Tuesday, October 22, 2019

Je, Yesu Alitumwa kwa Israeli Peke Yake?

Image result for yesu kwa mataifa yote

Waislamu “wanahubiri” kuwa Yesu  hakuja kwa ajili ya ulimwengu wote bali alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao. Kisha wanasema kuwa Muhammad ndiye mtume sahihi kwa sababu huyo alikuja kwa ajili ya ulimwengu wote. Andiko wanalotumia kupinga utume wa Yesu kwa ulimwengu ni lile alilolisema Yesu wakati akiongea na mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi), ambaye alikuwa anaomba Yesu amponye mwanawe.

Imeandikwa:
Akajibu akasema,  Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:26).


Mungu ni Mungu wa utaratibu na ratiba kamili. Ndiyo maana hakuumba kila mtu kwa mara moja. Alianza na mtu mmoja tu, kisha wengine wote tukatokea kwa huyo mtu. Vivyo hivyo, alianza kwa kujifunua kwa taifa moja tu duniani kote. Kisha kutokea hapo ndipo wokovu unasambaa kwenye mataifa yote. Ni ukweli ulio wazi kwamba, ukiacha Israeli, jamii zote zilizobakia duniani, kwa asili zilikuwa zikiabudu miungu (yaani mashetani). Ni Israeli peke yao ndio ambao kwa asili walianza na Mungu wa kweli.

Ndiyo maana Bwana Yesu alipoongea na mwanamke Msamaria pale kisimani alimwambia hivi:

Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. (Yohana 2:22).


Wokovu unatoka kwa Wayahudi kwa sababu hakuna taifa jingine lolote duniani ambalo lilimjua Mungu wa kweli – yote yalikuwa na dini za kipagani – iwe ni wazungu, Waafrika, Wahindi, Waarabu, n.k. Huo ndio ukweli.

Kusema kwamba Yesu hakuja kwa ajili ya mataifa yote hakuna tofauti na kusema kuwa, kwa vile Mungu alimuumba Adamu na Hawa peke yake, basi Yeye si wa familia yangu maana hakuniumba na mimi kama alivyomuumba Adamu.

Yesu aliongea na wanafunzi wake siku moja na akawaambia kuwa:

Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanzia tangu Yerusalemu. (Luka 24:46-47). 

Je, unaona kwamba Injili inatakiwa kuanzia Yerusalemu? Na je, unaona pia kwamba anasema kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake? Je, mataifa yote ni Israeli peke yake?

Mwanamke Mkananayo alikuja wakati usio wake. Huo ulikuwa ni wakati wa kuhubiri Injili kwa Israeli kwanza ndipo iende ulimwenguni kote.

Ufuatao ni ushahidi zaidi wa maneno ya Bwana Yesu mwenyewe kuthibitisha kwamba alitumwa kwa mataifa yote ulimwenguni na kwamba Yeye ndiye Masihi wa Mungu, yaani aliyepakwa mafuta kwa Roho Mtakatifu kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu wote.

  • Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wotena Samaria, na hata mwisho wa nchi. (Matendo 1:8). 
  • Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu (Mathayo 28:19).
  • Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. (Yohana 3:17).
  • Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu. (Yohana 12:47).
  • Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. (Yohana 10:15-16).
  • Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. (Mat 24:14). 

Nihitimishe kwa kurejea tena mambo machache niliyoyasema. Mungu amekuwa na kawaida ya kuanza jambo na mtu mmoja.

  • Aliumba mwanadamu mmoja, kisha tukatokea humo wote.
  • Alijifunua kwa taifa moja, kisha tukamjua wote.
  • Alianza na Mwana mmoja (Yesu), kisha tunazaliwa wote kwa imani katika huyo.
  • Vivyo hivyo, alileta wokovu kwa taifa moja la Israeli, kisha unasambaa kote – ndiyo maana anasema na mwanamke Msamaria pale kisimani – “Wokovu watoka kwa Wayahudi.” (Yohana 4:22).


Hali hii ya kuanza na mtu au sehemu moja, ni ushahidi kuwa wale wote wanaojifariji kwa maneno eti “dini mbalimbali ni njia tofauti ambazo zote zinaishia kwa Mungu”, wanajidanganya na kupoteza muda wao na uzima wao wa milele! “Wokovu watoka kwa Wayahudi” – yaani KWA YESU PEKEE!

Sasa, kwa kuwa muda wa kusambaa kwa wokovu huo ulikuwa haujatimia (maana Mungu anakwenda kwa ratiba ya majira na nyakati), ndiyo maana akamwambia yule mwanamke Mkananayo (yaani asiye Myahudi) kuwa hakutumwa ila kwa Israeli.

Lakini utimilifu wa majira ulipofika, yaani alipokufa na kufufuka, tunaona akiwaagiza sasa mitume wake waende ulimwenguni kote.

Na Biblia inasema wazi: Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu dunianiLakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. (Waefeso 2:11-16).


Tafakari

Hoji mambo

Jiulize

Chukua hatua

Je, Yesu alisema kuwa Yeye ni Mungu?

Image result for Who is Jesus

“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!

Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.”

Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).


Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.
  

Ufuatao ni ushahidi wa kibiblia kwamba YESU KRISTO  ni Mungu.

Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.
NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).

Mwanadamu yuko kwa sababu Mungu alisababisha awepo. Gari liko kwa sababu injinia au mbunifu alisababisha liwepo. Nyumba ipo kwa sababu fundi alisababisha iwepo. Lakini Mungu YEYE YUKO TU!! Hayupo kwa kusababishwa na yeyote! Ndiyo maana akasema MIMI NIKO AMBAYE NIKO! Yesu ni NIKO. Kwa hiyo, Yeye ni Mungu.

Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
Waislamu wana msemo wao kwamba eti, Yesu na Mungu ni wamoja katika malengo, si katika asili yao. Basi huwa nawauliza swali kuhusu aya ifuatayo ya Isaya, nao wanazimika na kukosa jibu:

Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu MTOTO amezaliwa, Tumepewa MTOTO MWANAMUME; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE, Mfalme wa amani.

Aya hii iko wazi kabisa. anayetajwa ni Yesu kwamba Yeye ni Mungu mwenye nguvu.


Yohana 14:9
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

Maneno haya Yesu aliyasema baada ya kuulizwa swali lililo wazi kabisa, ambalo lilikuwa na lengo la kumjua MUNGU BABA! Imeandikwa: 
Filipo akamwambia, Bwana, UTUONYESHE BABA, yatutosha.  Ndipo Yesu akajibu waziwazi: ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA. Maana yake ni kuwa, “Mimi ndio Baba mwenyewe.”

Ufunuo 1:17 na Ufunuo 22:13
Mimi ni wa kwanza na wa mwisho
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

Ni Mungu TU ndiye mwenye uwezo wa kuwa wa kwanza na wa mwisho; Yesu ni Alfa na Omega. Kwa hiyo Yeye ni Mungu.

Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye NENO ALIKUWA MUNGU.
Andiko hili Waislamu hawalipendi kabisa. ni kwa sababu liko wazi mno. Yesu ni Neno; na Neno ni Mungu; hivyo, Yesu ni Mungu!
Yohana 20:28
Tomaso akajibu, akamwambia, BWANA WANGU NA MUNGU WANGU!
Tomaso aliposema hivi, Bwana Yesu hakukanusha na kusema, “Mimi sio Mungu.” Badala yake: Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. (Yoh 20:29). 


Matendo 20:28
Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, ALILOLINUNUA KWA DAMU YAKE MWENYEWE.

Ni Mungu gani mwenye damu huyu? Jibu liko wazi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ndiye aliyetoa uhai wake na kumwaga damu yake msalabani; na hapo ndipo alipoanzisha Kanisa.

Wakolosai 1:16
Kwa kuwa KATIKA YEYE VITU VYOTE VILIUMBWA, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.

Katika Yeye Yesu vitu vyote viliumbwa. Ina maana kuwa vitu vyote vilitokana na Yesu; maana Yesu ni Neno la Mungu. Na tunajua kuwa Muumba wa vitu vyote ni Mungu; hivyo, Yesu ni Muumba – Yeye ni Mungu!!

Wakolosai 2:9
Maana KATIKA YEYE UNAKAA UTIMILIFU WOTE WA MUNGU, kwa jinsi ya kimwili.

Sisi sote ni watu wasio wakamilifu. Tunaanguka tena na tena kwenye dhambi. Kwa hiyo, hakuna mwanadamu wa kawaida ambaye anaweza kujigamba kwamba yeye ametimia kama alivyo Mungu. Lakini katika Yesu “utimilifu WOTE wa Mungu unakaa.” Kwa nini? Kwa sababu Yeye ndiye Mungu huyohuyo.

1Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.


Ni Mungu gani aliyedhihirishwa katika mwili? Jibu liko wazi. Ni Yesu Kristo peke yake.

Tito 2:13
….tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU

Yesu Kristo ni Mungu Mkuu!!

Shida KUU ya Waislamu ni hii: Wanampima Mungu kwa vigezo vya kibinadamu. Mungu anasema: Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? (Yer 32:27) 

Jibu liko wazo. HAKUNA!
Lakini utakuta Waislamu wanauliza maswali ya ajabu sana. Eti, kama Yesu ni Mungu, wakati amekufa, nani alikuwa anaangalia dunia?

Hili ni swali linalofaa kuulizwa juu ya kiumbe. Kama tungesema kuwa mwanadamu fulani alikuwa amekufa, ndipo kuna mantiki kuuliza kwamba, wakati amekufa nani alikuwa anatunza familia yake? Maana hili ni swali linalohusu tabia za kibinadamu kwa kuwa mwanadamu hawezi kuwa mahali kuwili au zaidi kwa pamoja. MUNGU SI MWANADAMU! ANAWEZA YOTE – NA HASA MUNGU WA IBRAHIMU, ISAKA NA YAKOBO!

YESU NI MUNGU MILELE NA MILELE!!

HALELUYA!!

Tafakari

Hoji mambo

Chukua hatua!

YESU NI NENO

No photo description available.
Kwa kawaida, maneno “Neno la Mungu” yanawakilisha ujumbe kutoka kwa Mungu au mkusanyo wa ujumbe huo au Yesu ambaye ni Neno. (Luka 11:28) Katika sehemu chache, “Neno la Mungu” au “Neno” hutumiwa kumwakilisha Yesu.​—Ufunuo 19:13; Yohana 1:​14.
Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!
Ujumbe kutoka kwa Mungu. Mara nyingi manabii walisema kwamba ujumbe ambao walitoa ulikuwa Neno la Mungu. Kwa mfano, Yeremia alianza ujumbe wake wa kinabii kwa kusema “Neno la Yehova likaanza kunijia.” (Yeremia 1:4, 11, 13; 2:1) Kabla ya kumwambia Sauli kwamba Mungu alikuwa amemchagua kuwa mfalme, nabii Samweli alisema hivi: “Simama tuli sasa ili nikuambie Neno la Mungu.”​—1 Samweli 9:27.
Pia “Neno” linaonekana katika Biblia likiwa ni Yesu Kristo, akiwa Roho mbinguni na pia akiwa Mwanadamu duniani. Fikiria sababu kadhaa za kufikia mkataa huo:
Neno aliishi kabla ya vitu vingine vyote kuumbwa. “Hapo mwanzo Neno alikuwako . . . Hapo mwanzo huyo alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.” (Yohana 1:1, 2,3).
Neno alikuja duniani. “Neno akawa mwili, akakaa katikati yetu.” (Yohana 1:14) Kristo Yesu “alijiondolea mwenyewe hali yake na kuchukua umbo la mtumwa na kuwa kama wanadamu.”​—Wafilipi 2:5-7.
Neno ni Mungu. Baada ya kusema kwamba “Neno akawa mwili,” kama ilivyonukuliwa hapo juu, mtume Yohana aliendelea kusema hivi: “Nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule ulio wa Mwana mzaliwa-pekee kutoka kwa Baba.” (Yohana 1:14) Pia, Yohana aliandika hivi: “Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”​—1 Yohana 4:15.
Neno ana sifa za Mungu. “Neno alikuwa Mungu.” (Yohana 1:1) Yesu “ndiye mng’ao wa utukufu [wa Mungu] na mwakilisho sawasawa wa utu wake wenyewe.”​—Waebrania 1:2, 3.
Neno anatawala akiwa mfalme. Biblia inasema kwamba kwenye kichwa cha Neno la Mungu “kuna vilemba vingi.” (Ufunuo 19:12, 13) Neno anaitwa pia “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.” (Ufunuo 19:16) Yesu anaitwa “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”​—1 Timotheo 6:14, 15.
Neno ni Mungu. Inaonekana kwamba jina “Neno” linamtambulisha Yesu. Yesu alisema kwamba alitimiza jukumu hilo: “Baba mwenyewe aliyenituma amenipa amri kuhusu jambo la kutangaza na la kusema. . . . Kwa hiyo mambo ninayosema, kama vile Baba alivyoniambia, ndivyo ninavyoyasema.”​—Yohana 12:49, 50.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

Wednesday, August 7, 2019

UTATU UNATHIBITISHWA KWA AYA NA HISABATI

Tuanze kwa kusoma aya :
1 Yohana 5:7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. 

Aya ya Biblia inasema ifuatavyo:

WAKO WATATU: 1 + 1 + 1 = 3
1. Baba
2. Neno - Yesu
3. Roho Mtakatifu
Hawa Watatu wanashuhudia Mbinguni.

HAWA WATATU NI UMOJA: 1 * 1 * 1 = 1

MUNGU NI WA MILELE: 
∞ INFINITY

Zaburi 90: 2 inatuambia kuhusu uzima wa milele wa Mungu: "Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu." Kwa kuwa wanadamu hupima kila kitu kwa wakati, ni vigumu sana kwetu kumpata mimba Ya kitu ambacho hakina mwanzo, lakini kimekuwa, na kitaendelea milele.


1. Baba ni wa Milele: Hana Mwanzo wala Mwisho 
2. Mwana ni wa Milele: Hana Mwanzo wala Mwisho 
3. Roho Mtakatifu ni wa Milele: Hana Mwanzo wala Mwisho 

YESU NI WA MILELE 
Yesu Kristo, Mungu wa mwili, pia alithibitisha uungu Wake na uzima wake wa milele kwa watu wa siku yake kwa kuwaambia, "Kabla Ibrahimu hajazaliwa, mimi ni" (Yohana 8:58). Ni wazi kwamba Yesu alikuwa akidai kuwa Mungu kwa mwili kwa sababu Wayahudi, waliposikia maneno hayo, walijaribu kumtupa kwa mawe. Kwa Wayahudi, kujitangaza kuwa Mungu wa milele kulikufuru na kustahili kifo (Mambo ya Walawi 24:16). Yesu alikuwa akidai kuwa ni wa milele, kama Baba yake ni milele. Mtume Yohana pia alitangaza ukweli huu kuhusu hali ya Kristo: "Katika mwanzo kulikuwa Neno, na Neno lilikuwa pamoja na Mungu, naye Neno lilikuwa ni Mungu" (Yohana 1: 1). Yesu na Baba yake ni moja kwa moja, wanapo bila muda, nao wanagawana sawa katika sifa ya milele.

ROHO MTAKATIFU NI WA MILELE 
Roho wa Mungu / Bwana / Kristo: (Mathayo 3:16, 2 Wakorintho 3:17, 1 Petro 1:11) Majina haya yanatukumbusha kwamba Roho wa Mungu ni kweli sehemu ya Mungu wa Utatu na kwamba Yeye ni sawa sawa na Mungu kama Baba na Mwana. Anatufunuliwa kwa kwanza wakati wa uumbaji, wakati "akitembea juu ya maji," akiashiria sehemu yake katika uumbaji, pamoja na ile ya Yesu ambaye "alifanya vitu vyote" (Yohana 1: 1-3). Tunaona Utatu huo wa Mungu tena wakati wa ubatizo wa Yesu, wakati Roho akishuka juu ya Yesu na sauti ya Baba inasikika.

SASA TUFANYE HISABATI:
Umilele katika Mahesabu au Hisabati unashika na au onyeshwa kwa alama hii 
∞. Kwa Kiingereza wanasema in "INFINITY"

Tukitumia Hisabati ya kawaida kabisaa utaona ∞ + ∞ + ∞ = ∞
BABA ∞ + MWANA ∞ + ROHO MTAKATIFU ∞ = ∞

1 + 1 + 1 = 3 Wapo Watatu wanao shuhudia Mbinguni: There are THREE that bear witness in heaven.

1 X 1 X 1 = 1 Hawa Watatu ni Umoja: These THREE ARE ONE

∞ + ∞ + ∞ = ∞
Mungu Baba hana Mwanzo wala Mwisho: The Father has no beginning or the end= ETERNAL=∞
Neno-Yesu hana Mwanzo wala Mwisho: 
The Word "Jesus" has no beginning or the end= ETERNAL= ∞

Roho Mtakatifu hana Mwanzo wala Mwisho: The Holy Spirit has no beginning or the end= ETERNAL= ∞

Sasa naiweka tena aya:
1 Yohana 5:7  Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.  For there are three that bear witness in heaven: the Father, the Word, and the Holy Spirit; and these THREE ARE ONE. ~ 1 John 5:7

NATUMIA KUJUMLISHA KWA KIZIO CHA TATU:

Kuhusu swala la UTATU, Linahusisha NAMBA TATU na hivyo sheria yake lazima iwe ya "TERNARY ADDITION" na sio "BASE TEN ADDITION" kama wengi wenu mnao tumia hiyo hesabu bila ya hata kufahamu kuwa addition yenu MNATUMIA SHERIA YA "BASE TEN" .

SASA NINI MAANA YA TERNARY ADDITION:

1. Ternary namba inatumia BASE 3, tofauti na BASE 10 ambayo mkihesabu na kufikia namba 9, unarudi kwenye 1 na kuongeza "SIFURI" = 10. SASA, katika Ternary addition, unapo hesabu namba mwisho wako ni NAMBA MBILI na inayo fuata ni 10, kama kwenye "BINARY ADDITION" namba yako ya mwisho ni MOJA http://www.allaboutcircuits.com/…/d…/chpt-2/binary-addition/ .
Ninafahamu wengi wenu labda hamjawai soma Hesabu za juu na mnaweza pata walakini, lakini ingia hapa na ujifunze mwenyewe Ternary addition 
http://homepage.cs.uiowa.edu/~jones/ternary/arith.shtml

SASA TUANZE KUTHIBITISHA UTATU WA MUNGU KWA KUTUMIA HESABU

MSINGI WA TERNARY ADDITION UNATUMIKA:

A. (1 + 1 + 1) Ternary = 10 Ternary

UNAONA JAWABU LAKO NI Ternary (10)

SASA namba zetu tumesha zipunguza na kufikia Tenary 10. Ikiwa na maana kuwa, MSINGI UNAO FUATA NI KUZIJUMLIZA HIZO NAMBA " DIGITS MBILI ZA MOJA NA SIFURI KWA KUTUMIA msingi ule ule wa Ternary addition.

B. (1 + 0) Ternary = 1 Ternary.

SASA TUMESHA PATA JIBU LETU KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA KWA KUTUMIA HISABATI, na leo nimewajibu wale wote ambao HESABU SIO SOMO LAO KUWA UTATU UNAJIBIKA HATA KWA KUTUMIA HISABATI.

SASA NENDA KAMUULIZE MKUFUNZI WAKO WA HISABABI YAFUATAYO:

A. Ternary ya (1 + 1 + 1 ) = ?

B. Ternary ya ( 1 + 2) = ?

UKISHA PEWA JIBU MUULIZE TENA HUYO MKUFUNZI WAKO
C. Ternary ya (1 + 0 ) = ?

HAKIKA MUNGU NDIE MWANZILISHI WA HISABABTI na hakuna asilo liweza.

Mungu awabariki sana, na leo UMESHA JIBIWA KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA HATA KWENYE HISABATI.

KURIDHIKA NA YALE TULIYOFUNULIWA .

A. BABA anaitwa MUNGU ( 1 WAKORINTHO 8:6 ).

B. MWANA ( YESU ) anaitwa MUNGU ( ISAYA 9:6; YOHANA 20:26-29 ).

C. ROHO MTAKATIFU anaitwa MUNGU ( MATENDO 5:3-4 )
Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1 na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza. Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.

Shalom

Max Shimba bond-servant of Jesus Christ Mighty God. Titus 2:13



TRINITY



HOW COMPLEX IS TRINITY?

 
1 + 1 + 1 = 3 There are THREE that bear witness in heaven.

1 X 1 X 1 = 1 These THREE ARE ONE

∞ + ∞ + ∞ = ∞
The Father has no beginning or the end= ETERNAL=∞
The Word "Jesus" has no beginning or the end= ETERNAL= ∞
The Holy Spirit has no beginning or the end= ETERNAL= ∞

For there are three that bear witness in heaven: the Father, the Word, and the Holy Spirit; and these THREE ARE ONE. ~ 1 John 5:7

Shalom

Max Shimba bond-servant of Jesus Christ Mighty God. Titus 2:13



WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW