Wednesday, October 30, 2013

UKRISTO NI NINI?


Leo nitajibu hoja ya, Je, Ukristo ni DINI AU NI NINI?

Neno Ukristo ni tegemezi ya kutoka kwa Jina "KRISTO". Hivyobasi, Mkristo ni mfuasi wa Kristo. Ni kama unavyoweza sema Mtanzania anatoka Tanzania na/ua neno Mtanzania ni tegemezi kutoka Tanzania.

Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba kupitia Mwana ambaye ni Yesu. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.

Wakristo huamini ya kuwa Biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.

Kwa hivyo, huku dini nyingine zikitaka waumini wao watende mambo Fulani Fulani au wasitende mambo Fulani ukristo ni juu ya kuwa na ushirika na Mungu. 

Hivyo Basi, Ukristo ni Ufuasi wa Kristo ambaye ni Mungu. Yesu Kristo ni Mungu. 

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW