Tuesday, August 13, 2013

JE, KUNATOFAUTI KATI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO?

Katika nyakati hizi za mwisho kumekuwa na roho nyingi zidanganyazo binadamu. Roho hizi za mpinga Kristo zinawadanganya wengi na kuwafanya wengi wajione kana kwamba wako na Mungu, kumbe Mungu hayupo kati yao na/au ndani ya maisha yao.

Katika soma hili, tutajifunza tofauti iliyopo kati ya Kupunga Pepo na Kutoa Pepo kwa ushaidi wa aya takatifu za Biblia.
( TIMOTHEO 4:1 ).
“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.
(2 TIMOTHEO 4:3-5 )
“Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”.
(2 WATHESALONIKE 2:7-12 )
Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.
Katika nyakati hizi tunaweza kuona jinsi watu wanavyofanyiwa maombezi kwa kuangushwa chini na hatimaye kusimama bila kupokea muujiza wa uponyaji. Utaweza kuona watu wamejazana madhabahuni wakigaagaa chini na baadaye husimama na kuondoka lakini wakati mwingine huchukua muda mrefu kwao kusimama na kuondoka. Jambo la kushangaza ni siku zote kuonekana watu haohao , mapepo yao hayatoki. Miujiza hii imeenea kote duniani, uatakuta watu wanapiga kelele lakini pepo hawawatoki watu hao. Miujiza ya kimungu huondoa pepo kabisa ndani ya mtu tena kwa mamlaka na kumwacha akiwa mzima. Watu hawa hawafanyi miujiza ya uponyaji bali wanapunga pepo. Ni muhimu kujua kuwa  hata wapagani wanaweza kupunga pepo na kuwafanya wapige kelele. Waganga wa kienyeji wanaweza kupunga pepo lakini hawawezi kuwatoa. Tunawaona wapunga pepo wakitaka kutoa pepo lakini wanashindwa  ( MATENDO 19:13-16 ). Watu hawa walikuwa wa kawaida lakini leo tungewaita walokole kwa kuwa walikuwa watu wa dini.
Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani  yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani  iwe dhahiri kwa mfano  wetu tunavyofanya  katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane  au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.
Kazi tuliyoitiwa  ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha  pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?
Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza  kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa  leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW