Saturday, February 19, 2022

LAWEZA NENO JEMA KUTOKA NAZARETHI ?



(CAN ANYTHING GOOD COME OUT OF NAZARETH?)

Nazareth
ANDIKO LA MSINGI: Yohana 1:43-46. Biblia inasema hivi
“43. Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate. 44. Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 45. Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 46. Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.”
Ni muhimu kufahamu kuwa Nazareth ulikuwa ni mji mdogo uliokuwa kusini mwa jimbo la Galilaya (Lower Galilee), Mji huu ulikuwa ni moja ya miji iliyodharauliwa sana, kwa ujumla Israel ilikuwa na majimbo makuu Matatu, Yuda, Samaria na Galilaya, Yuda ndio eneo ambalo liliheshimika sana hususani kwa kuwa lilikuwa ni eneo lililotoa manabii na viongozi wakubwa na walioonyesha utii na uwezo wa kumuamini na kumtegemea Mungu, maeneo yaliyofuata kama Galilaya na Samaria hayakuwa maeneo yaliyopewa heshima wala kipaumbele kutokana na historia zake za kuongoza katika ibada za Sanamu, watu wasioshika dini viongozi waovu na wasiomcha Mungu, hivyo Galilaya ilidharaulika na kuonekana kama miji isiyoweza kutoa neno Jema.
Aidha kwa habari ya Kumtazamia masihi ni wazi pia ilijulikana kuwa Masihi angekuja kutokea Uyahudi yaani Yuda katika mji wa Daudi Bethelehemu kwa vile nabii Mika alitabiri hivyo Mika 5:2 Biblia inasema “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.” Marabi na wataalamu wote wa Maandiko na wajuzi na wanasheria wa kiyahudi wote walikuwa wanatambua wazi unabii huu na kukubali kuwa Masihi angetokea Bethelehemu Mathayo 2:1-6 Biblia inasema hivi:- “1. Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2. Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5. Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii, 6. Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.”
Unaweza kuona ni kwa sababu na msisitizo mkuu ilikuwa ngumu kwa Mwanafunzi kama Nathaeli kuamini kuwa Yeye aliyetabiriwa na Musa na manabii kama angeweza kutokea Nazareth
Kwa ujumla Nazareth ulikuwa ni mji usioheshimika na uliongoza kwa umasikini na mmomonyoko mkubwa wa uadilifu, watu wasiomcha Mungu waabudu sanamu na kimji hiki hakikuwahi kabisa kutajwa katika unabii wa agano la kale, mtu aliyetokea Nazareth alionekana sawa tu na mtu aliyetokea Mbagala, au Gongo la Mboto au manzese tofauti na Ostabey au sinza ni sawa na mtu akikuambia unatokea Kwatango, au kilosa au mbulizaga kule Pangani, au kwa msisi huko Handeni, au Nchebebwa huko Newala au Naluleo huko Liwale, Nazareth na Galilaya ilidharaulika ilikuwa mtu akikuita wewe ni mgalilaya au Mnazareth ilikuwa ni Lugha ya dharau ya hali ya juu Yohana 7: 40-42, 52. Biblia inaonyesha jinzi ambavyo maadui wa Yesu Kristo pia waliutumia mji huu.
Mathayo anajaribu kuonyesha kuwa uko unabii, ulioashiria kuwa Yesu ataitwa Mnazareth Mathayo 2:19-23 unabii huu kwa undani, unabii huu unatokana na Mathayo kuunganisha Isaya 11: 1 ambao kuna neno shina na Chipukizi neno hili kwa kiebrania husomeka kama “NETSER” kwa Kiingereza Shoot au Root yaani shina hili ndio asili ya Jina Nazareth.
Ni muhimu kufahamu kuwa katika somo hili tunajifunza kuwa Mungu huweza kuinua mtu kutoka katika Hali ya kudharaulika, ingawa kijiji cha Nazareth kilidharaulika lakini kilipoungwa na jina la Yesu kilipata umaarufu mkubwa sana, Yesu mwenyewe alikubali kuitwa Yesu wa Nazareth, Majini na Mapepo yakitajiwa Yesu wa Nazareth yanalia kwa nguvu mitume walipoombea waginjwa na kufanya miujiza mara kwa mara walilitumia jina la Yesu Kristo wa Nazareth hivyo Nazareth leo umekuwa ni mji maarufu
Awaye yote bila kujali umetokea ukoo gani, kabila gani, dini gani, jamii gani ukiunganishwa na Yesu Kristo historia yako inabadilishwa hata kama ulikuwa mnyonge kiasi gani utakuzwa na utatiwa nguvu na utatumiwa na Mungu kwa namna ya kipekee Nazareth leo ikitajwa kila mtu anajua ni moja ya miji ambayo Bwana Yesu alilelewa na kukulia.
Mungu alitaka Jina hili dhaifu na lililodharauliwa liunganishwa na jina la Mwanae Mpendwa na kufuta Historia mbaya ya Jimbo la Galilaya, Filipo alimwambia Nathanael njoo uone, Mtu akiunga na Yesu hwi wa kawaida Maisha yake yanabadilishwa na Historia yake inakuwa mbaya na adui zako wataisoma Namba.
Na Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima!
Rev. Innocent Kamote.

YESU NI ALFA NA OMEGA

 

ALFA NA OMEGA.
“Alfa” ni herufi ya kwanza katika alfabeti za lugha ya kiyunani kama ilivyo “A” katika alfabeti za Kiswahili na Vivyo hivyo “Omega” ni herufi ya mwisho katika alfabeti za kiyunani kama ilivyo “Z” katika alfabeti za Kiswahili. Yesu Kristo anaposema hivyo anamaanisha kwa undani sana kwamba hata herufi zote za Alfabeti zinamzungumza yeye katika lugha yoyote duniani na siyo kiyunani pekee Yesu ni Mwanzo na mwisho wa alfabeti zote zote humtaja yeye na kumtukuza hii pia humaanisha ya kuwa yeye ni yote katika yote.

YESU NI A.
Yesu kristo anaitwa A yaani ni Afya yetu Zaburi 42;5.11, 43;5 Yeye ni Afya yetu na Mungu wetu tunapokuwa na upungufu wowote katika Afya zetu yeye3 alikuja ili sisis tuwe na uzima tena tuwe nao tele Yohana 10;10 Yeye pia ni Ahadi ya uzima 2Timotheo 1;1 mganga yeyote akikuhaidi uzima ahadi hiyo inaweza isiwe na uhakika lakini ahadi za Yesu ni ndiyo yaani ni hakika 2Wakoritho 1;19-20 Hesabu 23;19. Anaitwa pia Aliye juu Zaburi 46;4 wengine wako chini Yeye yu juu ya yote Yeye pia ni Aliyeko,Aliyekuwako na Atakayekuja Ufunuo 1;8,Yeye pia ni Amani ya Bwana. Zaburi 129;8 Yeye ni Amina Ufunuo 3;14. Anaitwa Arabuni ya roho zetu Efeso 1;14 yaani ni muhuri au uhakika.

YESU NI B.
Yesu huitwa Bwana wa mabwana Ufunuo 19;16 na pia huitwa Bwana mkubwa Luka 8;24 Huitwa pia Baraka ya Bwana Kumbukumbu 33;23 ni Bwana wa vita Yoshua 10;14 kutoka 15;3 ni Bwana harusi wa kanisa Mathayo 9;15

YESU NI C.
Ni chakula cha uzima Yohana 6;35 vyakula vingine hutupa uzima wa muda tu chakula hiki hutupa uzima wa milele yeye ni Chanda cha Mungu Kutoka 8;19 huitwa chapa ya nafsi ya Mungu Waebrania 1;13 na ni chemichemi ya maji ya uzima Yeremia 2;13 pia huitwa Chipukizi la haki Zekaria 6;12

YESU NI D.
Yesu Kristo ni dhabihu yetu Waefeso 5;2 alitolewa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu na kwa kupigwa kwake sisi tunmepona Isaya 53;5 hatuna haja tena ya kutoa kafara nyingine kama mbuzi kuku, na kuwapelekea waganga wa kienyeji

YESU NI E.
Yesu pia huitwa Elimu ya utukufu wa Mungu angalia katika 2Koritho 4;6 hakuna aliye na Elimu yenye utukufu kama Kristo wanadamu wenye madigrii kibao wana sehemu ndogo sana ya maarifa ukilinganisha na Kristo mwenye maarifa yote, ikumbukwe kuwa maarifa yote yanatoka kwake.

YESU NI F.
Yesu anapotajwa kama F katika Maandiko yeye ni Fadhili za Mungu Zaburi 57;3 tukikosa fadhili kwa wanadamu tumwendee Yesu yeye ni mfadhili wa ajabu atatupa mahitaji yetu yote Bure bila ya masharti.Huitwa pia Fahari ya Yakobo Zaburi 47;4 Yeye ni fahari yetu hatupaswi kumuonea aibu yeye pia ni Faraja Yetu au faraja ya Israel Luka 2;25,Ni fimbo ya Mungu Kutoka 4;20 na ni furaha ya bwana Nehemia 8;10

YESU NI G.
Yesu Kristo huitwa Gumegume Isaya 50;7 Gumegume ni aina Fulani ya jiwe ambalo ni gumu sana kwa kiingereza huitwa Flint mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika na yeyote ambaye litamwangukia jiwe hili litamsagasaga tikitiki Mathayo 21;44 Chochote kilichokigumu magonjwa mikosi balaa tuvilete kwa Yesu vitapondwapondwa kabisa

YESU NI H.
Yesu Kristo anatajwa pia kuwa ni Haki ya Mungu 2Koritho 5;21 hakuna mtu yeyote atakayehesabiwa haki mbele za Mungu isipokuwa katika Yesu Kristo aliye haki ya Mungu Warumi 3;26,5;1 Yeye pia ni Hakimu Zaburi 50;6 ndiye atakaye uhukumu ulimwengu Kristo pia ni Hekima yetu kwani huitwa Hekima ya Mungu 1Koritho 1;30iwapo tunalo hitaji la Hekima leo

YESU NI I.
Yesu huitwa pia Immanuel Mathayo 1;23 yaani ni Mungu pamoja nasi anatajwa pia kuwa ni Ishara Yesu ni udhihirisho wa uwezo wa Mungu mahali alipo kuna ishara Isaya 11;10

YESU NI J.
Jina la Yesu ni Jina lipitalo majina yote Wafilipi 2;9 si hilo tu Yesu ni Jiwe kuu la pembeni Matendo 4;11 Jiwe lililo hai 1Petro 2;24. Uimara wetu unatokana na jiwe kuu la msingi la pembeni na lililo hai yaani Yesu Kristo bila yeye hakuna uimara wowote

YESU NI K.
Yesu anaitwza kichwa cha kanisa Waefeso 5;23 yaani ndiye kiongozi mkuu wa kanisa lote,huitwa pia kiongozi mkuu wa wokovu wetu Waebrania2;10. Katika Waebrania 7;17;10;21 Ni Kuhani mkuu maana yake ndiye mpatanishi wetu mkuu 1Timotheo 2;5 yeye pia huitwa kweli Yohana 14;6 pia ni Kimbilio letu

YESU NI L.
Yesu Kristo ni Lulu moja ya thamani kubwa Mathayo 13;46 tukimpata katika maisha yetu tumepata lulu moja ya thamani kubwa yeye ndiye wa kumshika na sio dini Ufunuo 3;11 Dini au dhehebu Fulani sio lulu moja ya thamani

YESU NI M.
Ni Mfalme wa Wafalme Ufunuo 19;16 yapasa tumuogope na kumtii na kumuheshimu Ni Mfinyanzi wetu Isaya 64;8,Yeremia 18;1-6. Huitwa Mchungaji mkuu wa kondoo Waebrania 13;20 ni Mchungaji mwema Yohana 10;14. Ni Mlango wa kondoo Yohana 10;7 ni Moto ulao Waebrania 12;29, ni Mungu mkuu Tito 2;13 ni Mwana wa Mungu Yohana 9;35-37 ni Mwana wa Adamu Mathayo 26;64 Ni Mwokozi Tito 1;4,Mwalimu Yohana 3;2,na Muhukumu wetu siku ya mwisho Yohana 5;22

YESU NI N.
Yeye ndiye Nabii yule Yohana 6;14 huitwa pia Njia pekee ya kuingia mbinguni Yohana 14;6 ndiye Nyota ya kung’aa asubuhi Ufunuo 22;16 au Nuru ya ulimwengu Yohana 8;14 akiwa ndani yetu hatuta kwenda gizani kamwe yeye ni Neno Yohana 1;1

YESO NI O.
Yeye hutajwa kama Ondoleo la dhambi zetu Matendo 10;43 tukimuamini hutupa ondoleo la dhambi

YESU NI P.
Pendo la Mungu Warumi 5;5 ni chimbuko la upendo la kweli

YESU NI R.
Ni Rafiki Luka 12;4.pia ni mwalimu mkuu sana anayeheshimika Rabi au Rabon Yohana 20;16

YESU NI S.
Yeshu huitwa Shahidi aliye mwaminifu Ufunuo 1;5 ni Simba wa kabila la Yuda Ufunuo 5;5

YESU NI T.
Tabibu mkuu Mathayo 9;11-12,Yeye ni Tumaini letu kuu Zaburi 71;5 ni Taraja letu Zaburi 71;5 ni Tegemeo letu Yeremia 17;5-8.

YESU NI U.
Yesu Kristo ni uzima wa milele Yohana 14;6 na ukombozi wetu 1Timotheo 2;6 na ndiye upanga wa utukufu Kumbukumbu 33;29 upanga huu unaweza kushughulikia na yeyote anaye kutesa

YESU NI V.
Yesu ni Vazi jipya Luka 5;36 Torati ni vazi kuu kuu lakini Kristo ni vazi jipya

YESU NI W.
Ni Wokovu wetu Zaburi 27;1 tukiwa na Yesu hatupaswi kumuogopa mtu awaye yote Hesabu 23;23 hata wachawi hatupaswi kuwaogopa kwani Yesu ni wokovu wetu

YESU NI Y.
Huitwa Yesu Mathayo 1;21 yeye ndiye aokoanye watu wake na dhambi zao bila Yesu hakuna wokovu.Yeye ni Yeye yule jana leo na hata milele,ni Yeye ajaye wala hatakawia Ebrania 10;37.

YESU NI Z.
Yesu ndiye Zeri ya Gileadi Yeremia 46;11 nyakati za Biblia kulikuwa na dawa iliyoitwa zeri ambayo ilikuwa ikipatikana huko Gileadi dawa zote zikishindwa ndipo ilibidi itumike zeri ya Gileadi ilikuwa ni dawa isiyoshindwa ni zaidi ya muarobaini Zeri ni Yesu Kristo dawa isiyoshindwa kila kitu kinaposhindikana ndipo tumuitie Yesu yeye hashindwi kitu.

Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekim





Saturday, February 5, 2022

QUR'AN 15:15 ALLAH NA MUHAMMAD WAMEROGWA








Uthibitisho huu hapa unasema kuwa Mwenyezi Mungu au Mitume wake hawawezi kurogwa, lakini Allah na Mtume wake Muhammad wamerogwa. HUU NI MSIBA MKUBWA SANA
Quran inathibitisha kuwa Muhammad alirogwa kiasi cha kuto fahamu aya zipi zilitoka kwa Allah na zipi ni za Shetani kutoka Surah ya Kwanza mpaka ya Mia na Kumi na Nne.
Uthibitisho upo katika Kitabu cha Abdullah Saleh Al Farsy Ukurasa wa 977 Chapa ya Nane pamoja na Sahih hadith za Al Bukhari namba Juma Ally Mayunga
KWANZA ALLAH ALIDANGANYA KUWA MUHAMMAD HATAROGWA LAKINI MUHAMMAD ALIROGWA VIBAYA NA ALIATHIRIKA NA NGUVU ZA UCHAWI MPAKA KUFA KWAKE LAKINI PIA NAYE ALLAH KAKIRI KUWA ALIROGWA:
REJEA HII AYA
✔Quran 15:42(Allah akasema ) Hakika waja wangu, wewe shetani hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.
➖➖➖➖😛
LAKINI TUKIJA HAPA TUNAONA ALLAH WA WAISLAMU NAYE ALIROGWA AKIWA NA WENZAKE WAKINA SISI
MUNGU WA KWELI HAWEZI KUROGWA LAKINI ALLAH ALIROGWA PAMOJA NA WENZAKE WAKINA SISI
✔️Qur'an 15:15. Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
MASWALI YAJIBIWE KWA AYA ZA QUR-AN NA HADITHI
✔ 1: JE ALLAH ALIKUWA WAPI MUHAMMAD ALIPOROGWA MPAKA AKAWA ANAITA OVYO OVYO NA AKAWA ANAONA YUPO KIFUANI KWA MWANAMKE KUMBE ANAJIFANYA TENDO LA NDOA PEKEE YAKE MPAKA ANATOA MBENGU ZA KIUME BILA MKE ?
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
✔ 2: QURAN INASURA 114 SWALI KATIKA HIZO SURA AYA NGAPI ZATOKA KWA ALLAH NA AYA NGAPI ZATOKA WA WACHAWI WA MAKKA NA MADINA?
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
✔ 3: AYA IPI INATHIBITISHA KUWA MUHAMMAD JIBRIL ALIPOENDA KWA MUHAMMAD KUMPA WAHYI ALIMKUTA UCHAWI UMESHAONDOKA ILI APOKEE HUO UFUNUO ?
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
USHAHIDI HUU HAPA KUWA. MUHAMMAD SWT ALIROGWA NA ALIATHIRIKA NA UCHAWI MPAKA KUFA KWAKE USHAHIDI HUU HAPA WA QURAN PAMOJA NA HADITHI QUR'AN TAFASIRI YA ABDULLAH SALEH AL-FARSY UKRASA 977 CHAPA YA NANE UNAFAFANUA JINSI MUHAMMAD SWT ALIVYOATHIRIKA NA KUROGWA .
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
JIBRIL WENU ANATHIBITISHA KUWA MUHAMMAD ALIROGWA USHAHIDI HUU HAPA
✔Quran 17:47 “ Tunajua sana, sababu wanayosikiliza, na wanaponong’ona, wanaposema hao madhalimu. Nyinyi hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa”
✔ Quran 25:8. Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa na bustani ale katika hiyo? Wakasema madhaalimu: Nyinyi hamumfuati ila mtu aliye rogwa.
✔️Qur'an 26:153
153. Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa
185. Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
Ufafanuzi wa aya hizo juu zinasema TAFASIRI YA ABDULLAH SALEH AL-FARSY CHAPA YA NANE UKRASA 977 MUHAMMAD ALIROGWA AKATHIRIWA NA UCHAWI :
ATHARI YA KUROGWA KWA UCHAWI WA NGUVU NA MADHARA YA UCHAWI JUU YA MUHAMMAD SWT KATIKA MAISHA YAKE MPAKA KIFO
Jibril (a.s) alikuja na kumpa maelekezo Mtume (s.a.w) ya kusoma sura mbili hizi. Watafiti wengi zamani na wa sasa wamelifanyia upinzani jambo hilo, kwamba ikiwa hadithi zitakubaliwa, basi mfumo wote wa sharia utakuwa ni wa kutiliwa shaka, kwa sababu kama mtume (s.a.w) aliweza kuathirika kwa uchawi, na kwa mujibu wa hadithi hizi kweli uchawi huo ulionesha athari yake, basi hatuwezi kukaidi au kukana hadi kiwango gani maadui waliweza kumfanya Mtume (s.a.w) aseme na atende mambo kwa nguvu ya uchawi, na katika mafundisho yake mambo mangapi yatoka kwa Allah na mangapi yatokana na athari ya uchawi juu yake.
Si hiyo tu, bali pia wasema kuwa baada ya kuyatambua hayo kuwa ni kweli katu haitawezekana hata kule kukaidi kuwa (s.a.w) alishawishiwa kudai utume kwa mauzauza ya kinjozi kuwa alimjia malaika. Pia wanasema hadithi hizi zapingana na Qur’an, na kama ilivyo katika Qur’an kuwa tuhuma hiyo batili kwa makafiri ilivyotajwa kuwa mtume s.a.w amerogwa naye ameathirika na uchawi:
Wanaposema hao madhalimu, ‘Ninyi hamumfuati isipokuwa mtu aliyerogwa’.” (17:47), lakini hadithi hizi zinathibitisha madai ya makafiri kuwa kwa kweli aliathirika na kuongozwa na uchawi Kadri historia inavyohusika,ukweli kuwa kiasi fulani cha athari ya uchawi juu ya Mtume (s.a.w) ni hakika iliyothibiti; na kama kwa ustadi wa ubishi inawezekana kuthibitisha kuwa kweli.
Limesimuliwa jambo hilo na Bukhari, Muslim, Nasai, Ibn Majah, Ahmad, ‘Abdur Razzaq, Humaid, Baihaqi, Tabarani, Ibn Sa’d, Ibn Marduyah, Ibn Abi Shaibah, Hakim, Abd bin Humaid na Muhadithina wengine toka kwa Bi. ‘Aisha (r.a), Zaid bin Arqam, Ibn ‘Abbas kupitia silsila nyingi mno kiasi kwamba jambo lenyewe limefikia hali ya ufululizo kamili, isipokuwa kila Hadithi, yenyewe ni ripoti kamili.
Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha kuwa utume wa Muhammad una utata. Ikiwa na wao Waislamu kwa mujibu wa hadithi hizi hawajui ni mambo mangapi Muhammad aliyoyasema yanatoka kwa Allah na mangapi aliyasema akiwa ameshinikizwa na wachawi , Je ufunuo na utume wake utakuwa umetoka kwa Mungu wa Kweli? Tafakari !!
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
REJEA TENA HAPA NABII WA MUNGU HAWEZI KULOGWA ILA MUHAMMAD ALIROGWA AKAWA ANAITA OVYO NA AKAWA ANAONA ANAFANYA MAPENZI KUMBE ANAJIFANYA YEYE BILA KUWA NA MKEWE 😂😂
MUHAMMAD ALIROGWA USHAHIDI HUU HAPA HADITH YA SAHIH AL-BUKHARI 5765
Imesimuliwa na Aisha kuwa.
"Uchawi ulifanywa juu ya Mjumbe wa Allah (so) hivi kwamba alifikiri alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wake zake ilhali hakuwa na hivyo (Sufyan alisema: Huo ni uchawi mgumu zaidi kwani una athari kama hiyo). Ndipo siku moja akasema, "Ewe Aisha unajua kwamba Allah amenielekeza juu ya jambo ambalo nilimuuliza? Wanaume wawili walinijia na mmoja wao alikaa karibu na kichwa changu na mwingine alikaa karibu na miguu yangu.
Yule aliye karibu na kichwa changu alimuuliza yule mwingine. Ana shida gani huyu mtu? ' Mwisho akajibu yuko chini ya athari ya uchawi yule wa kwanza aliuliza, Nani amemfanyia uchawi? Mwingine alijibu Labid bin Al-A'sam, mtu kutoka Bani Zuraiq ambaye alikuwa mshirika wa Wayahudi na alikuwa mnafiki. ' Wa kwanza aliuliza, Alitumia nyenzo gani)? ' Mwingine akajibu, 'sega na nywele imeshikamana nayo.' Wa kwanza akauliza, "Yuko wapi?" Mwingine akajibu
Katika ngozi ya chavua ya mtende wa kiume iliyowekwa chini ya jiwe kwenye kisima cha Dharwan '' Kwa hivyo Mtume (ﷺ) alikwenda kwenye kisima kile na kutoa vitu hivyo na akasema "Hicho ndicho kisima nilichoonyeshwa (katika ndoto) Maji yake yalionekana kama kuingizwa kwa majani ya Henna na mitende yake ya mitende ilionekana kama vichwa vya mashetani. " Mtume (ﷺ) akaongeza, "Kisha kitu hicho kilichukuliwa nje" nikasema (kwa Mtume (ﷺ)) "Kwa nini hujishughulishi na Nashra?" Alisema, "Allah ameniponya; Sipendi kuruhusu uovu uenee kati ya watu wangu. "
حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عُيَيْنَةَ، يَقُولُ أَوَّلُ مَنْ حَدَّثَنَا بِهِ ابْنُ جُرَيْجٍ، يَقُولُ حَدَّثَنِي آلُ، عُرْوَةَ عَنْ عُرْوَةَ، فَسَأَلْتُ هِشَامًا عَنْهُ فَحَدَّثَنَا عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ قَالَتْ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم سُحِرَ حَتَّى كَانَ يَرَى أَنَّهُ يَأْتِي النِّسَاءَ وَلاَ يَأْتِيهِنَّ‏.‏ قَالَ سُفْيَانُ وَهَذَا أَشَدُّ مَا يَكُونُ مِنَ السِّحْرِ إِذَا كَانَ كَذَا‏.‏ فَقَالَ ‏"‏ يَا عَائِشَةُ أَعَلِمْتِ أَنَّ اللَّهَ قَدْ أَفْتَانِي فِيمَا اسْتَفْتَيْتُهُ فِيهِ، أَتَانِي رَجُلاَنِ فَقَعَدَ أَحَدُهُمَا عِنْدَ رَأْسِي، وَالآخَرُ عِنْدَ رِجْلَىَّ، فَقَالَ الَّذِي عِنْدَ رَأْسِي لِلآخَرِ مَا بَالُ الرَّجُلِ قَالَ مَطْبُوبٌ‏.‏ قَالَ وَمَنْ طَبَّهُ قَالَ لَبِيدُ بْنُ أَعْصَمَ، رَجُلٌ مِنْ بَنِي زُرَيْقٍ حَلِيفٌ لِيَهُودَ، كَانَ مُنَافِقًا‏.‏ قَالَ وَفِيمَ قَالَ فِي مُشْطٍ وَمُشَاقَةٍ‏.‏ قَالَ وَأَيْنَ قَالَ فِي جُفِّ طَلْعَةٍ ذَكَرٍ، تَحْتَ رَعُوفَةٍ، فِي بِئْرِ ذَرْوَانَ ‏"‏‏.‏ قَالَتْ فَأَتَى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم الْبِئْرَ حَتَّى اسْتَخْرَجَهُ فَقَالَ ‏"‏ هَذِهِ الْبِئْرُ الَّتِي أُرِيتُهَا، وَكَأَنَّ مَاءَهَا نُقَاعَةُ الْحِنَّاءِ، وَكَأَنَّ نَخْلَهَا رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ ‏"‏‏.‏ قَالَ فَاسْتُخْرِجَ، قَالَتْ فَقُلْتُ أَفَلاَ أَىْ تَنَشَّرْتَ‏.‏ فَقَالَ ‏"‏ أَمَا وَاللَّهِ فَقَدْ شَفَانِي، وَأَكْرَهُ أَنْ أُثِيرَ عَلَى أَحَدٍ مِنَ النَّاسِ شَرًّا ‏"‏‏.‏
HADITHI : Sahih al-Bukhari 5765
KITABU CHA : KITABU CHA 76, HADITHI 79
TAZAMA TOLEO : LA. 7, KITABU CHA 71, HADITHI 660
REJEA TENA HAPA NABII WA MUNGU HAWEZI KULOGWA ILA MUHAMMAD ALIROGWA AKAWA ANAITA OVYO NA AKAWA ANAONA ANAFANYA MAPENZI KUMBE ANAJIFANYA YEYE BILA KUWA NA MKEWE 😂😂
Hadithi ya Aisha (r.a) amesema Mtume (s.a.w) alirogwa, mpaka akawa anaona kama anawaingilia wakeze na hali ya kuwa hawaingilii sufiyan mmoja wa wapokezi wa hadhithi hii amesema ndiyo uchawi mbaya mno unapokuwa namna hivi… (Alu-lu-lu wal-marjan, uk 822, hadithi na. 1412
➖➖➖➖➖➖➖➖
NJOO TENA HAPA MUHAMMAD SWT BAADA YA KUROGWA ALICHANGANYIKIWA AKAWA ANAITA OVYO OVYO
Anasema Mwana Aisha Mkewe Mtume (r.a) kuwa:"Yahudi mmoja aitwaye Labiid bin Al'aanswam alimroga Mtume (s.a.w) ikawa Mtume baadhi ya nyakati huchanganyikiwa akiita ovyo ovyo." (Sahih Muslim,Juzuu ya 4,uk.38-39)
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
REJEA TENA HAPA ALLAH ALIPOZIDIWA UJUZI NA HUYU MYAHUDI AKATAREMSHA AYA HII HAPA😂😂
✔Quran 5:51. Enyi mlio amini! Waislamu Msiwafanye #Mayahudi na #Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
REJEA TENA HAPA MUHAMMAD ALISEMA NIMEKUWA MWENDAWAZIMU
✔Quran 15: 6. Na walisema: Ewe Muhammad uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe Muhammad ni mwendawazimu.
REJEA HADITHI INASEMA HIVI
Muhammad akisema: O Khadija, Ninaona Mwanga, na nasikia Masautisauti, nina hofu kuwa mimi nina Wazimu. "Kitab al-Tabaqat al-Kabir", (Kitabu cha Madarasa Meja), na Ibn Sad, kutafsiriwa na S. Moinal Haq, [4], ukurasa wa 225.
➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖
REJEA HAPA NABII WA MUNGU HAWEZI KUROGWA WALA LAKINI MUHAMMAD ALIROGWA NA HAJUI AYA NGAPI NDANI YA QUR-AN YENU KUWA HIZI NI AYA ZA ALLAH NA HIZI NI ZA UCHAWI
✔(Hesabu 23:19-21,23, )
------------
19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
20 Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.
21 Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
23 Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana #uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
Shalom

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW