Mwanzo yaweza oneekana ya kwamba ikiwa Mungu aliumba vitu vyite, kwa hivyo hata uovu uliumbwa na Mungu. Ingawaje uovu siyo “kitu” kama mwamba au umeme. Huwezi kuwa na ghala la uovu. Ouvu hauwezi kujitegemea; ni kutokuwa na uzuri halisi. Kwa mfano, shimo ni kitu wazi, lakini linaweza kuwa kitu kingine. Tunaita ukesefu wa ugumu shimo, lakini haiwezi tenganishwa na ugumu. Kwa hivyo wakati Mungu aliumba, ni kweli kwamba vyote alivyo viumba vilikiwa vizuri. Kati ya kitu kizuri Mungu aliumba, vilikuwa viumbe vyenye uhuru wa kuchagua lililo jema. Ili tuwe na chaguo halisi, Mungu aliweza kuruhusu kuwepo na jambo kando ya jambo jema ili kuwepo na chaguo. Kwa hivyo Mungu aliruhusu hawa malaika huru na wanadamu kuchagua jema ama kukataa lililo jema (uovu). Wakati uhusiano upo kati ya vitu viwili vizuri, huwa tunasema kwamba huo ni uovu, lakini hiyo haiwezi kuwa “kitu” kilicho mlazimisha Mungu kukiumba.
Hata elezo zaidi litazaidia. Ikiwa mtu ameulizwa, “Je baridi huwepo?” pengine jibu litakuwa “ndio” ingawa hii huenda isiwe kweli. Baridi haiwepo, bali huja kunapokosekana joto. Vile vile, giza haliwepo; ni kutokuwa na mwangaza. Kwa hivyo uovu ni kutokuwa na wema, ama uzuri, uovu ni kukosekana na uwepo wa Mungu. Haikumlazimu Mungu kuumba uovu, lakini kuhurusu uovu kwa kukosa kwa wema.
Mungu hakuumba uovu, lakini uruhusu uovu uwepo. Kama Mungu hangeruhusu nafasi ya uovu, wote mwanadamu na malaika wengemtumikia Mungu kwa lazima, bali si kwa kuchagua. Mungu hakutaka “miigizo” kwa ufupi yenye ingefanya chenye aliwataka wafanye kwa sababu ya “ratiba” yao. Mungu aliruhusu jukumu la uovu ili tuwe na nia njema ya kweli na kuchagua ikiwa ama hatukutaka kumtumikia.