Saturday, January 26, 2019

UKRISTO BARANI AFRIKA

Image may contain: mountain, outdoor and nature
Ukristo barani Afrika una historia ndefu inayokaribia miaka elfu mbili.
Wakati mwingine tunaweza kusikia kuwa Ukristo uliingizwa Afrika juzijuzi tu, na asili yake ni Ulaya. Hili si kweli. Ukristo ni imani ya kale sana katika Afrika. Tangu mwanzo wa Kanisa walikuwepo Wakristo Waafrika.
Ukristo uko Afrika katika wingi wa madhehebu yaliyopatikana katika historia ya Kanisa, baadhi katika bara hilo, baadhi katika mabara mengine.
Kwa sasa ndiyo dini kubwa zaidi barani, hasa Kusini kwa Sahara, pamoja na Uislamu ambao unaongoza Kaskazini kwa jangwa hilo.
Leo karibu nusu ya Waafrika wote ni Wakristo. Lakini asilimia ya Wakristo inaweza kuwa ndogo katika nchi kadhaa na kubwa katika nchi nyingine. Katika Afrika Kaskazini Wakristo ni wachache. Kumbe ni wengi kwa theluthi mbili za bara kusini kwa Sahara.
Kwa jumla Wakristo wanaishi kati ya wafuasi wa dini nyingine, hasa Uislamu na dini za jadi.
Idadi yao inaongezeka haraka sana. Kila baada ya nukta nne Mwafrika mmoja anaingia Ukristo. Wengine huzaliwa katika familia ikiwa mzazi mmoja au wote wawili ni Wakristo tayari. Katika madhehebu mengi iko desturi ya kuwabatiza watoto wadogo. Ubatizo huo unawafanya kuwa wanakanisa. Wakikua watafundishwa na pengine kukaribishwa kwenye Kipaimara. Katika ibada hiyo kijana atarudia ahadi ya ubatizo wake na kuwekewa mikono na askofu au mchungaji mwingine na kuombewa ili Roho Mtakatifu amsaidie katika maisha yake ya Kikristo. Madhehebu mengine hayabatizi watoto wadogo. Yanaweza kuwapokea katika Kanisa kwa ibada maalumu lakini yanasubiri mpaka mtoto atakapokuwa mtu mzima, halafu apokee ubatizo na kuwa Mkristo rasmi.
Njia nyingine ya kukua kwa Kanisa ni kuongoka. Maana yake mtu asiye Mkristo anasikia habari za imani na kuvutiwa moyoni. Halafu anafika kwa kiongozi wa Kanisa na kupata mafundisho juu ya imani na maisha ya Kikristo. Halafu anaweza kubatizwa. Atakuwa mwanakanisa katika dhehebu fulani lakini ni vilevile Mkristo katika Kanisa moja takatifu la Bwana Yesu lililopo popote duniani. Wakristo Waafrika wengi kidogo ni watu walioongoka: waliwahi kuwa wafuasi wa dini nyingine (hasa dini za jadi, lakini wengine Uislamu), wakasikia Habari Njema wakaamua kumfuata Yesu.
Ukristo nchini Tanzania ulianzishwa na wamisionari wa Shirika la Mt. Agostino kutoka Ureno walioongozana na Vasco da Gama mwaka 1499 hadi Zanzibar.
Huko walijenga konventi ya shirika lao ili kuhudumia kiroho Wakristo toka Ulaya tu.
Misheni ilipingwa na Waarabu Waislamu na e kukoma mwaka 1698, kisiwa hicho kilipotekwa na Waarabu wa Oman.
Uinjilishaji ulifanikiwa zaidi katika sehemu ya pili ya karne ya 19 hasa ulipofanyika katika maeneo ya bara.
Kati ya Waprotestanti, waliotangulia walikuwa wamisionari Krapf na Rebmann waliotumwa na chama cha C.M.S.; kutoka kwa kituo chao karibu na Mombasa walifika mpaka eneo la Tanzania ya leo. Kituo cha kwanza cha C.M.S. katika Tanganyika kilikuwa Mpwapwa mwaka 1876.
Mapadri Wakatoliki wa kwanza pamoja na masista walitokea Reunion wakakaa Unguja tangu tarehe 12 Desemba 1860 hadi mwaka 1863, walipokabidhi misheni kwa shirika la mapadri wa Roho Mtakatifu. Halafu hao mwaka 1868 wakafungua huko Bagamoyo kituo cha kukalisha watumwa waliowanunua na kuwapa uhuru. Walifuatwa na Mapadri Weupe (1878) walioanza mwaka 1879 kwenye Ziwa Tanganyika.
Katika mazingira ya Kanisa la Anglikana chama cha Misheni ya Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati U.M.C.A. (Universities` Mission to Central Africa) kiliundwa kutekeleza wito kutoka David Livingstone kuhubiri Injili na kukomesha utumwa katika Afrika. Waliingia kule Zanzibar mwaka 1864, wakajenga kanisa kuu mahali pa soko la watumwa lililofungwa, altari ikiwa imejengwa juu ya nafasi ya mti wa kuwafunga watumwa walioadhibiwa kwa viboko, na batizio kuwa mahali walipotupwa watoto watumwa ambao hawakuuzwa pamoja na mama zao.
Baada ya kwanza ukoloni wa Kijerumani serikali iliomba makanisa ya Ujerumani kuchukua wajibu badala ya kuwaachia watu wa mataifa wengine.
Walutheri wa kwanza walifika Dar-es-Salaam mwaka 1887.
Mwaka 1888 walifika watawa Wajerumani wa kwanza wa shirika la Mt. Benedikto waliounda baadaye monasteri za Peramiho na Ndanda na kushughulikia uinjilisti kote Kusini.
Mwaka 1891 walifika wamisionari Walutheri (misheni ya Berlin) na Wamoravia kupitia Ziwa Nyasa wakiwa wamepatana kugawa kati yao maeneo ya kazi kama walivyogawana wachungaji wa Ibrahimu na Lutu; walijenga vituo katika Unyakyusa kule Rungwe na Manow.
Ni kwamba Walutheri waliomba Wamoravia kuanza kazi pamoja katika Tanganyika Kusini-Magharibi. Baadaye walichapisha hata kitabu cha pamoja cha nyimbo za Kikristo.
Walutheri wengine yena (misheni ya Leipzig) walianza kule Uchagga kituo cha Moshi.
Wajerumani wengine waliofika mapema walikuwa Waadventista Wasabato.
Kutoka Kenya ilianzishwa kazi ya A.I.M. (Africa Inland Mission) katika mkoa wa Mwanza - chama hicho kiliundwa Marekani kama misheni ya kimadhehebu yenye athari kubwa ya Kibatisti.
Karne ya 20 iliona wamisionari wengi kutoka madhehebu mbalimbali ya Ulaya na Marekani. Baada ya vita vya pili vya dunia Wamarekani walianzisha Kanisa la Kibatisti Kusini-Magharibi mwa Tanzania. Walifika pia wamisionari mbalimbali wa Kipentekoste. Tofauti na nchi za Afrika Kusini na Magharibi, wamisionari wa makanisa ya Wamarekani Weusi hawakuwa na athari kubwa.
Tofauti na Kenya, ambako Kanisa la Kiorthodoksi la Kiafrika (linaloshirikiana na Patriarki wa Kigiriki wa Aleksandria-Misri) ni kubwa, nchini Tanzania halikuenea mapema, isipokuwa wahamiaji Wagiriki walijenga makanisa machache ya Kiorthodoksi kule Dar es Salaam, Iringa, Arusha n.k.
Hasa karne ya 20 imekuwa ya kurudisha umoja. Wakristo wa madhehebu mbalimbali yanashirikiana kirahisi katika shughuli mbalimbali.
Mwaka 1936 viongozi wa madhehebu kama Walutheri, Waanglikana, Wabatisti na Wamoravia waliunda "Baraza la Misheni Tanzania". Baraza hilo lilikuwa mtangulizi wa CCT (Jumuiya ya Kikristo Tanzania / Christian Council of Tanzania).
Katika miaka ya 1960 viongozi wa makanisa ya Kiprotestanti waliongea juu ya kuunda Kanisa la Muungano katika Afrika Mashariki. Kwa bahati mbaya wafadhili wengine kutoka ng'ambo waliona hawawezi kusaidia kanisa la muungano kama si tena la madhehebu yao. Ilionekana hiyo ni hatari kwa kazi kama hospitali na shule zilizotegemea msaada kutoka ng'ambo, hivyo muungano ulisimamishwa.
Lakini madhehebu yaliyoongea hivyo wakati ule yanaendelea kushirikiana katika vyombo vya pamoja kama vile CCT. Wanachama wa CCT ni kama wafuatao: Walutheri, Waanglikana, Wamoravia, African Inland Church, Wabatisti, Wapresbiteri, Jeshi la Wokovu, Kanisa la Uinjilisti (Mbalizi), pia vyama kama TCRS/Huduma ya Kikristo ya wakimbizi Tanzania.
Ushirikiano umejengwa pia kati ya Waprotestanti na Kanisa Katoliki. Zamani za wamisionari uhusiano huo ulikuwa mgumu mara nyingi. Lakini mabadiliko mengi yamejenga msingi wa uelewano na hali ya kuheshimiana.
Hatua muhimu sana ilikuwa mkutano mkuu wa Kanisa Katoliki duniani ulioitwa Mtaguso wa Pili wa Vatikano miaka 1962-1965. Hapo maaskofu wote chini ya uongozi wa Papa (kwanza Papa Yohane XXIII, halafu Papa Paulo VI) walitamka kwamba Wakristo wote ni ndugu na kwamba kujenga umoja wa Kanisa ni wajibu wa kila mmojawao.
Leo hii makanisa ya CCT na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hushirikiana katika shughuli mbalimbali kama vile Baraza la Kikristo la Afya Tanzania (Tanzania Christian Medical Board) au katika kuandaa mafundisho ya pamoja katika elimu ya Kikristo mashuleni.
Chama cha Biblia ni chombo kingine cha ushirikiano wa kimadhehebu. Chama hicho kina kazi ya kutoa Biblia kwa bei nafuu kwa watu wengi. Kinasimamia tafsiri ya Biblia katika Kiswahili cha kisasa na lugha nyingine za kikabila. Kinaandaa matoleo mapya ya Biblia na misaada ya kuielewa kama "Itifaki ya Biblia".

JINSI YA KUMPENDA NA KUMTHAMINI MKEO KWA KUTUMIA BIBLIA

Image may contain: 2 people, people smiling, text and outdoor

Je, unajua mambo yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke?

Waefeso 5:25, 28-29 
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa”

Mume kumpenda mke ni agizo. Agizo hili halibadiliki mke akiwa mkorofi, sio mtii au vyovyote vile. Biblia inamuagiza mume ampende mke kama Kristo alivyolipenda Kanisa. Huu ni upendo mkubwa sana, japokuwa kanisa lilikengeuka mbali naye bado upendo wa Kristo haukubadilika. Kumpenda mwanamke kama mwili wako mwenyewe, kumjali na kumtunza.

Akiwaandikia waume Wakristo kuhusu jinsi wanavyopaswa kuwatendea wake zao, Petro, mwandikaji aliyeongozwa na roho, aliwahimiza waige mtazamo wa Mungu na Yesu Kristo. ‘Enyi waume, endeleeni kuwapa heshima,’ akaandika. (1 Petro 3:7) Kumpa mtu heshima hutoa wazo la kwamba unamthamini na kumheshimu sana. Hivyo, mtu anayemheshimu mke wake hamwaibishi, hamshushii heshima, au kumtendea kwa jeuri. Badala yake, yeye huonyesha kwa maneno na matendo, hadharani na faraghani, kwamba anamthamini na kumpenda.

Tunaweza kupataje picha kamili ya jinsi ambavyo Mungu Mungu huwaona wanawake?

Njia moja ni kwa kuchunguza mtazamo na mwenendo wa Yesu Kristo, kwani yeye ndiye “mfano wa Mungu asiyeonekana,” naye huonyesha kikamili maoni ya Mungu kuhusu mambo mbalimbali. (Wakolosai 1:15) Jinsi ambavyo Yesu aliwatendea wanawake katika siku zake huonyesha kwamba Mungu anawaheshimu wanawake na hawaungi mkono kamwe ukatili dhidi ya wanawake ambao umeenea sana katika nchi nyingi leo.

Wanaume wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha.

Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.

Upweke, kwa hakika, huzaa migogoro isiyokwisha inayowafanya wanaume [ambao kimsingi ndio wasababishi wa upweke huo] washindwe kuwaelewa wanawake. Kwa mtazamo wao, ni vigumu kumridhisha mwanamke. Wengine wanaenda mbali na kufikiri , 'mwanamke ni kiumbe mgumu kueleweka' kwa sababu, ‘hata ufanye nini...hata umpe nini hawezi kuridhika’.
Lakini wanachosahau wanaume wenye mawazo haya ni kuwa mwanamke kwa asili yake anayo mahitaji ya msingi ambayo yanapopuuzwa, chochote kinachofanyika kama mbadala wa mahitaji hayo hakiwezi kuwa na maana yoyote. Usipoweza kujua mahitaji yake halisi, unaweza kumpa chochote kile unachodhani anakihitaji na bado mambo yasiende kama unavyotamani iwe.

Kusema hivyo, haimaanishi sielewi kuwa wapo wanawake wengi wanaopenda kujipatia fedha kwa wanaume. Hawa ni wanawake wanaofanya biashara ya mahusiano. Kwao, hakuna sababu yoyote ya kuwa na uhusiano imara na wenzi wao isipokuwa mpangilio wa kujipatia vitu na fedha.
Hatuzungumzii uhusiano huo wa kibiashara kati ya mwanamume na mwanamke bali uhusiano wa dhati unaojengwa katika misingi ya upendo, uaminifu, kuelewana na ahadi ya kuwa pamoja katika dhiki na raha.
Hebu na tutazame mahitaji makubwa ya kihisia aliyonayo mwanamke mwenye upendo wa dhati kwa mwenzi wake.

JINSI MUNGU ANAVYO WAPENDA WANAWAKE

Masimulizi mbalimbali yanayoonyesha jinsi Mungu alivyotenda kwa niaba ya wanawake yanathibitisha kwamba anawajali waabudu wake wanawake. Mara mbili aliingilia kati ili kumlinda Sara asilalwe kinguvu. (Mwanzo 12:14-20; 20:1-7) Mungu alimpendelea Lea, mke wa Yakobo ambaye hakupendwa sana, kwa ‘kufungua tumbo lake la uzazi,’ naye akazaa mwana. (Mwanzo 29:31, 32) Wazalishaji wawili Waisraeli ambao walimwogopa Mungu walipohatarisha uhai wao ili kuwalinda watoto wa kiume Waebrania wasiuawe huko Misri, Mungu alionyesha uthamini wake kwa ‘kuwapa familia.’ (Kutoka 1:17, 20, 21) Pia alijibu sala ya Hana ambayo alitoa kwa bidii. (1 Samweli 1:10, 20) Na mjane wa nabii fulani alipokabiliwa na mkopeshaji ambaye alitaka kuchukua watoto wake kuwa watumwa ili kulipia deni lake, Mungu hakumwacha. Kwa upendo, Mungu alimwezesha nabii Elisha aongeze mafuta yake ili alipe deni, na bado abaki na mafuta ya kutosha kwa ajili ya familia yake. Hivyo akahifadhi familia yake na heshima yake.—Kutoka 22:22, 23; 2 Wafalme 4:1-7.

Mara nyingi manabii walishutumu zoea la kuwatumia vibaya wanawake au kuwatendea jeuri. Nabii Yeremia aliwaambia hivi Waisraeli katika jina la Mungu: “Toeni haki na uadilifu, nanyi mumkomboe yeye anayenyang’anywa kutoka mkononi mwa mpunjaji; wala msimtendee vibaya mkaaji mgeni yeyote, mvulana asiye na baba au mjane. Msiwatendee jeuri yoyote. Wala msimwage damu yoyote isiyo na hatia mahali hapa.” (Yeremia 22:2, 3) Baadaye, matajiri na wenye mamlaka katika Israeli walishutumiwa kwa sababu ya kuwafukuza wanawake kutoka nyumbani mwao na kuwatendea watoto wao kwa ukatili. (Mika 2:9) Mungu wa haki huona na kushutumu uovu huo ambao wanawake na watoto wao hutendewa.

MPENDE MKEO KWA VITENDO

Kumpenda mke wako zaidi ya kitu chochote iwe ni wazazi, kazi, biashara, watoto n.k. Mume mwema siku zote huthamini nafasi ya mke katika maisha yake na mara zote mke wake ni namba moja kwake.

Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Waefeso 5: 25,28 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake,..vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

Ni rahisi sana kwa mwanamke kuonyesha utii pale anapoonyeshwa upendo. Wanaume wengi huonyesha upendo wakiwa wanachumbia ila wakishaoa tu wanajisahau na kusahau kama mke anahitaji upendo ili aweze kutimiliza majukumu yake kama mke vizuri kwa furaha. Upendo unaanzia kumjali hisia zake, kumtunza kimahitaji na kumtia moyo, kumsifia na kumuonyesha unamthamini.

Tulishaona kuwa hadhi ya mwanaume inategemea kwa kiasi kikubwa namna anavyoheshimiwa. Kwa mwanamke hali ni tofauti. Hadhi yake inategemea namna anavyopendwa na mwenzi wake.

Upendo kwa mwanamke unaeleweka anapoambiwa bila kuchoka na kuthibitishiwa kwa kutendewa vitendo kuwa anapendwa. Katika lugha ya kiingereza, hapa tungetumia neno affection, yaani matendo yanayoonesha mapenzi kwake.

Hata hivyo, lugha ya mapenzi hutegemea mambo mengi. Kuna athari za utamaduni, desturi na imani zilizopo katika jamii aliyokulia mwanamke. Hata hivyo, yapo matendo yaliyothibitika kuvuka mipaka ya kiutamaduni.

Mfano, kumwambia mwanamke unampenda mara nyingi iwezekanavyo, ni hitaji la msingi. Kwa mwanamume, kuambiwa anapendwa inaweza isiwe jambo la maana, lakini si kwa mwanamke. Mwanamke anatamani kusikia mara nyingi kadri inavyowezekana kuwa anapendwa.

Pia kuna vitu kama kupewa zawadi asizotarajia, kutumia muda wa mapumziko pamoja nae, kutoka naye kwenda mbali na nyumbani na mambo kama hayo yanayoonesha kuwa kweli unampenda.

Ndio kusema, ikiwa unataka kuugusa moyo wa mwanamke, akupe heshima unayoihitaji kama mwanaume, unawajibika kujua vitu gani mahususi ukimfanyia vinatuma ujumbe wa wazi kuwa unampenda. Usipoweza kumfanya mwanamke ajisikie kupendwa, anapoteza hamu ya uhusiano. Huchoka kihisia na anaweza kufanya mambo yasiyotarajiwa ili tu kuhujumu mahusiano.

Huruma nyororo ya Yesu kwa watu ilionyeshwa kwa namna alivyoshughulikia wanawake. Katika pindi moja mwanamke fulani aliyekuwa ameteseka kutokana na mtiririko wa damu kwa miaka 12 alijitahidi kumtafuta Yesu kati ya umati. Hali yake ilimfanya asiwe safi kidesturi, kwa hiyo yeye hakupaswa awe huko. (Mambo ya Walawi 15:25-27) Lakini alikuwa amehitaji msaada sana hivi kwamba akaenda nyuma ya Yesu kimya-kimya.

JINSI YESU ALIVYO WATENDEA WEMA WANAWAKE

Mwanamke huyo alipogusa vazi la Yesu, yeye aliponywa mara moja! Hata ingawa Yesu alikuwa njiani kwenda katika nyumba ya Yairo, ambaye binti yake alikuwa mgonjwa mahututi, Yesu alitua. Akiwa amehisi nguvu ikimtoka, yeye alitazama huku na huku ili amwone yule aliyekuwa amemgusa. Hatimaye, yule mwanamke akaja na kuanguka mbele yake akitetemeka. Je, Yesu angemkemea kwa ajili ya kuwa kati ya huo umati au kwa ajili ya kugusa vazi lake bila ruhusa yake? Kinyume cha hilo, mwanamke huyo alimwona Yesu kuwa mchangamfu na mwenye fadhili sana. “Binti,” yeye akasema, “imani yako imekuponya.” Huo ulikuwa wakati pekee ambao Yesu alimwita mwanamke “binti” moja kwa moja. Ni lazima neno hilo liwe lilistarehesha moyo wa mwanamke huyo kama nini!—Mathayo 9:18-22; Marko 5:21-34.

Yesu aliona zaidi kupita yale ambayo Sheria ilisema. Yeye aliona maana yayo hasa na uhitaji wa rehema na huruma. (Linganisha Mathayo 23:23.) Yesu aliona hali ya kuhitaji msaada sana ya mwanamke huyo mgonjwa akafahamu kwamba yeye alikuwa amechochewa na imani. Kwa njia hiyo yeye aliwawekea kielelezo kizuri wanaume Wakristo, hasa waangalizi. Ikiwa dada Mkristo anakabili matatizo ya kibinafsi au hali ngumu au yenye kujaribu sana, wazee wa kutaniko wapaswa kujaribu kuona zaidi ya maneno na matendo ya sasa hivi na kufahamu hali na madhumuni. Ufahamu huo wenye kina huenda ukaonyesha kwamba subira, uelewevu, na huruma vinahitajiwa badala ya shauri na usahihisho.—Mithali 10:19; 16:23; 19:11.

Yesu alipinga mapokeo ya kirabi naye alistahi heshima ya wanawake si kwa matendo yake pekee bali pia kwa mafundisho yake. Kwa kielelezo, fikiria yale aliyofundisha juu ya talaka na uzinzi.

Kuhusu talaka, Yesu aliulizwa swali hili: “Je! ni halali mtu kumwacha [“kutaliki,”] mkewe kwa kila sababu?” Kulingana na simulizi la Marko, Yesu alisema hivi: “Yeyote yule atalikiye mke wake [isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati] na kuoa mwingine afanya uzinzi dhidi ya mke, na ikitukia wakati wowote mwanamke, baada ya kutaliki mume wake, aolewa na mwingine, yeye afanya uzinzi.” (Marko 10:10-12, NW; Mathayo 19:3, 9) Maneno hayo yenye kusemwa kwa usahili yalionyesha staha kwa heshima ya wanawake. Jinsi gani?

MKE WAKO NI KIPAUMBELE CHAKO

Wajibu wa kuonyesha heshima si kwa waume peke yao. Ingawa mume apaswa kumheshimu mke wake kwa kumtendea kwa upendo na kwa heshima, mke apaswa kumheshimu mume wake kwa kuwa mwenye kujitiisha na kuonyesha staha nyingi. (1 Petro 3:1-6) Zaidi ya hayo, Paulo aliwaonya Wakristo kwa upole, ‘waonyeshane heshima.’ (Warumi 12:10) Huo ni wito kwa wanaume na wanawake kutanikoni kutumikia pamoja kwa kustahiana.

Mwanamke hapendi kujikuta katika mazingira ya kushindania nafasi ya kwanza na kitu kingine chochote iwe ni kazi, mtu au chochote kile unachokipenda wewe mwanamume.

Tulishaona kuwa kwa mwanaume, hadhi yake hutegemea zaidi namna uwezo wake unavyotambuliwa. Hali hiyo humfanya mwanamume atumie muda mwingi kufanya mambo yanaweza kumpa heshima katika jamii. Inaweza kuwa kazi, biashara, mamlaka na namna zozote zile zinazomwongezea uwezo.

Lakini wakati anapotumia muda mwingi katika mambo hayo, ni rahisi kuonekana ameyafanya mambo mengine kuwa ya muhimu kuliko uhusiano wake na mwenzi wake. Wanawake wengi hawapendi kujikuta katika hali hii. Hapa ndiko iliko tofauti.

Mwanamke hatamani kuwa kwenye nafasi ya ‘mengineyo’, ‘ziada’, ‘baadae’ ‘nikipata muda’. Unapomweka 'akiba' mwanamke hawezi kufurahia kwa sababu anatamani awe kipaumbele chako.

Waefeso 5:23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe; kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

Mambo mengi huthibitisha kuwa umempa nafasi ya kwanza. Mfano kuwa na muda wa kuwa naye mara nyingi kadri inavyowezekana, kuahirisha mambo mengine ya muhimu kwa ajili yake, kuwahi miadi unapoahidi kukutana nae, kuwasiliana naye kwa karibu na mambo kama hayo. Unaposhindwa kufanya hivyo, mwanamke hupata ujumbe kuwa yeye ni mtu wa ziada baada ya mambo ya muhimu.
Kadhalika, ili kumwambia yeye ni kipaumbele, mwanamke anatamani kila unapoongea nae akili yako yote iko pamoja naye. Kuwa pamoja naye maana yake ni kuachana na vyote vinavyokuondolea uzingativu na kumsikiliza kwa makini.

Mwanamke anatamani unapozungumza naye ufuatilie anachokisema, umpe mrejesho kuwa unamwelewa na uonesha kuwa mwili, akili, hisia ziko pamoja naye kumsikiliza. Vinginevyo, mwanamke anakuoana kama hujaweza kumpa nafasi yake anayoistahili.

Tangu wanadamu wafanye dhambi na kupoteza ukamilifu, wanawake katika utamaduni mbalimbali wamevunjiwa heshima. Wametendewa vibaya kimwili, kiakili, na kingono. Lakini Mungu hakukusudia watendewe kwa njia hiyo. Biblia inaonyesha wazi kwamba haidhuru maoni ya kidesturi ambayo yanashikiliwa na watu wengi, wanawake wote wanapaswa kutendewa kwa staha na heshima. Ni haki yao kutoka kwa Mungu.

Mume anapoonyesha kumsikikiza na kujali ushauri wa mkewe na kushauriana naye kabla hajafanya jambo lolote mke anaona anapendwa sana na yeye atazidisha upendo na heshima kwa mumewe. Mpende mkeo ili aweze kukuheshimu kwa furaha na sio kwa kujilazimisha. Kumpenda mke ni kujipenda mwenyewe. Mara moja moja mtoe out bila watoto na umueleze unavyompenda, zawadi sio lazima siku ya sherehe au kitu kikubwa, hata chocolate(unanunua kwa ajili yake na sio watoto), mke atahisi kupendwa sana.

1Petro 3:7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

Saturday, January 19, 2019

HIVI UNAJUA MJI WA NINAWI UPO IRAKI?

Image may contain: people standing, sky, mountain, outdoor and nature
Ninawi (kwa Kiakadi: Ninwe; kwa Kiashuru: ܢܸܢܘܵܐ; kwa Kiebrania נינוה , Nīnewē; kwa Kigiriki Νινευη, Nineuē; kwa Kiarabu: نينوى, Naīnuwa) ulikuwa mji mkuu wa Waashuru upande wa mashariki wa mto Tigri.
Magofu yake yako ng'ambo wa mto huo ukitokea Mosul (Iraki).
Katika Biblia ni maarufu hasa kutokana na habari zinazopatikana katika kitabu cha Yona na zilizotumiwa na Yesu kuhimiza toba.
Mji huu ulikuwa mkubwa kuliko yote duniani kwa miaka hamsini hadi mwaka 612 KK uliposhindwa na Wababuloni.
Kitabu katika Agano la Kale ambacho kinaelezea juu ya tukio moja katika maisha ya Yona. Yona yawezekana hakuandika kitabu hiki yeye mwenyewe. Wazo kuu la kitabu cha Yona ni kwamba Yehova anatawala kila mahali na upande wake hauzuiliwi katika taifa moja au watu fulani tu.
Katika mlango wa 1, Bwana anamwita Yona kwenda kuhubiri Ninawi. Badala ya kufanya kama Bwana alivyomwamuru, Yona alitoroka kwa mashua na akamezwa na samaki mkubwa. Katika Mlango wa 2, Yona alisali kwa Bwana, na yule samaki akamtapika Yona nje kwenye ardhi kavu. Mlango wa 3 unaandikwa kuwa Yona alikwenda Ninawi na akatoa unabii wa kuanguka kwa mji huo. Hata hivyo, watu wale wakatubu. Katika Mlango wa 4, Bwana anamkanya Yona kwa kukasirika kwa vile Bwana aliwaokoa wale watu.
Katika Agano la Kale, ni mji mkuu wa Ashuru na kwa zaidi ya miaka mia mbili ulikuwa mji maarufu wa kibiashara katika kingo ya mashariki ya mto Tigri. Ulianguka wakati wa kushuka kwa ufalme wa Ashuru, 606 K.K.
Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliishi Ninawi, 2 Wafalme 19:36.
Yona alitumwa kuhubiri toba kwa mji ule, Yon. 1:1–2 (Yona 3:1–4).
Watu wa Ninawi walitubu, Yona 3:5–10.
Kristo aliitumia Ninawi kama mfano wa toba mbele ya Wayahudi, Mathayo 12:41.
Kwa jiji la Ninawi, lilitambuliwa tena katika karne ya 19 baada ya miaka zaidi ya 2,500 ya mashaka. Sasa inaaminika kuwa ndiyo jiji kubwa zaidi duniani lilikuwa wakati wa mauti yake (tazama Tertius Chandler ya Miaka Elfu Nne ya Ukuaji wa Mjini: Sensa ya kihistoria). Kulingana na Mheshimiwa Austen Henry Layard, ambaye aliandika juu ya utambuaji tena wa Ninawi katika fasihi yake Ugunduzi Huko Ninawi, mzingo wa Ninawi Kuu ilikuwa "safari ya siku tatu kamili", kama ilivyoandikwa katika Yona 3:3 (Austen Henry Layard. Akaunti Maarugu ya Ugunduzi Huko Ninawi, J.C. Derby: New York, 1854, uk. 314). Kabla ya ugunduzi wake, wenye kushuku walidharau kwa uwezekano kwamba jiji kubwa sana lingeweza kuwepo katika ulimwengu wa kale. Kwa kweli, wenye kushuku walikanusha uwepo wa Ninawi kabisa. Ugunduzi wake katikati ya miaka ya 1800 ulionyesha kuwa ni uthibitisho wa ajabu kwa Biblia, ambayo inataja Ninawi kwa jina mara 18 na kutoa vitabu vyote viwili (Yona na Nahumu) kwa hatima yake.
Shalom,


Tuesday, January 15, 2019

MBINGUNI, PEPONI, KUZIMU NA JEHANNAM NI WAPI?

Image may contain: text
Mpendwa mmoja aliniuliza maswali yafuatayo ambayo nimeona ni muhimu niyajibu kama Makala fupi kwa ajili hata ya faida ya watu wengine wenye maswali kama haya:
Swali la 1: Hivi watu wakifa, roho zao zinakuwa wapi hasa?
Swali la 2: Roho hizo zinakuwa katika hali gani hasa?
WATU WAKIFA, ROHO ZAO ZINAKUWA WAPI?
Biblia inasema kuhusu Bwana Yesu kuwa:
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; (Wafilipi 2:9-10).
Kulingana na mstari huu, tunagundua kuwa kuna sehemu kuu tatu:
Mbinguni
Duniani
Chini ya nchi
Mbinguni ni mahali aliko Mungu; duniani ni mahali tuliko sisi wanadamu tulio hai; na chini ya nchi ni mahali aliko ibilisi.
Tangu nyakati za Adamu kulikuwapo wanadamu wema na waovu. Wanadamu wema walikufa na waovu nao walikufa. Swali ni kuwa, je, walipokufa walienda wapi?
Mwinjilisti Luka anatupatia picha nzuri kutokana na kisa alichosimulia Bwana Yesu juu ya tajiri na Lazaro. Tunasoma katika Luke 16:22-26:
22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.
23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
Tunachoona hapani kuwa Lazaro alikuwa ni mwenye haki kama Ibrahimu na tajiri alikuwa ni asiye na haki. Hawa walikaa sehemu mbili tofauti, maana zilitenganishwa na bonde. Sehemu hizi zote mbili zilikuwa chini ya nchi.
Kabla ya Yesu kufa, wanadamu wote walipokufa walienda chini ya nchi. Na huko kulikuwa na sehemu mbili – kwa shetani na kifuani mwa Ibrahimu. Katika habari hii ya tajiri na Lazaro – ambayo ilitokea zamani sana hata kabla ya Musa, Bwana Yesu anatuonyesha kuwa tajiri alikuwa kwenye mateso; na Lazaro alikuwa penye raha.
Lakini mtu anaweza kusema hivi, “Huoni kuwa tajiri aliinua macho yake? Je, hii si ishara kuwa Lazaro na Ibrahimu walikuwa mbinguni?
Wakati huo mbingu zilikuwa hazijafunguliwa kwa ajili ya wanadamu. Tuendelee kusoma na hapo mbele tutapata jibu la maswali hayo.
Bwana alipokuja duniani, akateswa na akauawa, tunaambiwa kuwa:
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri. (1Petro 3:18-19)
Mbinguni hakuna vifungo; vifungo viko chini ya nchi. Kwa hiyo, Bwana alienda kuwahubiria waliokuwa kifungoni.
Bila shaka hii ndiyo sehemu ambayo Wakatoliki huita toharani. Sehemu hii ilikuwapo zamani kama makao ya muda kwa wale waliokufa kabla ya Kristo. Humo waliwekwa kungojea ukombozi wa mwanadamu ufanye na Kristo. Lakini sasa hivi haipo tena.
Maana ya andiko hili katika Petro ni kuwa, wale waliokuwa kifuani mwa Ibrahimu (au tuseme toharani), Bwana alienda akawahubiria katika zile siku tatu alipokuwa katika tumbo la nchi.
Je, baada ya kuwahubiria, nini kilifuata?
Imeandikwa:
Hivyo husema, alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? (Efe 4:8)
Shetani alikuwa amewashikilia wanadamu wote kuzimu, lakini Bwana akaenda akawateka na kuondoka ndao. Na ndiyo maana kabla Bwana hajafa, alisema:
Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. (Mathayo 12:29)
Na ushahidi wa jambo hili uko wazi kwa sababu Biblia inatuambia kwamba baada ya Bwana kufa, watakatifu waliokuwa wamekufa zamani walionekana Yerusalemu.
Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi. (Mat 27:50-53)
Je, alipoteka mateka aliwapeleka wapi?
Imeandikwa kuhusu yule mwizi aliyesulubiwa pamoja na Bwana:
Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja namipeponi. (Luka 23:42-43)
Ukisoma kwenye Kiingereza, imeandikwa hivi: And Jesus said unto him, Verily I say unto thee, To day shalt thou be with me in paradise. Peponi ndio paradiso.
Paradiso si Yerusalemu Mpya. Paradiso ni makao ya muda kwa ajili ya watakatifu, kusubiria mwisho wa mambo yote ambapo Yerusalemu mpya itafunguliwa na kuwa makao ya milele pamoja na Bwana.
Kama ambavyo watakatifu wako kwenye makao ya muda paradiso, ndivyo ambavyo na wenye dhambi wako kwenye makao ya muda kuzimu aliko shetani sasa – maana shetani hayuko jehanamu bado. Yaani, wako kule alikokuwa yule tajiri aliyezungumza na Ibrahimu kuhusiana na Lazaro kutumwa duniani.
Pia tunasoma kuwa:
Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu. (2Petro 2:4)
Hawa mashetani wako kifungoni lakini kumbe wala hiyo si hukumu bado. Ndiyo maana anasema wako pale hata ije hukumu. Itakapofika sasa mwisho wa mambo yote, ndipo kila mtu ataenda sasa kwenye makao ya milele.
Biblia inasema kuhusu wakati huo:
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; (Mat 25:34)
Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; (Mat 25:41).
Kumbe moto wa milele ndiyo hukumu ya mwisho iliyotajwa hapo juu.
Hata tukisoma kwenye Ufunuo imeandikwa: Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. (Ufu 21:8)
Kwa nini inaitwa mauti ya pili? Ni kwa sababu japo tajiri yuko kwenye mateso na hayuko duniani tena (yaani alishakufa); japo wale malaika walio kifungoni wako kwenye mateso sasa; lakini iko mauti nyingine tofauti nay a sasa. Kitendo cha kutupwa kwenye ziwa la moto (jehanamu) na kubaki humo milele ndicho kinachoitwa mauti ya pili.
Hata roho hii ya mauti inayotutoa duniani sasa pamoja na kuzimu aliko shetani sasa navyo vitaingia jehanamu kwenye mauti ya pili:
Imeandikwa: Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. (Ufu 20:14)
JE, ROHO ZILIZOONDOKA DUNIANI ZINAKUWA KATIKA HALI GANI?
Hawa ni watu kamili kama tulivyo sisi. Sisi kama roho tumo ndani ya mwili wa nyama, lakini ukivua mwili huu (yaani, ukifa) unavikwa mwili wa kiroho; na unaendelea kuishi kama kawaida.
Biblia inasema: Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. (1Kor 15:40)
Tofauti ni majukumu tu. Huku tunafanya kazi, tunasafiri, n.k. Lakini kule wenye dhambi wanateswa na watakatifu wanamfurahia Yesu, kwa mfano kwa kusifu.
TOFAUTI YA KUZIMU NA JEHANAMU NI NINI?
Mfano ili uweze kuelewa ni huu: Hapa duniani mshukiwa wa kosa la jinai la mauaji akikamatwa huwekwa rumande na polisi (lock-up); ili kusubiri kupelekwa mahakamani kusikilizwa kesi yake na kuhukumiwa kwenda kutumikia jela kama akithibitishwa ya kuwa ana hatia. Hivyo
(1) KUZIMU NI RUMANDE YA KIROHO YA WATENDA DHAMBI AMBAKO HUPELEKWA BAADA YA KUFA WAKISUBIRI SIKU ILE YA MWISHO YA HUKUMU YA MWISHO.(Tofauti na rumande ya duniani ni kwamba ukiingia kuzimu wewe moja kwa moja ni wa motoni! wenzetu Wakatoliki wanamafundisho yanayotaka kufanana na hapa-wanaita-TOHORANI (PAGATORY)-Katika biblia hakuna sehemu inayoitwa tohorani!
(2) JEHANAMU (MOTONI) NI JELA YA KIROHO YA WATENDA DHAMBI AMBAKO HUPELEKWA BAADA YA KUHUKUMIWA HATIA ZAO SIKU ILE YA HUKUMU YA MWISHO. ( Na kwa kuwa Mungu hukihukumu kila chenye dhambi, viyo hivyo na MAUTI NA KUZIMU AMBAO DHAMBI ZOTE ZITAKUWA KWAO SIKU ILE YA MWISHO - MAUTI NA KUZIMU NAO WATATUPWA JEHANAMU!) Hebu tuone Neno la Mungu lisemavyo kuhusu maelezo haya katika kitabu cha UFUNUO WA YOHANA-Mlango wa 20; Ambao unasema maneno haya:-
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu;
3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
NINATUMAINI UMEPATA JIBU. MUNGU AKUBARIKI!
HITIMISHO
Kuzimu ni mahali aliko shetani sasa hivi pamoja na wanadamu wote wanaokufa katika dhambi. Haya ndiyo makao makuu ya uovu wote unaoendelea duniani leo. Baada ya mambo yote, yaani mwisho wa nyakati, kuzimu na kila kilichomo ndani yake vitatupwa kwenye ziwa la moto wa milele.
Wanadamu wanaokufa ndani ya Yesu wako paradise sasa hivi. Baada ya mwisho wa mambo yote, wataingia Yerusalemu mpya na kuishi pamoja na Bwana milele na milele.
Usipange kukosa kuingia Yerusalemu Mpya!

Monday, January 14, 2019

ALLAH NA MUHAMMAD WASEMA KUWA JUA LINAZAMA KWENYE TOPE

Related image
1. Je, ni kweli kuwa Allah aliumba kila kitu?
2. Je, kuna ushahidi wowote ule wa kisayansi kuwa Jua linazama kwenye tope?
3. Je, Muhammad ni kweli aliliona Jua likizama kwenye tope?
Ndugu msomaji,
Huu ni Msiba kwa Waislam wote wanao sema kuwa Allah aliumba kila kitu na Muhammad ni Mtume wake.
Zul-Qarnain na Kutua kwa Jua katika Sura 18:85-86
Je, ni kweli kuwa jua linazama katika chemichemi za maji zenye tope au giza, au Koran ina makosa, au kuna maelezo mengine? Kwanza tutaangalia maana ya wazi Sura ya 18:85-86, na kisha tutaangalia maelezo na majibu ya baadhi ya Waislam kuhusu jambo hili.
UNAJIMU KIDOGO
Inawezekana kuwa haijulikani kwa mapana kwamba watawala wa kislam wa Abbasid, Waarabu na Waajemi waliendelea sana katika unajimu, wakizipa majina nyota nyingi, hata walinukuru na kusahihisha baadhi ya orodha za hesabu za watawala wa Misri (Ptolemy’s tables). Hata hivyo jua ni kubwa mara nyingi zaidi ya dunia nzima, na dunia husafiri ikilizunguka jua. Jua halizami katika chemichemi za maji zenye tope.
Zul-Qarnain ni Nani?
Hatuna ushahidi kama Muhammad alimwambia mtu yeyote kuwa Zul-Qarnain alikuwa nani hasa. Waislam wana mitazamo minne tofauti.
Alexander Mkuu (wa Makedoni) ni mtazamo wa Waislam wengi zaidi. Zul-Qarnain humaanisha kuwa ni "mtu mwenye pembe mbili." Kuna hadithi ya kubuniwa isemayo kuwa Alexander Mkuu alikuwa mungu na alikuwa na pembe mbili za kondoo dume zilizokuwa zinakua pembeni mwa kichwa chake. Licha ya ukweli kwamba hii haikuwa kweli (na ni tatizo kupata kofia ya vita—helimeti inayoweza kutosha), hadithi hii ilijulikana, na waislam wengi hudhani kuwa Allah katika sura ya 18 Alexander alitajwa kwa jina hili, mungu.
Koreshi I Muajemi ni mtizamo mwingine. Ufalme wake hasa ulikuwa ufalme uliohusisha makundi mawili: Wamedi na Waajemi, lakini zaidi ya hayo hakuna uthibitisho kuwa pembe mbili zinamhusu yeye.
Mfalme wa Yemeni ambaye alivaa kofia ya vita yenye pembe mbili za kondoo dume, ni mtazamo walionao baadhi ya Waislam.
Mtu asiyejulikana ni mtizamo wa nne. Hata hivyo inaonekana si vema sana kutoa maelezo juu ya watu ambao msemaji hajawahi kuyasikia.
Hitimisho: Haijalishi kuwa Zul-Qarnain alikuwa nani hasa. Kama aligundua kuwa jua hutua kwenye chemichemi za maji zenye tope, na huwa halizami kwenye chemichemi za maji zenye tope, kwa hiyo huu ni ubatili, bila kujali mtu ambaye Muhammad alimzungumzia.
Sura 18 Mawazo na Majibu

Wazo la I: Jua huzama kwenye chemichemi za maji zenye tope!
Kwa Waislam wa awali, Koran iliwafundisha kuwa jambo hili linatokea hasa. Mwanahistoria wa kiislamu wa awali al-Tabari juzuu ya 1 uk.234 anaonesha hili. Kama mfano wa pili, "[Dhu al-Qarnaiyn] alishuhudia kuzama kwa jua katika sehemu yake ya kupumzika ndani ya bwawa jeusi na tope la kunuka." Kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 5 uk.173-174. Dul Qarnain [Zul Qarnain] anapatikana pia kwenye al-Tabari juzuu ya 1 uk.371.
Jambo jingine linaloingiliana na hili, dunia hukaa juu ya samaki mkubwa kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 1 uk.220 (839-923 K.K.).
Wazo la 2: Jua lilionekana kwa Alexander likitua katika ziwa la Ithaca Makedonia
Wazo hili hubashiri kuwa Zul-Qarnain alikuwa Alexander, na kwamba Alexander alikuwa Muislam mzuri. Wazo hili haliendani na ukweli kwamba Alexander alikuwa na hekalu lililotengenezwa kwa ajili yake. Pia Alexander alikwenda kuteka kaskazini na magharibi mwa Ithaca ambayo ni Albania ya sasa.
Kibaya zaidi katika wazo hili, Wayunani walifanya makazi mamia ya maili magharibi mwa Ithaca ambayo ni Hispania, Sicily, n.k. za asa, miaka mia tano kabla ya Alexander. Kitu gani kingemfanya Myunani mwenye akili sana afikiri kuwa jua lilizama katika ziwa la Makedonia wakati meli za kiyunani zilikuwa zinaenda mbali zaidi magharibi mwa nchi ya Alexander? Kwa nyongeza, Tertullian katika Hoja Juu ya Nafsi [A Treatise on the Soul] sura 49 uk.227 anasema kwamba Aristotle, aliyeishi wakati ule ule, anataja shujaa kutoka kisiwa cha Sardinia mbali magharibi mwa Makedoni lakini ni kama kwenye latitudi ile ile.
Wazo la 3: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni Bahari ya Atlantic
Bahari ya Atlantic haina tope na si nyeusi, bali ni bluu-kijani. Pia si chemichemi bali ni bahari. Jua huwa halizami katika bahari. Cha muhimu zaidi, Alexander, Koreshi I wa Uajemi na wafalme wa Yemeni hawakuwahi kwenda kwenye Bahari ya Atlantic na Sura ya 18:85-86 inasema kuwa Zul Qarnain aliona au alishuhudia hili.
Sababu yoyote kati ya hizi nne inatosha kulindoa wazo hili, hivyo basi kwa Waislam wanapendekeze hili? Hiki ndicho kiwango ambacho wanajaribu kwenda ili kuonyesha kuwa Sura ya 18:1-2 sio potofu. Ikiwa Allah [Mungu] wa uislam alikuwa na wazo hili katika Koran, na Allah alijua kuwa hili ni wazo potofu, hivyo jambo hili litakuwa uongo. Kama Allah wa uislam hakujua ukweli huu, wasingelikuwa na ufahamu na hakika wasingekuwa na uwezo wa kujua kila kitu. Kama mistari hii isingetoka kwa Allah [Mungu] wa uislam, basi Koran ingekuwa na makosa dhahiri, kwa sababu inathibitisha upotofu huu kutoka kwa Allah wakati sivyo hivyo. Bila shaka, ikiwa kweli si Allah wa uislam, na Mungu wa kweli si mwandikishi wa Koran, basi Allah wa uislamu hakusema uongo kwa sababu hayupo.
Wazo la 4: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni Koreshi I alikoangalia Bahari Nyeusi (Black Sea)
Hata kama Koreshi I alikwenda magharibi mwa ufuko wa mashariki mwa Bahari Nyeusi (Black Sea), na jua lingeonekana vipi likitua katika Bahari Nyeusi, ikiwa alikuwa ameshaupita ufuko wa mashariki kuelekea kusini na mashariki? Hatuna ushahidi kuwa Koreshi aliwahi kusafiri kwenda ukanda unaojumuisha Georgia, Amernia, Azerbaijan, n.k. za sasa, zilizo mashariki mwa Bahari Nyeusi. Muislam angekuwa na hoja yenye udhaifu kidogo kama angesema kuwa Koreshi aliliona jua likichomoza kutoka kwenye Bahari Nyeusi, kwa sababu alivuka hadi Uyunani, lakini Koran inaongelea kuzama kwa jua. Hata hivyo Bahari Nyeusi sio chemichemi, kila mtu kuanzia wamisri na wengineo kaskazini ya mbali, walijua kuwa jua halikuzama kwenye Bahari Nyeusi.
Wazo la 5: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni Koreshi I alikoangalia Bahari ya Aegean
Lakini Waajemi walikuwa wakiwafahamu vema Waatene, Waspartani, (asili ya Wayunani), na Wayunani wengine. Waajemi wangelijua kuwa Wayunani hawakuwa upande mwingine wa jua.
Wazo la 6: Hakika "Chemichemi ya maji yenye tope" ni mfalme wa alikoangalia Bahari Nyekundu
Wayemeni (Wasaba/Waseba) wakati wote waliwafahamu Waabisinia (Waethiopia) ng’ambo ya mto. Ikiwa walifikiri kuwa jua lilizama katika Bahari Nyekundu (Red Sea) basi Waabisinia wangelikuwa watu waliokuwa upande mwingine jua lilikokuwa.
Wazo la 7: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni usemi wa kufananisha na kitu kingine
Ikiwa kitu hiki hakikuwa halisi, bali ni kifananishi cha kitu au vitu vingine, basi Koran imeshindwa kuelezea kuwa hakikuwa kweli, na wazo hili lilikuwa la kupotosha. Zaidi ya yote, hakuna mtu anayeweza kusema kwa hakika kuwa kitu hiki kilifananishwa ni nini hasa.
Hakuna kitu chochote kwenye Koran kinachoonyesha kuwa kitu hiki si halisi, na Waislam wengi wa awali walikichukulia kuwa kitu halisi, yaani ukweli halisi. Kwa kuzingatia kuwa walijua maana hasa ya jambo hili kutoka kwa wafuasi wa Muhammad, kwa hiyo walipotoshwa na Sura ya 18.
Wazo la 8: Muhammad alikuwa akisimulia juu ya ndoto yake
Wazo hili halimfahamu Zul-Qarnain kuwa ni nani hasa. Ikiwa Muhammad alikuwa anasimulia juu ya ndoto yake, jua lingeweza kutua popote alipotaka litue. Hata kama haifahamiki ni muhusika gani dhahania aonaye kitu kilicho potofu kabisa, na watu wanaoamini kuwa ni kitu cha kweli, atatufundishaje sisi juu ya kuiamini kweli.
Hata hivyo, ikiwa mtu atasema kuwa walimwona mtu fulani aitwaye ‘Ali akifanya kitu cha ajabu ajabu, na mamilioni ya watu wakamwamini kwa karne nyingi. Je, mtu huyo ataweza kuwa mwongo ikiwa alisahau kuwaambia watu kwamba, "ilikuwa ndoto yangu tu na sikumwona Ali akifanya hivyo kwa macho yangu."?
HITIMISHAO
Bila kujali kama Zul-Qarnain alikuwa Alexander Mkuu au mtu mwingine, Korani yaeleza jambo hili kama ukweli kuwa jua huzama katika chemichemi za maji yenye tope. Hata watu wa zamani miaka 1,000 kabla ya Muhammad walijua kuwa jua halikuzama upande huu wa Hispania. Wazo hili halikuwa kifananishi cha kitu kingine kwa sababu hakuna Muislam wa zamani aliyepatikana kuwa hakulichukua jambo hili kuwa halisi au kutoa maana yake kama usemi wa kufananisha na kitu kingine, na Waislam wote wa zamani waliamini kuwa Koran haikutolewa kwa ajili ya kudanganya.
Orodha ya Vitabu vya Tafsiri ya Korani
1. Arberry, Arthur J. The Koran Interpreted. Macmillian Publishing Co., Inc. 1955.
2. Dawood, N.J. The Koran. Penguin Books. 1956-1999.
3. Malik, Farooq-i-Azam. English Translation of the Meaning of AL-QUR’AN : The
Guidance for Mankind. The Institute of Islamic Knowledge. 1997
4. Pickthall, Mohammed Marmaduke. The Meaning of the Glorious Koran. Dar al-
Islamiyya (Kuwait) (no date given)
5. Rodwell, J.M. The Koran. First Edition. Ivy Books, Published by Ballantine
Books. 1993.
6. Shakir, M.H. The Qur’an. Tahrike Tarsile Qur’an, Inc. 12th U.S. Edition 2001.
7. Sher Ali, Maulawi. The Holy Qur’an. Islam International Publications Limited
(Ahmadiyya) 1997
8. Yusuf ‘Ali, Abdullah. The Holy Qur-an : English translation of the meanings
and Commentary. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (Al Madina
Saudi Arabia) 1410 A.D.
Vitabu Vingine vya Rejea
Encyclopaedia Britannica. Encyclopaedia Britannica, Inc. 1958.
The History of al-Tabari : An Annotated Translation. Ehsan Yar-Shater, General Editor. State University of New York Press 1989-.

Saturday, January 12, 2019

UTAFUTENI UFALME WA MUNGU NA HAYO YOTE MTAONGEZEWA

Image may contain: 3 people, people sitting, hat, beard and outdoor
Ufalme wa Mungu (au Ufalme wa mbinguni unavyoitwa hasa katika Injili ya Mathayo) ni mojawapo kati ya mada kuu za ujumbe wa Yesu Kristo katika Injili . Neno "ufalme" (kwa Kigiriki βασιλεία, Basileia) linapatikana mara 162 katika Agano Jipya, kawaida kwa maana ya Basileia tou Theou (βασιλεία τοῦ θεοῦ), Ufalme wa Mungu, au Basileia tōn Ouranōn, (Βασιλεία τῶν Ουρανῶν), Ufalme wa Mbinguni.
Kwa uwazi, ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu wa milele, Mwenye nguvu juu ya ulimwengu wote. Vifungu vingi vya Maandiko vinaonyesha bila kupinga kuwa Mungu ndiye Mfalme wa viumbe vyote: "Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote" (Zaburi 103: 19). Na, kama Mfalme Nebukadineza alivyosema, "Ufalme wake ni ufalme wa milele" (Danieli 4: 3). Kila mamlaka iliyopo imeanzishwa na Mungu (Warumi 13: 1). Kwa hiyo, kwa maana moja, ufalme wa Mungu unahusisha kila kitu ambacho kilichoko.
"Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa" ( Mathayo 6:33)
Kutokana na maneno haya ya Yesu Kristo, tunapata msingi wa tatu ambao ukiuelewa na ukautumia, unaweza ukawa na uchumi mzuri sana! Msingi huo ni huu:
Tafuta kwanza ufalme wa Mbinguni na haki yake, na hayo yote unayoyatafuta katika uchumi utapewa na kuzidishiwa."
Ukisoma Mathayo 6:24-34 utaona ya kuwa Yesu alipokuwa anasema "na hayo yote mtazidishiwa" alikuwa na maana ya mavazi, vyakula na mahali pa kulala. Kwa tafsiri iliyo laini na nyepesi ya Mathayo 6:24-34,Yesu Kristo alitaka watu wake tujue ya kuwa. Mfumo wetu wa maisha na matokeo ya kuishi kwetu, kunaonyesha ya kuwa kuna kitu ambacho mioyo yetu inakitafuta.
Luka 12: 28 Basi, ikiwa Mungu huvika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatawatendea ninyi zaidi, enyi wa imani haba?
29 Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msifanye wasiwasi,
30 kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
31 Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.
32 Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.
33 Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu.
34 Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu.
= NA HAKI YAKE MAANA YAKE NINI? =
Haki ni tunda la utawala wa Mungu katika moyo. Zaburi 119:172, “Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, maana maagizo yako yote ni ya haki.”
Yesu hatuambii tu kutafuta haki, bali haki Yake. Haki yo yote tuliojitengenezea haina uthamani wowote.
• Isaya 64:6, “Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa kama upepo uondoavyo.
• Rumi 10:3, “Kwa maana wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.”
Haki Yake ni ya nguo safi yote na haita haribika. Filipo 3:8-10, “Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi kwa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili
nipate Kristo; tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; ili nimjue yeye na uweza, wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake.”
Paulo alisema kuwa haki ya Agano La Kale ili kuwa ni kuwekwa pembeni. Imani uja kwa kusikia neno la Mungu.
Je ulishawahi kujiuliza kwamba kwa nini Yesu alibatizwa?
Mathayo 3:13-17, “Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili ambatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akakubali. Naye Yesu alipotokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini, na tazama mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama sauti
kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaye pendezwa naye.”
Hivyo, tunapaswa mkuruhusu Mungu awe na mamlaka juu yetu; atawale pasipopingamizi.
“UTAFUTENI KWANZA MAANA YAKE NINI?”
“Kwanza” inamaanisha kwamba kuna vitu vingine ambavyo tunavitafuta, lakini vinapaswa kutothaminishwa (shushwa kiwango).
“Kwanza” inamaanisha kwamba kuna mengine.
Hatupaswi kuutafuta ufalme wa Mungu kwa kukataa majukumu yetu ya dunia; hataivyo, hatuwezi kuruhusu majuku haya ya kidunia kuingilia majukumu ya mbinguni.
Bwana wetu haitaji kwamba tuwe bila mawazo kuhusu vitu vya maisha haya.
1 Timotheo 5:8, “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”
Roho ambayo haijali na kuwajibika huondolewa katika roho wa kweli wa Ukristo. Rumi 12:11, “Kwa bidii si walegevu, mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;”
Mkristo wa kweli anachukia uchafu kama anavyochukia ulevi, na kukimbia mambo ya kipuuzi kama anavyo kimbia kutoka katika zinaa.
Bali tunapaswa kuweka vitu vya kwanza nambari moja , na
tusiruhusu kazi ya Mungu katika maisha yetu yatingwe na mambo ambayo hayana umuhimu.
Hatuwezi kuruhusu kazi zetu, masomo ya chuo, michezo, burudani, au kitu chochote kile kije kati yetu na huduma yetu kwa Mungu. Lazima tumuweke awe wa kwanza katika kila jambo tunalofanya.
Ujuzi wangu wa kuomba kazi katika shamba la Real Estate.
Niliombwa kufanya kazi siku ya juma pili. Niliambiwa, “Hufai katika kazi hii”. Nikajibu, “Hapana hii kazi sio ya kwangu.”
Ujuzi wangu wa kuomba kazi katika Kiwanda Cha Ndege.
Niliwaambia nilikuwa napenda kufanya kazi siku yo yote ya wiki na muda wo wote katika siku, isipokuwa niliitaji kuwa kanisani jumapili asubuhi. Tulikubaliana katika hili na barua ya makubaliano iliwekwa katika faili langu kwamba sitahitajika kazini siku za juma pili asubuhi.
Walijaribu hili mara moja tu. Nikawakumbusha makubaliano yetu, na wakanigeuka wakitaka nifanye kazi jumapili moja asubuhi. Nimefanya kazi masaa mengine yote ya siku isipokuwa siku ya jumapili asubuhi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

NINAWEZAJE KUWA MWANA WA MUNGU?

Image may contain: text
1 Yohana 5:11-12 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
Mkutadha huu watwambia ya kwamba Mungu ametupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe, Yesu Kristo. Katika maneno mengine, njia ya kuumiliki uzima wa milele ni kumkubali Mwana wa Mungu. Swahili ni, mtu anawezaje kuwa na Mwana wa Mungu?
Isaya 59:2 Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso Wake msiuone, hata hataki kusikia maombi yenu.
Warumi 5:8 Bali Mungu aonyesha pendo Lake Yeye Mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Kulingana na Warumi 5:8, Mungu alionyesha pendo Lake kwetu sisi kwa njia ya mauti ya Mwanawe. Kwa nini ilimpasa Kristo kutufia? Kwa sababu Andiko la tangaza watu wote kuwa wafanya dhambi. Kufanya "dhambi" kuna maanisha kukosa alama. Biblia inatangaza "wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu (utakatifu mkamilifu) wa Mungu" (Warumi 3:23). Katika maneno mengine, dhambi zetu zatufarikisha sisi na Mungu wetu aliye utakatifu mkamilifu (haki na kweli) na kwa hivyo sharti Mungu awahukumu watenda dhambi.
Habakuki 1:13a Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, Wewe usiyeweza kutazama ukaidi; mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya?
Tito 3:5-7 alituokoa; si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema Yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7 ili tukihesabiwa haki kwa neema Yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Mpokee Yesu leo na ufanyike kuwa Mwana wa Mungu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA

Image may contain: text
Tangu mapema kabisa Mungu wetu anatufundisha kwamba, mbingu na nchi za sasa zitachakaa na kuharibika, na kama mavazi, Mungu atazibadilisha
Zaburi 102:25 Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako. 26 Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu Naam, hizi zitachakaa kama nguo; Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika.
Nchi ya sasa yaani dunia hii au ulimwengu, umechosha na kuchakaa mno Baaya ya kukaliwa na mamilioni ya wenye dhambi wanaofanya machukizo mbele za Mungu. Dunia hii imechakazwa kwa gharika wakati wa Nuhu na vita vya kila namna mpaka vita ile ya mwisho “GOGU NA MAGOGU”.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena.
Watu wengi wako na dhana potovu juu ya mbinguni itakuwa kama nini. Ufunuo mlango wa 21-22 yatupa kiupana picha kamili ya mbingu mpya na nchi mpya. Baada ya matukio ya nyakati za mwisho, mbingu ya sasa na nchi ya sasa zitatolewa na zibadilishwe na mbingu mpya na nchi mpya. Mahali pa kukaa milele pa Wakristo patakuwa katika nchi mpya. Nchi mpya ni “mbinguni” mahali ambapo tutakaa milele yote. Ni katika nchi mpya Yerusalemu mpya, mji mkuu wa mbinguni utakuwa. Utakuwa katika nchi mpya ambapo milango yake na njia zake zitakuwa sha dhahabu
Mbingu- na nchi mpya- ni mahali panapoonekana, ambapo tutaishi na miili ya utukufu (1 Wakorintho 15:35-58). Hoja kwamba mbinguni itakuwa katika “mawingu” ni jambo lisilo la kibibilia. Dhana kuwa tutakuwa “roho zinazo elea mbinguni” pia sio la kibibilia. Mbingu ambayo watakatifu wataiona itakuwa sayari mpya na kamilifu ambapo tutaishi. Nchi mpya haitakuwa na dhambi, uovu, magonjwa, mateso na kifo. Itakuwa sawa na nchi hii ya sasa, au pengine nchi iumbwe upya lakini isiwe na laana yoyote au dhambi.
MBINGU MPYA
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.'' ( Ufunuo 21:1-4 )
Ni muhimu kukumbuka kwamba wazo la kale, “mbinguni” ilimaanisha mawinguni ya juu kabisa ambapo Mungu anakaa. Kwa hivyo wakati Ufunuo 21:1 yazungumzia mbingu mpya, kuna uwezekano kuwa inamaanisha kuwa sayari mpya itaumbwa- nchi mpya, mawingu mapya, na sayari ya juu kabisa mpya. Inaonekana kana kwamba mbingu ya Mungu itaumbwa upya pia, kukipa kila kitu ulimwenguni “mwanzo mpya,” hata kama ni mwili au kiroho. Je! Tutapata ruhusa ya kuingia mbingu mpya milele yote? Labda, lakini tutangoja tuone. Tafadhali wote tuliruhusu neno la Mungu lichonge uelefu wetu wa mbinguni.
Tazama atayafanya yote kuwa mapya ( Isaya 66:22; Isaya 65:17; 2 Petro 3:13; Ufunuo 21:1-7 ). Mbingu hizi na nchi mpya zitakuwa ni nzuri mno, hakuna mfano wake uliowahi kuwako au utakaokuwako. Ufundi wote wa uumbaji wa Mungu utaishia hapa. Hapa ni mahali watakapoishi wateule wake Mungu milele na milele. Wala walio ndani ya Kristo Yesu ni viumbe vipya na hivyo wanastahili kukaa katika MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

Sunday, January 6, 2019

LA IILAHA 'IILAA YASUE ALMASIH

Image may contain: text

LA IILAHA 'IILAA YASUE ALMASIH 

Kama wewe ni Muislam na umesoma "LA IILAHA 'IILAA YASUE ALMASIH" basi teyari wewe umesha MKANA ALLAH NA MUHAMMAD WAKE. Wewe sasa ni Mkristo na sio Mfuasi wa Allah.

Karibu sana kwenye Ukristo kwenye upendo na amani na uhakikisho wa uzima wa milele kupitia Yesu Kristo.

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

Saturday, January 5, 2019

AMINI KWA KURATARAJIA YASIYOWEZA KUTARAJIWA

Image may contain: sky, cloud, nature and outdoor
Katika maisha ya kawaida mwanadamu yeyote anataka awe na usalama wa maisha, kwa mfano awe na nyumba nzuri na mali za kutosha na labda biasha kubwa inayo muingizia kipato kizuri; Lakini, matakwa haya ya binadamu si mara zote yanakuwa kama tupendavyo na wakati mwingini maisha yanaweza kuwa magumu kiasi cha kujiuliza, hivi Mwenyezi Mungu yupo wapi?

Mambo yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.” (Luka 18:27)

Yesu anatuambia katika Luka 18 aya ya 27 kwamba, yote yasiyo wezekana kwa Mwanadamu, yanawezakana kwa Mungu. Je, ni jambo gani basi tufanye ili tuweze kupokea baraka za Mungu?

Hebu tumsome Abraham na tujifunze yeye alifanya nini mpaka akawa na Isaka ambaye alimpata uzeeni.

Warumi 4: 18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
22 Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.

Abraham aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa. Aliamini ahadi ya Mungu na hakusita kwa kuto kuamini ingawa alikuwa umri karibia miaka mia moja na Mkewe Sara alikuwa amekufa kizazi.

Mwanzo 18: 9 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.
10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
12 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?

Abrahamu aliamini yote yalio semwa na Bwana kwa hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi. Warumi 4:21.

Neno la Mungu linasema katika Isaya 55: 11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Hakika Neno la Mungu litokalo kwenye kichwa chake halitarudi bure, bali litatimiza mapenzi yake na ndio maana Abraham aliamini kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyo ahidi.

Je, ni ahadi gani ulipewa na Mungu na bado unasubiri mpaka hii leo? Je, bado unaamini kuwa Mungu kamwe Neno lake haliwezi kurudi bure bali litakamilisha na kutimiza mapenzi yake?


Basi anza kuamini Neno la Mungu kama jinsi Baba yetu Abrahamu alivyo amini. Mambo yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu.” (Luka 18:27)

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW