya ("usifanye hivyo"). Kama ladha ilivyo kwa vyakula ndivyo dhamira ilivyo kwa maadili. Dhamira uhukumu: umtetea mtu na kumletea amani; pengine, umshutumu na kumletea huzuni. Hata isemaje, watu wote hukubali ni vema kutii dhamira yako. Lakini, dhamira imepata wapi mamlaka hayo ya kusikilizwa? Kutoka maumbile yangu asilia? Iweje asili iliyo chini yangu inikalie? Iweje nihuzunike ninapoiasi ikiwa mimi ndiye niliyeitunga? Kama imepewa mamlaka na jamii iliyonilea, iweje wana jamii walio sawa nami wawe juu yangu? Ni nani aliye na sauti ya mwisho kunipeleleza niliye chini, halafu kuniruhusu au kunikataza kabla sijatenda, kunitetea au kunishtaki baada ya kutenda? Hakika, "pumzi [neshamah kiebrania, au roho, dhamira,] ya mwanadamu ni taa ya Bwana; hupeleleza yote yaliyomo ndani yake" (Mithali 20:27)
UNABII AINA TATU - HATIMA TATU
Baada ya kufika hapa, ni kitu cha manufaa kufanya muhtasari wa yale tuliyoona.
Babeli: Ile dola kuu kabisa Mashariki ya Kati, ilikuwa ipoteze mamlaka yake, na jiji lake kuu maridadi sana liwe mahame, likiepukwa na watu na wanyama pori. Na ndivyo ilivyotokea.
Misri: Nayo dola kuu nyingine, ingelibakia kuwa ufalme unaotambulika. Wamisri wangeendelea kukaa katika nchi yao wenyewe. Lakini mara zote wangetawaliwa na mamlaka zingine, wakibakia 'ufalme wa chini.' Na ndivyo ilivyokuwa.
Hatima ya Israeli haikuwa ya kufananishwa na yoyote kati ya hizi. Wakiwa wametawanywa mbali na nchi yao kwenye nchi nyingine, na kupata mateso makali na manyanyaso, wangerudi tena katika nchi ile ile walipotawanywa, na kujianzisha tena hapo.
Tuzingatie kwa makini yafuatayo:-
1. Unabii kuhusu mataifa haya ulitolewa kama miaka 2500 iliyopita.
2. Ukweli wake umekuwa matukio halisi ya kihistoria mpaka leo.
3. Mifano hiyo hapo juu ilihusu mamlaka tatu tofauti, zenye hatima tatu tofauti kabisa. Moja ilikuwa kutoweka; ya pili kubakia, lakini kukaliwa na mataifa mengine; ya tatu kuangamizwa, na watu wake kufukuzwa na kutawanywa dunia nzima, na bado hatimaye kurudishwa katika nchi ya awali.
4. Hii sio 'mitazamo ya mbeleni ya kisiasa,' ya wachunguzi wajanja wa kisiasa, bali ni utabiri usiokosea wa mambo.
Nani angeweza kujua?
Utabiri wa mambo wa muda mrefu hivyo unawezekanaje? Kuna jibu moja tu linaloridhisha; Lazima awepo aliyeyajua kabla; lakini ni nani?
Kwa hakika hakuna mtu wa miaka 2500 iliyopita au tangu hapo,
angeweza kujua. Tukiupima utabiri wa namna hii kibinadamu tu hauelezeki. Lakini hata hivyo, manabii wa Agano la Kale hawakudai wanatabiri kwa uwezo wao. Walisema walikuwa wakisema maneno yaliyotoka kwa Mungu. " Hivi ndivyo asemavyo BWANA," ndivyo walivyokuwa wakianza kusema wakati wote. Kama Mungu alikuwa nyuma ya yale waliyosema, tunapata jibu la nani aliyejua.' Hakuna maelezo mengine yanayoleta maana. Unabii tuliouchunguza hapa ulihitaji uwepo wa Mungu kama chanzo chake. Inaleta maana.
Mifano hii mtatu tuliyoinukulu ilichaguliwa kuonyesha aina tofauti za unabii wa Biblia. Lakini mifano iko mingi. Tungeweza, kwa mfano, kuchunguza ule unaomhusu Yesu Kristo: alipaswa kuwa na mzao wa Ibrahim, na wa Daudi; alikuwa azaliwe Bethlehem; alikuwa akataliwe na watu wake; na bado afe kifo cha upatanisho kwa ajili yao; na maelezo mengi mengineyo - yote yakiwa yametamkwa mamia ya miaka kabla hajazaliwa, na bado yakawa hivyo hivyo atika kuzaliwa, kwa Yesu, utumishi, kifo na kufufuka kwake.
Lakini tutahitimisha uchunguzi wetu mfupi kwa mifano miwili zaidi itakayoleta mpango wa kiunabii mpaka kufikia wakati tulionao.
====USIKOSE SEHEMU YA TISA ==== BIBLIA NA MATAIFA
Unabii wa Daniel unao mpango wa kuvutia unaohusu kukua na
kuanguka kwa dola, na hali ya mataifa ya kile kilichokuwa kikiitwa 'Dunia iliyostaarabika,' yaani mataifa ya Ulaya, Mashariki ya Kati, Misri na pwani ya kaskazini mwa Afrika, yote yanayoizunguka Bahari ya Kati (Mediterranean sea).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW